Kufuata dini ama Kuwa na mawazo makali?!

4

  • | Friday, 27 January, 2017

Miongoni mwa namna za kisasa za kufuata mawazo makali ni kufuata mawazo ya kundi au chama fulani, ambapo tunakuta kwamba anayejiunga kwa lo lote kati ya makundi hayo hutangaza utiifu wake kwa watu wa kundi hilo au chama hicho tu, bila ya kujali waislamu wengineo. Jambo ambalo baadhi ya watu wanadhni kuwa ni aina ya kufuata dini, lakini hakika dini imekataza kufanya hilo na imelikosoa, Mwenyezi Mungu Amesema: { Hakika Waumini ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu, na mcheni Mwenyezi Mungu ili mrehemewe} [Al-Hujuraat:10], bali imejaali imani na matendo mema ni msingi wa kupendelezana baina ya watu, Mwenyezi Mungu Amesema {Enyi watu! Hakika Sisi tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekujaalieni kuwa ni mataifa na makabila ili mjuane. Hakika aliye mtukufu zaidi kati yenu kwa Mwenyezi Mungu ni huyo aliye mchamngu zaidi katika nyinyi. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kujua, Mwenye khabari} [Al-Hujuraat:13].

Zaidi ya hayo, uwezo wa Mwenyezi Mungu unadhihiri sana kupitia kwa jambo hilo, ambapo Mwenyezi Mungu Amesema: {Na katika Ishara zake ni kuumba mbingu na ardhi, na kutafautiana ndimi zenu na rangi zenu. Hakika katika hayo zipo Ishara kwa wajuzi}.[Ar-Ruum:22].

Na hakika Uislamu umekataza kuwa na mawazo makali kwa sababu jambo hilo husababisha athari mbaya juu ya umma na wanadamu wote, labda mawazo makali humsukuma mtu kufuata myenendo mibaya inayokwenda kinyume na maadili mema, inaweza kudhulumu na kufanya ujeuri bila ya kujali wengine na rai zao, na labda anasema uongo kwa ajili ya kuinusuru rai, fikira na madhehebu yake.

Jambo lisilo na shaka ni kwamba kuwa na mawazo makali ya "kifikira" humpelekea mtu kufuata misimamo mikali ya kifikra, kidini, na kimadhehebu, jambo linaloichafusha dini na kuidhihirisha kwa sura mbaya mbele ya ulimwengu, na kuwachukiza watu wote na kuwafanya wasiifuate, na tukifanya hivyo tunakuwa walinganiaji wa mawazo makali, sio walinganiaji wa msamaha, kujuana kama ilivyosifika dini ya Uislamu.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.