Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Hotuba ya Mheshimiwa Imamu MkuuKatika Mkutano wa Ofisi ya Mufti ya Misri (Mchango wa Fatwa katika Utulivu wa Jamii Mbalimbali)
Anonym
/ Categories: Main_Category

Hotuba ya Mheshimiwa Imamu MkuuKatika Mkutano wa Ofisi ya Mufti ya Misri (Mchango wa Fatwa katika Utulivu wa Jamii Mbalimbali)

 

 

 

 

 

 

 

Hotuba ya Mheshimiwa Imamu Mkuu

Profesa Ahmad Al-Tayyib

Sheikh wa Al-Azhar

 

 

Katika Mkutano wa Ofisi ya Mufti ya Misri

Chini ya Anwani

Mchango wa Fatwa katika Utulivu wa Jamii Mbalimbali

 

Katika Hoteli ya Al-Maasa – Madenat Nasr - Kairo

 

Katika Kipindi cha: 26 – 28 Muharram 1439 A.H.

17 – 19 Oktoba 2017 A.D.

 

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu

 

Shukurani za dhati ni za Mwenyezi Mungu. Sala, amani na baraka zimshukie Bwana Mtume Muhammad, watu wake, na Masahaba zake wote.

Waheshimiwa Maimamu wa Utoaji Fatwa na Wasomi!

Ndugu Mliohudhuria!

Assalamu Alaikum Warahmatullahi Wabarakatuh…. Baada ya hayo:

Nina furaha kukualikeni Waheshimiwa - pamoja na ndugu yangu mtukufu Profesa Shauqy Allam, Mufti wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri - katika nchi yenu ya Misri, chimbuko la staarabu, ardhi ya Mitume, makutano ya Dini mbalimbali, na mji wa Al-Azhar Al-Sharif, ambayo ni ngome na kibla cha akili za Waislamu Mashariki na Magharibi.

Karibuni sana mbele ya jamaa zenu, ndugu zenu na wenzenu..

Hivyo, nawaombeni mniruhusu - enyi Waheshimiwa! Nifupishe hotuba yangu mbele yenu kuhusu kuzungumzia masuala ya fatwa, kwa utafiti wa kiakademia wa kisasa, sawa kwa yale yanayohusiana na uitikiaji wa fatwa za kisheria kwa mahitaji ya jamii, au kuchangia na kusaidia kurahisisha maisha ya watu na hali zao, au kuzizoeza fatwa hizo na kuziteremsha kwenye uhalisia na mabadiliko mapya mapya yanayojitokeza… hadi mwisho wa masuala yenye silka ya utafiti wa Fiqhi, na ambayo ninakumbuka kwamba nimeonesha upande wake fulani katika mkutano wa mwaka jana uliohusiana na vurugu za ndoa na vurugu za talaka, na mambo ya dhuluma anayofanyiwa mwanamke kwa jina la sheria ya uadilifu na haki, na kumtakasa aliyedhulumiwa na kumwokoa aliyepatwa na maafa.

Hotuba yangu ambayo leo hii nina furaha kutoa mchango wangu katika mkutano huu muhimu, na ambao una bahati ya kupata ulezi mwema na mtukufu kutoka kwa Mheshimiwa Raisi wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri Bwana: Abdul-Fatah Al-Sisi, ambayo inafanana na joto lililomo kifuani au mpumuo wa aliyejeruhiwa; bali hotuba hii ni malalamiko mageni ninayoyabeba kuwafikishia wasomi, watunzi wa sheria, na walinzi wa maadili ya mbinguni; kwa yale ambayo yanapigiwa kelele hivi sasa na mazingira yaliyopo, kutokana na sarafu feki (ya udanganyifu) kuifyagia sarafu huru ya asili katika nyanja za utoaji fatwa na ulinganiaji wa sheria ya Mwenyezi Mungu kwa watu, na yale yanayotolewa na baadhi ya madai ya elimu ya vikao vya upotoshaji wa Uislamu na kuthubutu kuitokea Qurani, Hadithi na Urithi mwema wa Waislamu; na kukaa katika viti na mabaraza ya wanachuoni katika kampeni zilizotawanywa maeneo tofauti, na katika uthubutu wa chuki, sidhani kwamba unajificha kwa mtu yeyote, na ambao unatia unyonge katika vurugu na ghasia hizi, na kuishughulisha huzuni ambayo hakuna huzuni nyengine yoyote inayozidi hatari yake hata iwe huzuni na majonzi ya maisha na mambo ya lazima katika maisha.

Fatwa - zimebakia kuwa - na zitaendelea kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu - kuwa zinaelezwa na kusimuliwa katika ulimwengu wetu wa Kiarabu na wa Kiislamu - na wanachuoni na wasomi safi wenye kubeba amana juu ya hukumu za Dini. Ofisi ya Mufti ndiyo kamisheni pekee walizozijua watu, na kugonga milango yake kila wanapozidiwa na jambo la utafiti kuhusu hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa yale yanayowajia miongoni mwa mambo ya dunia na Dini, na yale yenye hamu ya kuyanyoosha katika uongofu wa maisha yao: ili kuepukana na dhimma na kuwa na tamaa ya kuyapata yale yaliyo mbele ya Mwenyezi Mungu.

Chaguo la Mufti ndilo lililokuwa sawa pamoja na chaguo la yule anayefikisha na kulingania kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Na nakumbuka siku niliyopewa jukumu la umufti mimi mja fakiri ninayesimama mbele yenu, khofu iliniandama kwa muda mrefu nisije kuhalalisha haramu au kuharamisha halali. Wala sio vigezo vya kifiqhi ndio ambavyo vikinipa mashaka, kwa sababu nafungamana na kizazi alichokikirimu Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa mwanafunzi na kujifunza kwa wanachuoni waliobobea zaidi, waliosimamia malezi yao kwa matunzo ya kielimu katika misingi ya mashina na matawi; vyote sawasawa, na hasa: somo la Fiqhi ambalo lina fungu la kubwa katika nyakati za masomo, kiasi kwamba lilikuwa likisomeshwa saa za kwanza za mapema asubuhi siku tano kwa wiki kwa muda wa miaka tisa ya masomo. Na wakati tulipojiunga na kitivo cha elimu ya Misingi ya Dini, mwanzoni mwa miaka ya sitini ya karne iliyopita, tukaendelea na masomo kwa somo liitwalo: Hali na Mazingira ya Mtu, na somo liitwalo Misingi ya Fiqhi. Tukasoma kwa mwanachuoni Imamu: Muhammad Abu Zahra – Mwenyezi Mungu amrehemu – kwa muda wa miaka miwili ya masomo, mfululizo. Maelezo haya ya mazingira yaliyopita yanayohusiana na Fiqhi na Misingi yake na mambo yake ya lazima miongoni mwa sayansi na elimu nyengine – ambazo tumeziegemeza kwenye migongo yetu katika umri wetu wa mapema (tukiwa wachanga) – ndizo zilizonihamasisha kukubali kubeba jukumu na cheo cha umufti. Na imenibainikia kwamba maswali mengi ya wenye kutafuta ufumbuzi wake ni yale yenye kusaidia kuyajibu, na kwamba baadhi ya maswali hayo haiwezekani kabisa kujitegemea kwa kutoa fatwa mufti mmoja pekee, kwa vyovyote atakavyokuwa na hadhi ya juu kwa kuzungukwa na elimu ya Fiqhi na Misingi yake. Kwa mfano: masuala yanayohusiana na mambo ya benki, uhamishaji wa viungo vya mwili, mabenki ya maziwa, sindano za hadubini na uainishaji wa jinsia ya mtoto, na mengine mengi.

Na kujiepusha na dhima, nilikuwa najadiliana kwa yale yanayojibu masuala ya aina hii katika vikao vya jopo la tafiti za Kiislamu, jopo ambalo limetimia wataalamu wa fani tofauti hata kuliko ofisi ya Mufti. Kama vile madaktari, wataalamu wa uchumi na mabenki, wasomi wa uhandisi wa vinasaba, maprofesa wa sheria, na wengineo. Kisha tunategemea rai ambayo inamalizikia na kutolewa maamuzi yake na baraza hili.

Na jambo linalopasa kulitaja katika majaribio haya ni kwamba mimi nikiwa nafuatana na Sheikh wetu imamu aliyetangulia Profesa: Muhammad Sayyid Tantwawy - Sheikh wa Al-Azhar aliyepita - Mwenyezi Mungu Amrehemu - nimekutana na marehemu Mshauri: Farouq Saifu Nnasr, ambaye alikuwa Waziri wa Sheria wakati huo, nikawa ninachelea kupata miongozo kutokana na yale waliyokuwa wakinong’onezana wenzangu kutoka kwa maprofesa na wengineo, isipokuwa nimeshtushwa na sheikh ananiambia akiwa ananikabidhi jukumu: sema yale yanayoridhiwa na dhamira yako na yale yatakayokuondosha na jukumu mbele ya Mwenyezi Mungu Mtukufu. Sisi tumeshajivua jukumu letu kwa kukukabidhi wewe amuzi hili (jukumu).

Nimechukua usimamizi wa jukumu la umufti kwa mwaka mmoja na nusu, nilikuwa nafanya kazi katika mazingira ya uhuru wa kila upande wenye kujitegemea kikamilifu, na katika heshima ya wazi kutoka kwa maofisa na watu wengine na kutoka kwa magazeti na vyombo vya habari, mpaka wasomi sahihi na wataalamu wa kutoa fatwa katika siku zetu hizi wamepewa mtihani wa aina ya mibinyo na dhiki ambayo haikuwahi kutokea kwa changamoto ya namna hii. Nakusudia shambulizi dhidi ya urithi wa Waislamu na uchochezi unaofanywa na watu wasiokuwa na vigezo vya maarifa yake na ufahamu wake, sio katika elimu wala katika usomi, wala katika adabu njema au heshima kwa zaidi ya watu bilioni moja na nusu kutoka kwa wale wanaouadhimisha na kuutukuza urithi huu, na kuupa heshima yake ya kweli kweli. Shambulizi lenye miito batili inayozongewa udanganyifu wa vijana. Kama madai, unawirishaji na uhuru wa kubuni na kujieleza, bali na haki ya kubadilisha hata kama mabadiliko hayo yamo katika Dini na sheria yake. Ikawa ni jambo la kawaida linalojikariri kuzikata ibara za wanachuoni wa Fiqhi katika mtiririko wake na nyanja zake za ushahidi ili zionekane ni ibara ngeni zilizotoka nje ya mizani na utaratibu na zenye kukataliwa ambazo haziingii masikioni wala hazina kionjo na ladha. Na kabla ya kuenezwa na kusambazwa katika vikao vya mijadala, zinaambatanishwa na sheria ya Uislamu na hukumu za Fiqhi ya Waislamu kupitia mazungumzo yaliyojazwa falsafa, mikanganyo, uchochezi, makosa katika maarifa, na kushindwa kudiriki tofauti kati ya wasifu wa tendo lenyewe na athari za elimu ya kale za kisheria zinazofungamana nayo. Tendo husika na yanayofungamana nayo linaweza kuwa kutokana na athari za elimu ya kale kutokana na mlango wa kukisia kisia ambazo zinapelekea kuwepo kukisia kiakili ndani ya akili na wala sio nje, au kukisia kisia ambako hakuwi kwa yeyote isipokuwa kwa watu wa maumbile yaliyokengeuka kutokana na wanaolindwa na sheria na makubaliano ya kimataifa katika ustaarabu wa Magharibi leo hii.

Na kufikia hapa, inaonekana jambo la vurugu na ghasia hizi linatarajiwa kutokea ikiwa litachukuliwa katika muktadha wa vimbunga vinavyokuja ambavyo vimevuma kwenye maeneo yetu na kuyabomoa iliyoyabomoa na kuyabakisha iliyoyabakisha mpaka ukaribie muda wa wavunaji wake katika agenda ya watu husika.

Lakini jambo ambalo halikupitikia akilini ni hadaa ya baadhi ya wanaojinasibisha na elimu au wenye kuvaa vazi la wasomi na kuwarubuni kwa umashuhuri na mali ili washiriki kuufinyanga finyanga uongo huu na ili wawe mashahidi wa uongo kwa ajili ya kupigia debe batili hizi kati ya watu.

Mabibi na mabwana mliohudhuria, ni juu yetu kufikiria kidini katika uhalisia wa upekee wa Uislamu kati ya dini nyengine kwa mashambulizi haya mabaya. Na tunajiuliza: je, tumesikia au kushuhudia programu ya Kiyahudi kutangazwa kwa lugha ya Kiebrania au kwa lugha nyengine yoyote ile, tunabadilisha zamu za kukebehiana – waziwazi – kutoka kwenye kitabu cha Taurati na Talmoud?! Na katika kuyalenga waziwazi mabadiliko ya familia ya Kiyahudi kutoka katika Dini yake na sheria yake? Na je tumeona au kusikia – katika viunga vyetu vya Kiarabu na Kiislamu – programu inayokejeli kitabu cha Injili? Au inayothubutu kutoa wito kwa Wakristo kuyapukutisha mafundisho yake kwa mikono yao? Na je, mashambulizi kama haya – kama yametokea – inawezekana kupita kiulaini kama vile unavyopita upuuzi huu kwa Uislamu kwa wanachuoni wake kwa kuona na kusikia?!

Ndugu waheshimiwa wanachuoni!

Siyo kwa bahati mbaya kabisa kwenda sambamba kwa baadhi ya miaka tu kuyabomoa mataifa ya Kiarabu na Kiislamu yote kwa pamoja, pamoja na miito na milinganio yenye shakashaka inayojitokeza kwa kuona haya kwa mwanzisha jambo husika, unanadi kwa ulazima wa kuvunja haiba kubwa na heshima yake na kutazama kwa uigaji huu ambao tunajifakharisha kwa kuwaanzishia watoto wetu kwa mtazamo wa kejeli kwa kuzingatia kuwa ni tabia ambayo haina nafasi katika utamaduni wa vurugu na ghasia za kisasa, pamoja na mpango wa kutisha ili kuuvunjavunja urithi wa kale wa Waislamu pamoja na kuwakejeli maimamu na wasomi wake. Na katika joto la ukaidi linaloakisi ukubwa wa njama dhidi ya ustaarabu wa Kiislamu.

Hayo yanaenda sambamba pamoja na shambulizi lililopangiliwa vyema dhidi ya Al-Azhar mpaka ikawa ni jambo la kawaida kuilaani Al-Azhar na kuulaani mtaala wake kutokana na tukio lolote la kigaidi, katika juhudi za kusikitisha zilizofeli kwa jaribio la kufifisha kukubalika kwake katika nyoyo za Waislamu. Na mpaka tumekuwa tunajua nyakati za mashambulizi haya baada ya kuyafwatilia na kuyachungua kwa makini. Tukakuta kwamba yanatokea katika moja ya hali mbili: ya kwanza baada ya kutokea shambulizi la kigaidi. Na hali ya pili ni pale kila mara Al-Azhar inapopiga hatua ya mafanikio katika kutimiza na kufikisha ujumbe wake ndani na nje. Na mpango husika katika hali hii ima ni ukimya unaofanyiwa kazi na kuyaficha yaliyo mema na mazuri, au utafiti na upelelezi wa kasoro na dosari na kuzitangaza baada ya kuzikuza na kuzifanya zionekane ni majanga makubwa. Nami sina ufafanuzi wa ung’ang’anizi huu wa kufungamanisha kati ya ugaidi na Uislamu isipokuwa ni udanganyifu wa mwamko wa Waislamu na kuyaondosha macho yao kwenye kasoro na ila ya kweli kweli ambayo imeutengeneza ugaidi huu ukaukuza na kuunenepesha. Nao – kwa mtazamo wangu – ni siasa mbovu za kimataifa zisizojua kitu kuhusu undugu wa kiutu, wala tabia za umma. Hayo ni mataifa ambayo uchumi wake unasimama kwenye utengenezaji silaha na kuzisafirisha nje ya nchi na yale yanayohitajika kwa ulazima kutokana na kuchochea fitina na kuuwasha moto wa vita katika mataifa ya Waislamu na sio watu wengineo.  

Yote hayo yameenda sambamba na mahitaji ya pamoja ya kuruhusu mambo mageni ya ajabu-ajabu kwa kuyazingatia kuwa ni haki miongoni mwa haki za binadamu, na katika uthubutu wa kigeni ambao ni wa kushangaza zaidi kuhusu vijana wa Mashariki ambao wamejulikana kwa ujanadume wao na kukirihishwa kwao kimaumbile kutokana na ukengeukaji huu na maradhi haya ya kitabia yenye kusambaratisha.

Na kwa kwenda sambamba na kupinduliwa kwa vitongoji kwa namna ya kuwakumbatisha na umagharibi, na miito ya kuwepo wajibu wa usawa kati ya mwanamke na mwanamme katika urithi, kuolewa mwanamke wa Kiislamu na mwanamume asiyekuwa Mwislamu, ambao ni mlango mpya kati ya milango ya makubaliano ya Sidaw na kuondosha ubaguzi wa aina yoyote ile kwa mwanamume kutoka kwa mwanamke. Kinachotakiwa hivi sasa kwa Waarabu na Waislamu ni kufuata na kutii na kuachana na uhafidhina wao.

Tulikuwa tunatamani kusikia sauti ya kamati yetu kuu kwa mchango wa kamisheni za idara za Mufti ulimwenguni na ukelele wake wenye kupinga uadui huu wa waziwazi dhidi ya Qurani na sheria yake, au utoaji wa msukumo wake kwa Al-Azhar Al-Sharif ambayo imesimama ikikitetea Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kando yake kuna ofisi ya Mufti ya Misri ambayo – inashukuriwa mno – kwa kutoa taarifa yake yenye kukataa wito huu. Mangapi tumeyatamani pia kutoka kwa kamisheni na majopo makubwa ya Fiqhi ya Kiislamu kuharakisha kupinga uthubutu huu dhidi ya dini ya Mwenyezi Mungu. Shukurani za dhati kwa Shekhe Mtukufu: Hamdah Suaiyyid – Mufti aliyepita wa Tunisia, na wanachuoni wa Zaituna na mashekhe wake ambao wamewaonya Waislamu kutokana na kutiririka nyuma ya mwito wa usawa katika urithi kati ya mwanamume na mwanamke, na kuruhusu mwanamke wa Kiislamu kuolewa na mwanamume asiyekuwa Mwislamu.

Enye Watukufu mliohudhuria!

Ikiwa nina pendekezo kwa semina hii jumuishi kwa maimamu wa fatwa katika ulimwengu wetu wa Kiarabu na wa Kiislamu kwa jina la “kitengo cha fatwa na sayansi zake” litaanza kwa mwaka wa kwanza, na kuundiwa mifumo yenye tabia ya upana kwenye kila kitu, haufungiki au kufupishika kwenye sayansi ya Fiqhi tu, bali unarefuka kukusanya misingi ya kina ya kisayansi katika sayansi ya zana (nyenzo), sayansi ya hoja za kunukuu na kiakili, pamoja na kuichunga elimu ya mantiki na elimu ya mjadala yakifanyiwa kazi masuala ya Fiqhi, na kushughulikia - kwa kiwango cha hali ya juu - kusoma na kuchunguza makusudio ya sheria na hasa katika peo za kisasa.

Al-Azhar, msikiti wake na chuo kikuu chake hivi sasa inasimamia jambo hili muhimu mno, na inasubiri mapendekezo yenu matukufu katika maudhui hii.

 

Asanteni sana kwa kuhudhuria kwenu

 

Assalamu alaikum warahmatullahi wabarakatuh

 

Imetolewa kutoka kamisheni kuu ya Al-Azhar:

26 Muharram 1439 A.H.

Sawa na 17 Oktoba 2017 A.D.

 

Ahmad Al-Tayyib

Sheikh wa Al-Azhar

Print
5930 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.