Afrikaans (Suid-Afrika)

منبرٌ كبيرٌ لنشر وسطية الأزهر الشريف بكل لغات العالم

 

HOTUBA YA IMAMU MKUU KATIKA MAHAFALI YA UFUNGUZI WA KANISA KUU LA MAZAZI YA KRISTO KATIKA MJI MKUU MPYA WA KIIDARA
Anonym
/ Categories: مقالات

HOTUBA YA IMAMU MKUU KATIKA MAHAFALI YA UFUNGUZI WA KANISA KUU LA MAZAZI YA KRISTO KATIKA MJI MKUU MPYA WA KIIDARA

HOTUBA YA IMAMU MKUU KATIKA MAHAFALI YA UFUNGUZI WA KANISA KUU LA MAZAZI YA KRISTO KATIKA MJI MKUU MPYA WA KIIDARA

  • Ulizeni historia itakufahamisheni kuwa Makanisa ya Misri mengi yao yalijengwa zama za Waislamu.
  • Dola ya Kiislamu ni yenye kulinda Makanisa ya Wakristo na hii ni hukumu ya kisharia na wala siyo kupendezesha maneno.
  • Waislamu wapo mstari wa mbele kulinda Makanisa kuliko ndugu zao Wakristo.
  • Msikiti na Kanisa Kuu yanakubaliana kupambana na kila jaribio la uchafuzi wa utulivu wa nchi.
  • Tupo kwenye tukio la aina yake halijawahi tokea kabla ya hapo katika historia ya Ukristo na Uislamu.
  • Msikiti na Kanisa la Mji Mkuu wa Kiidara ni ngome mbili katika ngome za ibada nchini Misri.
  • Misri ina haki ya kujifaharisha na mafanikio haya mazuri na kuwa ni mfano ulio bora katika undugu wa Kidini.

Imamu Mkuu Prof. Ahmad At-Tayyib Sheikh Mkuu wa Al-Azhar Al-sharif jioni ya siku ya jumapili alitoa hotuba wakati wa ufunguzi wa Kanisa Kuu la Mazazi ya Kristo kwenye Mji Mkuu Mpya wa Kiidara, alielezea kupitia hotuba hiyo furaha yake ya kushiriki akiwa pamoja na Mheshimiwa Abdulfattah El-Sisi Rais wa Jamhuri ya Kiarabu ya Misri, akiwa na Mheshimiwa Mahmuod Abbas Rais wa Dola ya Palestina na ndugu yake kipenzi Mtakatifu Papa Tawadrus wa Pili, Papa wa Alexandria na Askofu Mkuu wa Injili ya Mtakatifu Marko katika maadhimisho haya ya ufunguzi wa ngome mbili kubwa, bali ni ngome kubwa zaidi za ibada nchini Misri, nazo ni Msikiti wa “Al-Fattah Al- A’leem” na Kanisa Kuu la “Mazazi ya Kristo”.

Imamu Mkuu alisema kuwa “Tukio hili linazingatiwa ni la aina yake na huenda halijawahi kutokea kabla ya hapo katika historia ya Ukristo na Uislamu, kwa mujibu ninavyofahamu, kwani sijui kama kuna Msikiti na Kanisa vimejengwa ndani ya wakati mmoja na kumalizika pia ndani ya wakati mmoja lengo ni kuleta hisia za undugu na ubadilishanaji wa upendo kati ya Waislamu na ndugu zao Wakristo - na wala sijui kama tukio kama hili limetokea kabla hatujashuhudia leo ngome hizi mbili zenye kiwango kikubwa cha utaalamu wa ujenzi ambao Misri ina haki ya kujifaharisha nazo kwenye nchi nyengine, na Mji Mkuu wake mpya una haki ya kujifaharisha katika miji mingine”.

Imamu Mkuu akaelezea shukurani zake nyingi kwa Mheshimiwa Rais Abdulfattah El-Sisi kwa mafanikio haya mazuri, pia alitoa salamu za pongezi kwa Papa Tawadrus “Na wale waliokuwa nyuma yake ndugu zetu Wakristo waliopo nchini Misri na waliokuwa nje ya Misri kwa Kanisa hili jipya ambalo bila ya shaka yoyote litasimama imara pembezoni mwa Msikiti mpya, Msikiti wa Al-Fattah Al-A’leem, yakipambana na kila jaribio la kuchafua utulivu wa Taifa na kueneza fitina za makundi”.

Imamu Mkuu katika hotuba yake alizungumzia msimamo wa Uislamu kuhusu Kanisa, na akasema kuwa ni maudhui isiyo na mjadala na kuwa: Uislamu au Dola ya Kiislamu kisharia ni yenye jukumu la kulinda Makanisa ya Wakristo, na hii ni hukumu ya kisharia, ikiwa Sharia inampa jukumu Mwislamu kulinda Msikiti, basi yenyewe kwa kiwango hicho hicho inampa jukumu Mwislamu kulinda Makanisa. Waislamu wapo msitari wa mbele kulinda Makanisa zaidi ya ndugu zao Wakristo, na hii siyo hukumu inayokuja kwa lengo la kupendezesha maneno, bali ni hukumu inayosimama kwenye msingi wa Aya ya Qurani Tukufu ambayo sisi sote tumeihifadhi, pamoja na maana yake kwa masikitiko makubwa wakati mwengine imejificha kwa watu wengi mpaka kwa wale wenye weledi. Aya hii ndiyo ambayo inampa jukumu au kumruhusu Mwislamu kupigana kwa ajili ya kulinda nafasi ya ibada kwa Mayahudi, Waislamu na Wakristo, nayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: [Na lau kuwa Mwenyezi Mungu hawakingi watu kwa watu, basi hapana shaka zingeli vunjwa nyumba za watawa, na makanisa, na masinagogi, na misikiti, ambamo ndani yake jina la Mwenyezi Mungu linatajwa kwa wingi]{Al-Hajj, 40}.

Imamu Mkuu alitahadharisha kutumia fatwa za kauli zilizotolewa wakati fulani kwa hali maalumu kuwa katika Uislamu haifai kujenga Makanisa, hili halipo kielimu wala chochote katika haki, hili ni kosa kubwa, ulizeni historia itakufahamisheni kuwa Makanisa ya Misri mengi yao yalijengwa zama za Waislamu.

Alirudia tena mwishoni mwa hotuba yake kumshukuru Rais Abdulfattah El-Sisi kwa “Mafanikio haya mazuri ambayo yanayapa Misri yetu haki ya kujifaharisha nayo, na kuifanya Misri ni mfano bora wa kuigwa katika upendo na undugu wa Dini, hasa kati ya Uislamu na Ukristo, kama vile Imamu Mkuu alitoa shukurani kwa vijana wote shupavu wa Misri waliosaidia kufanikisha ngome hizi mbili ndani ya muda wake uliopangwa na kushuhudiwa na wote”.

Print
7123 Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.

أقسم بالله العظيم أن أكون مخلصًا لديني ولمصر وللأزهر الشريف, وأن أراقب الله في أداء مهمتى بالمركز, مسخرًا علمي وخبرتى لنشر الدعوة الإسلامية, وأن أكون ملازمًا لوسطية الأزهر الشريف, ومحافظًا على قيمه وتقاليده, وأن أؤدي عملي بالأمانة والإخلاص, وأن ألتزم بما ورد في ميثاق العمل بالمركز, والله على ما أقول شهيد.