Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

تجريبي
Anonym
/ Categories: Main_Category

تجريبي

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu, Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Mheshimwa Papa Farnsis / Papa wa Vatikani

Waheshimiwa wanaohudhuria, nakuamkieni kwa maamkio ya Uislamu:

Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakaatuh

Amani iwe kwenu na rehema za Mwenyezi Mungu na Baraka zake.

Al-Azhar Al-Sharif na Baraza la Wazee la Kiislamu wanakuamkieni, tena wanakushukuru sana kutoka moyoni kwa kuitikia mwaliko, na sisi tunathamini ziara yenu ya kihistoria kwa Misri na Al-Azhar Al-Sharif, ziara hii yenye kuitikia mwaliko wa Al-Azhar inatekeleza jukumu la kihistoria tunalolibeba sisi sote, licha ya kushirikiana na Wakuu wa Dini za Kimbinguni na Maulamaa wake na watu wake, kwa ajili ya amani ipoteayo inayotafutiwa na watu, nchi, maskini, wagonjwa, wanaopotea nyusoni jangwani, na wanatoroka nchi zao kwa nchi nyingine zilizo ni mbali, ambao hawajui kama watazifikia nchi hizo au hawatazifikia kwa sababu ya mauti na maangamizo na kuzama na vipande vya mwili vya wanadamu wanaofiwa na maiti waliotupa vibaya miambao ya bahari, katika mateso ya kibinadamu yenye huzuni, sisi hatutavukia mipaka ya ukweli tukisema kwamba: mateso hayo haya mfano katika historia.

Na bado wenye busara na wenye dhamiri zenye uhai wanachunguza sababu ya kimantiki kwa mateso hayo, ambayo tanalipa thamani yake kubwa kutoka roho zetu na nchi zetu, basi wenye busara hao hawaipati sababu moja tu ya kimantiki, inayohalilisha kutokea kwa majanga haya ambayo yaliyafikia maeneo ya mafukara, mayatima, wajane na wazee, hawapati sababu isipokuwa biashara ya silaha na mauzo yake, na kudhamini kuendelea kazi za viwanda vya mauti, na utajiri kutokana na mauzo yasiyo na njia halali, na matumizi za kimataifa yasiyo na busara, na kuziumba maeneo ya mahangaiko na kuiwasha fitina za kidini na kuichochea ukabaila na utaifa, na hitilafu za madhehebu baina ya wana wa nchi moja, hayo yote kwa ajili ya kuyageuka maisha yao yawe yenye mateso yasiyo na mfano.

Miongoni mwa mambo yenye ushangaa kutokea kwa mzozo huu mkali katika karne ya 21, karne ya utamaduni na ustaarabu na haki za mwanadamu, na zama za maarifa ya hali  ya juu, na maendeleo ya kisayansi, na kiteknolojia, na pia ni zama za taasisi za amani ambazo zinzozihifadhi usalama na amani ya kimataifa, na mikataba yake inaharimisha kutumia nguvu, au hata kutishia mahusiano ya kimataifa. Zama hizi pia ni zama za madhehebu na falsafa ya za kibinadamu, na kubashiri kwa usawa usio na ukomo na jamii yenye tabaka moja, usasa usio na dini na mambo mengine mengi ya mafanikio hayo ya kijamii na kifalsafa inayosifiwa nayo zama yetu.

Na swali muhimu la kipenyo katika ushangaa huo ni kuwa: pamoja na mafanikio hayo makubwa, vipi amani ikawa kama Pepo iliyopotea? Na vipi zama hizi za haki za mwanadamu zinashuhudia kazi za ushenzi namna hii, ambazo hazitokee katika zama zilizotangulia? Nadhani jibu - na nyinyi mtaafikiana nami kuhusu jibu hili – ni kuwa: kutojali kwa utamaduni wa kisasa kwa Dini za kimbinguni, na misingi yake ya kimaadili inayo ni imara sana wala haibadiliki kwa mabadiliko ya manufaa na malengo, wala haibadiliki kwa utashi na matamanio. Msingi wa kwanza: ni undugu, na kujuana na kurehemiana baina ya watu, na kuwakumbusha watu kwamba viumbe vyote ni vya Mwenyezi Mungu, na anayependezwa zaidi miongoni mwao ni anyeweza kuwanufaisha wana wake, na hayo kwa ajili ya ulimwengu usigeukie msitu wa wanyama wakali wanaokula nyama za wao kwa wao..

Na kama wanavyosisitiza Maulamaa wenye kufikiri katika Magharibi na Mashariki; hauna ufumbuzi isipokuwa kurudia ufahamu na uelewano wa jumbe za mbingu, na kuweka mazungumzo yasiyonyooka katika wigo wa uchunguzi wa kimantiki unaookoa akili ya kibinadamu kwa yale yaliyoipata miongoni mwa ufukara wa falsafa ya kitendo na maana yake finyu, na kuvuka mipaka kwa akili wa kipekee yenye ujeuri na utawala mbaya maisha ya watu, na upande mwingine wanafalsafa na wanaoamini wanaona kwamba: hanabudi wala mahali pa kukimbilia ila kwa kurudia tena utaratibu wa hayo yote katika Muktadha wa undugu na rehema, na Muktadha huo ninaizingatiwa kama dawa inayofufua uhai katika madhehebu ya kifalsafa, na fremu za kielimu na kitendakazi zenye pamoja, na dawa hii haipatikani ila katika duka la dawa la dini pekee yake.

Na ninafikiri kwamba ardhi inatandika sasa ili dini zitekeleze mchango wake katika kubainisha maana ya amani, uadilifu na usawa, na kumheshimu mwanadamu bila ya kujali dini yake, rangi yake, ukoo wake na hugha yake, na katika Qurani Tukufu inayosomwa na Waislamu asubuhi na jioni; tunasoma kauli yake Mwenyezi Mungu: (Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba) {Al-Isra’, 70}.

Lakini kabla ya kufanya hayo, sisi tunalazimika tusafishe sura ya dini kutoka dhana zenye makosa na matendo yasiyo sahihi yanayoambatana nayo pamoja na kushikia dini kwa uwongo kunakowasha ugomvi na kunaeneza chuki, na kunahimiza ukatili .. wala hatuhukumu dini kwa halifu za wachache wapumbavu miongoni mwa wanaoamini dini hii au ile. Uislamu si dini ya ugaidi kwa sababu ya kundi moja linalouamini walikimbia haraka kuzifafanua baadhi ya maandiko yake kwa ufafanuzi wenye ujinga na ufisadi, kisha wakaelekea kumwaga damu, na wakaua nafsi, wakaasi katika nchi kwa uharibifu, na wanapata wanaowapa silaha na kuwazoesha namna ya kutumia kwake .. na Ukristo si dini ya ugaidi kwa sababu kundi moja linalouamini waliubeba msalaba na wakawa wanawaua watu bila ya kupambanua baina ya mwanamume, na mwanamke na mtoto, na mpigaji vita na mtekwa, Uyahudi si dini ya ugaidi kwa sababu ya kuyatumia mafunzo ya Musa A.S. - anatukuka kufanya hivyo - katika kuteka nchi kwa vitendo vilivyokuwa na wahanga mamilioni miongoni mwa watu wa Palestina wenye haki wasiomiliki amri wala utawala wao. Wala utamaduni wa Ulaya ni utamaduni wa ugaidi kwa sababu vita viwili vya dunia vilivyowaua zaidi ya 70 milioni, wala utamaduni wa Kimarikani ni utamaduni wa ugaidi wakati ambapo bomba zake ziliteketeza watu na mawe katika Heroshima na Nagazaki, mlango huu ukifuguliwa - kama ulifungulia dhidi ya Uisilamu sasa - haitasilimika dini wala mfumo wala historia kutoka tuhuma ya ukatili na ugaidi.

Ewe Mheshimiwa Papa! sisi tunayathaminisha sana maelezo yako yanayoinusuru haki, na yanautetea Uislamu dhidi ya tuhuma ya ukatili na ugaidi, na sisi tuliona uangalifu wenu na uangalifu wa Papa wote wa Makanisa ya Magharibi na Makanisa ya Mashariki kuheshimu itikadi na Dini na Wakuu wake, na kupambana na wanaozitia ubaya, na anayetumia ubaya huu katika kuwasha ugomvi baina ya Waumini..

Ndiyo! Al-Azhar ilifanya kazi na inaendelea kufanya kazi kwa ajili ya kusaidiana katika wito wa kuishi pamoja na kufufua mazungumzo, na kuheshimu itikadi za wengine, na kutozigusia, na kuchunguza mambo yenye ushirikiano baina yetu, na yale ni mengi sana, pia vipo vikwamizo vingi vinavyotupambana sisi ni viongozi wa dini.

Basi tufanye pamoja kwa ajili ya wanyonge, wenye njaa, wenye woga, mateka, na wenye mateso ardhini, bila ya ubaguzi wala usanifishaji wala kasumba.

Tufanye pamoja kuiokoa familia na yale yanayoitakia miongoni mwa maadili mbaya na utawala mbaya wa kisayansi, na kutotembea sawa kwa baadhi ya watafiti na matendo yao ovyo, na kuyaokoa kutoka mazingira ya ufisadi na wafisadi.

Tupambane pamoja na siasa zinazotawala vibaya, na Nadharia za: ugomvi wa kistaarabu, mwisho wa historia, wito wa ukafiri, mawazo ya Mikavilia, na usasa usio na dini, na yale yaliyotokana na hayo miongoni mwa mateso na majanga mahali po pote.

Na katika hitimisho la hutuba yangu namwelekea Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu Aujaalie mkutano huo ni hatua ya kweli tunaisaidiana nayo wote kueneza dhana ya amani, undugu na kuishi pamoja.

Asanteni sana,      

Assalaam Alaikum Warahmatullah Wabarakaatuh

 

Makao Makuu ya Al-Azhar.

2 mfunguo wa Shaabani Mwaka 1438. A.H.

28/4/2017A.D.

 

Imamu Mkuu

Sheikh wa Al-Azhar.

      

Print
5183 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.