Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

Hotuba ya Imamu Mkuu nchini Ureno 2018
Anonym
/ Categories: Main_Category

Hotuba ya Imamu Mkuu nchini Ureno 2018

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu.

Suala la misingi ya Kidini na matatizo ya jamii za sasa.

Makaribisho na Shukrani.

Baada ya hayo

Neno langu ambalo leo ninafuraha kulisema mbele yenu linakuja katika jumla ya kazi za majukumu ya Al-Azhar Al-Sharif, na Baraza la Wazee wa Kiislamuu katika juhudi zao kubwa za kujenga msingi wa “Mazungumzo kati ya Mashariki na Magharibi” pamoja na jaribio la utekelezaji wake ndani ya miji mikuu mbalimbali ya Ulaya Afrika na Asia.

Lengo la kazi hizi ni kukunjua daraja la maelewano ya ustaarabu kati ya mwanadamu na nduguye mwanadamu, hata kukiwa na tofauti gani ya kijinsia kati yao na tofauti ya lugha imani, Dini, pamoja na tamaduni desturi na jadi…

Na hilo ni kupitia msisitizo wa ushirikiano wa Kidini – na zaidi ya hilo – kati ya Waumini wa Dini za mbinguni, na hata wasiokuwa Waumini, miongoni mwa wale wenye kuheshimu Dini na wanafahamu umuhimu wake katika mwenendo wa ulimwengu wa sasa, pamoja na kuurudisha kwenye usahihi wake, baada ya kukaribia kupoteza mwelekeo “Dira” na kupoteza njia sahihi chini ya miguu yake, na kusimamia kile kinacho wezekana kufanana na “Mporomoko wa Kimaadili” na kuingia kwenye fujo ambayo huenda historia ya mwanadamu haijapatapo kufahamu fujo hiyo kabla ya hapo.

Enyi Waheshimiwa!

Huenda katika mambo yaliyothibiti kwa watu wote wa Mashariki na Magharibi ni kuwa, ulimwengu wetu wa zama hizi unapita kwenye matatizo magumu mbalimbali ikiwa ni pamoja na: tatizo la kiuchumi ambalo limeeneza umasikini, njaa, ukosefu wa ajira kwa vijana, madeni, kuongeza mwanya kati ya walionacho na wasionacho, tatizo la mazingira na matatizo ya siasa za kisasa za kimataifa, na machungu yanayozaliwa kwenye mizozo na utendanji wa kimataifa pamoja na mvutano wa kuwa na ushawishi “kueneza fujo kuharibu family na kutengwa mwanamke” [1]  na yasiyokuwa hayo miongoni mwa matatizo kasoro na maradhi ya kimaadili kijamii na kibinadamu ambayo yanamfika mwanadamu wa karne ya ishirini na moja hali ya kukata tamaa pamoja na kumuharibia raha ya maisha utulivu wa kuwa makini na dhamira.

Matatizo haya yametoa msukumo kwa wasomi wa Magharibi wazee wake viongozi wa Dini pamoja na wanachuoni wake kuzingatia wajibu huu ambao leo unajikusanya kwenye anga ya ulimwengu kama yanavyojikusanya mawingu meusi yenye kuonya hali ya maangamizi, wamerejesha mtazamo na kufanya mikutano ya kimataifa, ikiwa ni pamoja na mkutano wa pili wa Dini za ulimwengu, ambao wawakilishi wa Dini mbalimbali walitoa wito wa kile kilichoitwa umuhimu wa “Maadili ya Ulimwengu” ili kujenga mfumo mpya wa dunia unaotutoa kwenye matatizo haya na kuleta miongozo iliyothabiti ambayo ni: “kuwajibika na utamaduni usio na vitendo vya utumiaji nguvu, kuheshimu viumbe wote hai, na ushirikiano wa utamaduni na mfumo sawa wa kiuchumi, kuwajibika na utamaduni wa usamehevu, na utamaduni wa usawa katika haki na ushirikiano kati ya mwanaume na mwanamke”[2]

unashukuriwa kwa maadhimio haya kwani yanazindua duru muhimu ambayo inawezekana kutekelezwa na wanadini

Print
7232 Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.