Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Al-Azhar katika Maelezo yake Kuhusu Janga la Myanmar
Anonym
/ Categories: Main_Category

Al-Azhar katika Maelezo yake Kuhusu Janga la Myanmar

Kwa Jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

Al-Azhar katika Maelezo yake Kuhusu Janga la Myanmar

  • Waislamu wa Ruhinga wanakabiliwa na mashambulizi ya kinyama na ya kihuni ambayo hayakujulikanwa na utu hapo kabla.
  • Kufa kwa dhamira ya kimataifa ndiyo sababu ya tukio la kihuni na ya kinyama nchini Myanmar.
  • Mikataba yote ya kimataifa ambayo imeahidi kuzilinda haki za binadamu imekuwa ni wino tu kwenye karatasi, bali ni uongo.
  • Wanayokumbana nayo Waislamu wa Ruhinga yanatukumbusha mtindo wa kinyama porini mwituni.
  • Mashirika ya kimataifa yangechukua msimamo mwengine kama kundi la watu hawa wangekuwa ni wafuasi wa dini yoyote au imani yoyote isiyokuwa ya Kiislamu.
  • Viongozi wa kidini nchini Myanmar wamezipiga na vikuta juhudi za Al-Azhar na wakaungana na makundi ya watu wenye itikadi kali katika jeshi la taifa lenye kubeba silaha ili kutekeleza operesheni za mauaji ya makundi kwa makundi.
  • Mauaji ya kimbari dhidi ya wananchi Waislamu yataweka usajili wa fedheha katika historia ya Myanmar ambayo haitafutwa na wakati wala zama.
  • Al-Azhar Al-Sharif haiwezekani isimame ikikunja mikono mbele ya ukiukwaji huu wa haki za binadamu.
  • Al-Azhar itaongoza harakati za kiutu kwa ngazi ya Kiarabu, Kiislamu na kimataifa ili kusitisha mauaji haya.
  • Mfano wa uhalifu huu unachochea kutenda uhalifu wa ugaidi ambao unausumbua utu wote kwa ujumla.
  • Tunatolea ukelele wa kiutu ukitoa sauti ya kutaka kusitishwa siasa za ubaguzi wa rangi au kabila au kidini kati ya wananchi.
  • Tunasikitika kutokana na msimamo unaopingana na mwenye kubeba tuzo ya “Nobel” ya amani kwa mkono wake mmoja, huku mkono mwengine akiubariki kwa uhalifu ambao unaiwacha “amani” ikivurumishwa na upepo.

Taarifa kutoka kwa Al-Azhar Al-Sharif

Siku kadhaa zilizopita ulimwengu umefuatilia taarifa zilizosambazwa na vyombo vya habari na tovuti za kijamii miongoni mwa picha za kufadhaisha na kutisha za mauaji, uhamishaji, uchomaji moto, mauaji ya kimbari, na mauaji ya kinyama ambayo mamia ya kina mama, watoto, vijana na vikongwe wamepoteza maisha yao wakiwa wamezingirwa katika jimbo la Rakhin nchini Myanmar. Utawala nchini humo umewalazimisha kuzikimbia nchi zao chini ya mbinyo wa mashambulizi ya kinyama na kishenzi ambayo historia ya utu haikuwahi kuyajua hapo kabla. Wamo miongoni mwa raia hao waliokufa kutokana na maumivu ya kutembea na ukali wa njaa, kiu na jua lenye kubabua. Miongoni mwao wamemezwa na mawimbi baada ya kukimbilia kuipanda bahari.

Tukio hili la kishenzi na ambalo si la kibinadamu lisingetokea lau kama si kufa kwa dhamira ya kimataifa, na kufa watu wake, na kufa kwa maana zote za maadili ya kiutu. Kwa kufa kwake huko zikanyamaza sauti za uadilifu, uhuru na haki za binadamu kimya cha makaburi. Mikataba yote ya kimataifa ambayo imewekwa kwa ajili ya kuzihami na kuzilinda haki za binadamu, amani ya raia na haki zake za kuishi katika nchi zao zote hizo zikawa ni wino kwenye karatasi, bali zikawa ni uongo usio na thamani wala haustahiki thamani ya wino ulioandikiwa.

Hayo, hayakuwa yakitosha kwa kulaani tu na wala hakuna manufaa yoyote mbele ya yale yanayowakumba Waislamu wa Ruhinga kutokana na mauaji ya makundi kwa makundi kwa mtindo wa khiyana. Mtindo huu unatukumbusha unyamapori wa mwituni. Kama ambavyo maombi ya kutahayari ya mara kwa mara ambayo yanatolewa na mashirika ya kimataifa na ya kiutu kwa ajili ya kuwaokoa wananchi Waislamu kutokana na uadui wa jeshi la Burma na utawala wa Myanmar, kusihi huku kumekuwa ni pigo lisilo na maana na kupoteza wakati. Sisi tuna yakini kwamba mashirika haya ya kimataifa yangechukua msimamo mwengine tofauti kabisa na wenye nguvu na wa haraka kama kundi hili la wananchi lingekuwa ni Mayahudi au Wakristo au Mabuda au wafuasi wa dini au imani nyengine yoyote isiyokuwa ya Kiislamu.

Al-Azhar Al-Sharif kwa kushirikiana na Baraza la Wazee wa Busara wa Waislamu wamehangaikia kuwakusanya waliotengana na kuzozana, na kuiweka karibu mitazamo yenye migogoro katika jimbo la Rakhin wakati ilipowaalika idadi kadhaa ya viongozi vijana wanaowakilisha dini zote na makabila yote nchini Myanmar mwanzoni mwa mwaka huu jijini Kairo. Walikuwepo miongoni mwao watawa wa Kikristo na viongozi wa dini. Hayo yalikuwa ni hatua ya kwanza ya kuliweka suala hilo kwenye njia ya amani. Isipokuwa baadhi ya viongozi wa kidini nchini Myanmar wamezipiga na vikuta juhudi hizi, na kuiruhusu dhamira yao ya kuungana pamoja na makundi yenye itikadi kali kutoka jeshi la nchi hiyo lenye kubeba silaha ili kufanya mauaji ya kimbari na makundi kwa makundi na safishasafisha dhidi ya wananchi Waislamu katika unyama ambao utu haukuwahi kuyajua. Msimamo huu ambao unakataliwa na dini zote utaandika mistari ya usajili wa fedheha katika historia ya Myanmar. Historia ambayo haitafutwa na zama wala dahari.

Kuanzia na jukumu la kidini na la kiutu la Al-Azhar Al-sharif na kuufuata ujumbe wake wa kimataifa haiwezekani kusimama ikiwa imekunja mikono mbele ya ukiukwaji huu wa haki za binadamu. Na Al-Azhar Al-Sharif itaongoza harakati za kiutu kwa ngazi ya Kiarabu, Kiislamu na kimataifa ili kukomesha mauaji haya ambayo wananchi Waislamu pekee nchini Myanmar ndio wanaolipa thamani. Al-Azhar hivi sasa inazitaka kamisheni zote na mashirika yote ya kimataifa pamoja na jumuiya za haki za binadamu ulimwenguni kote kusimamia wajibu wake katika kuchukua hatua za lazima ili kufanya uchunguzi katika mauaji haya mabaya na kuwachukulia hatua wahalifu wake na kuwafikisha katika mahakama ya uadilifu ya kimataifa ili kuwahukumu kuwa ni wahalifu wa kivita kama ni sehemu ya waliyoyatenda katika maovu na unyama.

Inawapasa watu wote kuchukua mazingatio kwamba mfano wa uhalifu huu ni moja ya sababu kubwa ambazo zinachochea kufanyika uhalifu wa ugaidi ambao utu unasumbuliwa nao.

Kuanzia hapa, kutoka nchini Misri ambayo ni moyo wa Uarabu na Uislamu na Al-Azhar Al-Sharif tunatoa ukelele wa kiutu ukitaka kuchukuliwa hatua za haraka na Jumuiya ya Mataifa ya Kiarabu, Jumuiya ya Mashirikiano ya Kiislamu (OIC), Umoja wa Ulaya na Umoja wa Mataifa, khasa Baraza la Usalama. Na kabla ya hayo, kuchukuliwa hatua na watunga sheria katika mataifa ya Kiarabu na Kiislamu kwa kutoa juhudi zao kwa kadiri ya wanavyoweza ili kutoa mbinyo wa kisiasa na kiuchumi ambao utawarejesha nyuma watawala nchini Myanmar kuelekea katika kwenye uongofu na kusitisha siasa za ubaguzi wa rangi na wa kidini kati ya wananchi.

Al-Azhar haitasahau kutangaza masikitiko yake kwa msimamo unaopingana na ambaye anabeba tuzo ya amani “Nobel” kwa mkono mmoja, na mkono mwengine anaubariki kwa uhalifu ambao unaiweka “amani” ikipeperushwa na upepo na kuifanya kuwa ni “tamko tu” lisilokuwa na maana yoyote.

Mwisho, tunasema kuwaambia ndugu zetu nchini Burma .. kuweni thabiti katika kuukabili uadui huu mbaya kabisa. Na sisi tuko pamoja nanyi na wala hatutakuacheni mkono. Na Mwenyezi Mungu ndiye atakayekunusuruni. Jueni ya kwamba Mwenyezi Mungu hayafanikishi matendo ya waovu na mafisadi. Hivyo, (Na wanaodhulumu  watakuja jua mgeuko gani watakaogeuka).

 

Wassalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh.

Imetolewa tarehe: 17 Dhul-hijjah, mwaka 1438 A.H.

Sawa na tarehe: 8 Septemba, mwaka 2017 A.D.

 

Ahmad Al-Tayyib

Sheikh wa Al-Azhar

Print
5304 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.