AL-AZHAR AL-SHARIF: VITENDO VYA UDHALILISHAJI KWA WANAWAKE NI HARAMU KISHARIA, NI TABIA YA KULAANIWA MOJA KWA MOJA WALA HAIFAI KUTETEWA
AL-AZHAR AL-SHARIF: VITENDO VYA UDHALILISHAJI KWA WANAWAKE NI HARAMU KISHARIA, NI TABIA YA KULAANIWA MOJA KWA MOJA WALA HAIFAI KUTETEWA
Al-Azhar Al-Sharif imetoa maelezo kuhusu yale yanayosambaa kwenye vyombo ya habari na mitandao ya mawasiliano ya kijamii juu ya vitendo vya udhalilishaji kwa wanawake, jambo hili limefikia kiwango cha kufanyiwa uadui yule mwenye kufanya kitendo cha udhalilishaji kwa wanawake, kwa dhana ya kupambana na vitendo hivyo au kujaribu kumlinda mwanamke anayefanyiwa udhalilishaji huo, wakati ambapo baadhi wanafanya juhudi kutumia mavazi ya baadhi ya wasichana au tabia zao kuwa ndiyo sababu ya kufanya vitendo hivyo viovu, au kumshirikisha msichana katika dhambi hii.
Mukabala wa vitendo hivi. Al-Azhar Al-Sharif inasisitiza kuwa, kitendo cha udhalilishaji kwa mwanamke iwe kwa ishara, tamko au kwa kitendo, ni vitendo haramu ni ukiukaji wa maadili, kisheria anapata dhambi mwenye kutenda, kama vile ni kitendo kinachomuingiza kwenye makosa kisheria na kisharia. Mwenyezi Mungu Anasema: {Na wale wanao waudhi Waumini wanaume na wanawake pasi na wao kufanya kosa lolote, bila ya shaka wamebeba dhulma kubwa na dhambi zilio dhaahiri}[Al-Ahzaab: 58].
Al-Azhar Al-Sharif inasisitiza kuwa udhalilishaji kwa wanawake ni kosa la jinai na mdhalilishaji anapaswa kutokuwa na sharti au muundo wowote, kwani kuhalalisha vitendo vya udhalilishaji kwa sababu ya tabia za wakina dada au kwa sababu ya mavazi yao yaonesha juu ya ufahamu potofu, hili ni kutokana na vitendo vyenyewe vya udhalilishaji ndani yake ni kuna uadui kwa mwanamke kwenye uhuru wake na heshima yake, kuongezea pia yale yanayopelekea ongezeko la vitendo hivi vya kuchukiza ni kupotea kwa hisia za usalama, na kufanya uadui kwenye heshima na utukufu wa watu.
Al- Azhar Al-Sharif inaendelea kueleza kuwa, ustaarabu wa jamii mbalimbali na maendeleo yake hupimwa kutokana na namna anavyochukuliwa mwanamke kwa upande wa kuheshimiwa kwake kufanyiwa vitendo vya adabu katika mashirikiano naye, na pia kutokana na usalama alionao na utulivu, pindi Mtume S.A.W. alipotaka kuleta dalili juu ya ukubwa wa Uislamu na utulivu wa nguzo zake, alitumia dalili ya utulivu wa wanawake wa usalama kuwa ni kiashirio juu ya hilo, imekuja katika Hadihti sahihi kuwa: “Utamuona mwanamke msafiri akisafiri kutoka eneo la Al-hiira (ni sehemu iliyokaribu na Kuufa) mpaka kufanya ibada ya kutufu Ka’aba akiwa haogopi yeyote isipokuwa Mwenyezi Mungu tu”.
Al-Azhar Al- Sharif inatoa wito wa kuboreshwa kwa sheria ambazo zinamtia hatiani mwenye kufanya vitendo hivi vya udhalilishaji kwa wanawake pamoja na kuadhibiwa kwa mwenye kutenda, kama vile inatoa wito kwa taasisi husika kuendesha kampeni za kuinua mwamko na uelewa kwa jamii aina za vitendo hivi vya udhalilishaji na hatari zake, pamoja na kukwepa athari zake zenye kubomoa maadili na maisha, hasa vitendo vya udhalilishaji kwa watoto wadogo, pamoja na kuendesha vipindi vingi kwenye vyombo vya habari ili kuwafahamisha wananchi yale yaliyo wajibu kwao wakati wa kutokea kwa vitendo hivyo, na yale yanayopelekea kitisho kwa mdhalilishaji wanawake pamoja na kuimarisha ulinzi kwa mwanamke au msichana anayefanyiwa kitendo hicho cha udhalilishaji, kama vile Al-Azhar inavitaka vyombo vya habari kuepukana na kurusha hewani mada zozote zinazotangaza vitendo hivi au kuoneshwa mtendaji wake kwa sura yoyote ile inayotoa hamasa kwa wengine kumuiga.