Neno "Jihad" limekuja kwa minyambuliko yake katika Qurani Tukufu katika aya 31, wakati ambapo neno "Vita" limekuja katika aya 4 tu. Tunatambua kwamba maana ya Jiahd katika aya za Qurani na matiniza Sunna za Mtume Muhammad (S.A.W.) ni maana mpanazaidi kuliko maana ya kupigania vita; ambapo maana ya kupigania vita inamaanisha –hasa- mapambano kwa kutumia silaha katika vita, ilhali jiahd inamaanisha kufanya jiuhudikatika kupinga maadui, sawa sawa maadui hawawakiwa ni watu wanaofanya uvamizi au Shetani ambayeni lazima Mwamini kujitahidi kwa bidii ili kujikinga naye, au hata nafsi ya mtu mwenyewe, na ambayo inamshawishi kufanya maovu.