Tangazo la Al-Azhar la Uwananchi na Kuishi Pamoja

  • | Wednesday, 14 June, 2017
Tangazo la Al-Azhar la Uwananchi na Kuishi Pamoja

Kutokana na kuitikia mahitaji mapya ambayo jamii zetu za kiarabu zinataka kuyahakikisha, na kupambana na changamoto zinazokabili dini, jamii, nchi.
Na kutokana na kutambua hatari kubwa zinazozuia jaribio la kukiri kuwepo dini mbalimbali katika jamii zetu na ustaarabu wetu.
Na kutokana na kufuatilia juhudi, mikataba na mipango ya kutatua mizozo iliyotekelezwa na Al-Azhar kwa upande mmoja, na ile iliyotekelezwa na taasisi za kidini na kiraia ulimwenguni wa kiarabu katika miaka iliyopita kwa upande mwengine.
Na kuanzia utashi wa kiislamu - kikristo yanayotaka kuishi pamoja kwa utiriri, na kutokana na kukataa misimamo mikali, kulaani uharibifu na jinai zinazotekelezwa kwa jina la dini, ilhali dini haihusiani nazo kabisa, kama ilivyokuja katika Taarifa ya Mkutano wa Al-Azhar iliyohusiana na kupambana na misimamo mikali na ugaidi uliofanyika hapo mwaka 2014 na mikutano na makongamano ya pamoja yaliyofanyika baadaye.

Image

 

Kwa mujibu wa hayo yote, Al-Azhar Al-Shareif na Baraza la Wakuu wa Waislamu zimeamua kufanya mkutano huu anuani "Uhuru na Uwananchi .. Kutofautiana na Kukamilishana" mkutano uliohudhuriwa na Wakuu wa dini za kiislamu, kikristo, na Watu husika miongoni mwa wakubwa wa jamii, siasa, utamaduni walio zaidi ya mia mbili kutoka nchi sitini, pamoja na wanahabari kutoka kwenye eneo la nchi za kiarabu na ulimwenguni kote, licha ya wahusika mashuhuri kutoka Misri.
Na kupitia siku mbili 28 February na 1 Machi vikao vya mkutano huu vilishuhudia mihadhara na mazungumzo kuhusu masuala ya Uwananchi, Uhuru, Kutofautiana na majaribio ya ufumbuzi na changamoto.
Waliohudhuria wamekubali kutoa "Tangazo la Al-Azhar" likiwemo nukta zifuatazo:
Kwanza:
Istilahi ya "Uwananchi" ni istilahi thabiti katika Uislamu, katika katiba iliyowekwa na Mtume (S.A.W.) inayoitwa “Katiba ya Madinah”, mikataba na ahadi za Mtume zilizohusiana na kuainisha uhusiano baina ya waislamu na wasio waislamu. Na tangazo hilo lina hamu ya kusisitiza kwamba uwananchi sio ufumbuzi ulioagizwa kutoka kwenye nchi za kigeni, bali ni kukumbuka mfumo wa utawala uliopitishwa na Mtume (S.A.W.) katika jamii ya kiislamu ya kwanza kabisa alyeianzisha Mtume ambayo ni nchi ya Madinah.
Jambo lisilojumuisha kadri yoyote kutoka katika ubaguzi au kudharau kundi lolote miongoni mwa makundi ya jamii wakati huo, bali imekusanya siasa za kukiri kuwepo dini, ukoo na kiujamii mbalimbali, kutofautiana huko hakufai kuwepo isipokuwa ndani ya wigo wa uwananchi kamili na usawa ambayo zilitajwa katika katiba ya Madinah kutangaza kuwa “Makundi tofauti ya kijamii kidini, ukoo ndio Umma mmoja, na kwamba wasio waislamu wana haki kama waislamu, na wana wajibu kama waislamu".
Na kwa mujibu wa hayo yote, jamii za kiarabu na za kiislamu zinamiliki urithi kuukuu kuhusu kuishi pamoja katika jamii moja, jambo linalotegemea kukiri tofautiana, uwingi, na kuheshemeana.
Na kwa sababu mambo hayo asili na maadili yamekabiliwa na bado inakabiliwa na changamoto ya ndani na ya nje, basi Al-Azhar na Baraza la Wakuu wa Waislamu pamoja na wakristo wa mashariki ya kati wanakutana upya leo chini ya bendera ya usawa baina ya waislamu na wakristo katika nchi, haki, wajibu kwani sote kwa hakika ni kama "Umma mmoja" waislamu wana dini yao na wakristo wana dini yao kufuatia katiba ya Mtume huko Madinah.
Kwa hiyo, basi majukumu ya kitaifa ni majukumu ya pamoja baina ya wananchi wote.
Pili:
Kwa Hakika kukiri dhana ya uwananchi, usawa na haki kunawajibika kulaani vitendo vinavyopigana na msingi wa uwananchi, na kulaani vitendo visivyokubaliwa na sheria ya kiislamu, ambavyo vinatokana na msingi wa kupambanua baina ya mwislamu na asiye mwislamu, jambo linalopelekea kuzuka udharau, kutojali, na kudhulumu, licha ya kufanya mauaji na kuwahamisha wachache kutoka kwa makazi yao kwa dai la kwamba wanafuata dini tofauti, na kadhalika miongoni mwa mambo isiyokubaliwa na Uislamu wala dini yoyote nyingine.
Pia, la kwanza miongoni mwa vitenda kazi vya kuimarisha utashi wa pamoja linadhihiri katika nchi inayozingatia uwananchi unaotegemea katiba yenye kuyatunza maadili ya uwananchi, usawa na kuhukumiwa na kanuni, kwa hivyo tunasema kwamba kuiweka mbali dhana ya uwananchi inapelekea nchi, taasisi za kidini wenye utamaduni na wanasiasa kufeli, na kuathiria vibaya maendeleo, na inawapa waangaliaji nafasi ya kuharibu nchi, utulivu wake, hatima yake na mapato yake.
Aidha kupuuza dhana ya uwananchi kunahimiza kuzungumzia masuala ya wafuasi wa dini walio chache na haki zao. 
Kuanzia tangazo hilo, linawaombea wasomi na wanachuoni kutahadhari hatari za kutumia istilahi ya wafuasi wa dini walio chache inayobebe maana ya kubagua na kujitenga kwa madai ya kusisitizia haki. Hakika tumeangalia miaka ya hivi karibuni kujitokeza upya kwa istilahi ya wafuasi wa dini walio chache, ilhali tulikuwa tunadhani kuwa ilifutwa baada ya zama za ukoloni, lakini imetumika tena mwishoni kwa lengo la kuwatenga baina ya waislamu na wakristo, bali baina ya waislamu wenyewe kwa wenyewe, kwani inapelekea kugawanya utii, na kutilia mkazo kufuata ajenda za nje. 
Tatu:
Kwa mujibu wa yaliyodhihiri katika miongo iliyopita hasa vitendo vya ukatili, uhalifu na ugaidi vinavyofanywa na wanaojinasibisha na dini, na kwa mujibu wa vitendo vinavyowalengea wafuasi wa dini na tamaduni nyinginezo katika jamii yetu kama vile kuhamisha, kuhofisha, kuteka nyara, kwa hivyo wanaokutana hapa miongoni mwa wakristo na waislamu katika mkutano wa Al-Azhar wamekubaliana kutangaza kuwa dini zote ziko mbali na ugaidi kwa aina zake zote, wakiulaani ugaidi sana.
Na wanawataka wanaotuhumu Uislamu au dini yoyote nyingine kwa kuhusiana na ugaidi, kutotoa tuhuma hizo kabisa, kwani kuzipachika tuhuma hizo kwa dini kumewafanya watu wengi hasa wa kawaida (wasio na elimu ya juu) kuzoea kuzifungamanisha dini na ugaidi wakiwazingatia wafuasi wa dini ndio magaidi.
Pia, Wanaokutana wanaona kwamba kuutuhumu Uislamu kwa mujibu wa baadhi ya makosa ya wafuasi wake, inarahisisha sana kuzisifu dini zote kwa ugaidi, jambo linalowapa wenye kuvuka mipaka wa sasa waseme kwamba kunahaja ya kuziondolea dini kwa madai ya kupitisha utulivu katika jamii.
Nne:
Hakika kulinda maisha ya wananchi, uhuru zao, heshima yao na ubinadamu wao na haki zao zote ndiyo wajibu wa kwanza kwa nchi ambayo haifai kupuuzwa, kwa ajili ya kulinda maisha ya wananchi na haki zao, pia haifai katika hali zote kuzizuia nchi kutekeleza wajibu hiyo.
Na historia ya kale na ya kisasa ina mifano mingi wazi inayosisitiza kwamba nchi yoyote ikawa dhaifu basi, haki za wananchi wake hupatwa na ukiukaji, ama zile nchi zenye nguvu huweza kuzitetea haki za wananchi wake. Na kwamba wahenga wa kitaifa na kiutamaduni na wanaohusika na masuala ya umma katika nchi za kiarabu zote wana majukumu makubwa pamoja na nchi kuhusu masuala ya kupambana na vitendo vya uhalifu sawa sawa ikiwa kwa kisingizio cha kidini, kitamaduni au kijamii.
Kwa hakika sisi sote tuna majukumu ya pamoja kwa mujibu wa kujinasabisha kwa uraia mmoja na hatima moja, majukumu hayo ndiyo kushikamana na kusaidiana kwa ajili ya kulinda kuwepo kwetu kwa upande wa kisiasa na kijamii kwani maslahi zetu ni moja na dhuluma ni moja, jambo linalotulazimisha kuzidisha juhudi za pamoja na iliyo muhimu zaidi ni kuzigeuza hisia hizo nzuri kwa kazi ya kikweli katika nyanja zote za maisha, kijamii, kitamaduni na kitaifa.
Tano:
Hakika sisi sote - taasisi na watu - tumefanya juhudi kubwa katika miaka ya hivi karibuni kuhusu kurejea, kurekebesha, kuandaa na kuimarisha kwa utamaduni wetu. Na sisi - waislamu na wakristo – bado tunahitaji kufanya marejeo ya ziada na kuyazidisha marekebesho kupitia kuangalia tena kwa ajili ya kuboresha na kuendeleza utamaduni wetu na hatua tunazozichukua katika taasisi zetu.
Miongoni mwa majaribio hayo ya kurekebesha na kuboresha utamaduni na fikira zetu ni yale mawasiliano yaliyofanywa upya baina ya taasisi za kidini katika ulimwengu wa kiarabu na ulimwengu mzima, hakika tumefanya uhusiano na Pop wa Vatican, Askofu wa Canterbury, na Baraza la Makanisa Duniani na kadhalika..
 Na sisi tunatamani kuanzisha uhusiano zaidi baina ya taasisi za kidini, kitamaduni na vyombo vya habari ulimwenguni wa kiarabu, kwa ajili ya kushirikiana pamoja katika nyanja za kuelekeza, na ulezi wa kidini na kitabia, na kuwalea vijana kufuatia msingi wa uwananchi, na kuendeleza husiano za kufahamiana baina ya taasisi za kidini za kiarabu na zile za kizungu, kwa ajili ya kuimarisha mazungumzo ya kiislamu - kikristo na mazungumzo ya staarabu.
Sita:
Hakika malengo ya Al-Azhar na Baraza la Wakuu wa Waislamu kutoka mkutano huu ni kuanzisha ushirikiano unaoendelea au mkataba unaoendelea baina ya waarabu wote, wakristo au waislamu au wengineo, mkataba unaojengwa juu ya msingi wa kukiri umuhimu wa kufahamiana baina ya pande zote na uwananchi na uhuru, jambo ambalo si lazima na muhimu tu, bali lina udharura kubwa mno kwa maendeleo ya jamii, nchi, ubinadamu na vizazi.
Hakika Mtume (S.A.W.) Ametoa mfano wa kushirikiana kamili na mkataba ulioandikwa baina ya kundi moja wa watu waliopanda meli moja yenye ghorofa mbili, basi watu waliochukua ghorofa ya chini walipotaka kujaza maji walikuwa wanapita juu ya watu waliochukua ghorofa ya juu, basi baadhi yao wakasema "tungefanya utundu katika ghorofa yetu ili tusiwaudhi walio katika ghorofa ya juu?" Mtume (S.A.W.) Akasema kuhusu tukio hilo "watu wa ghorofa ya juu wakiwaacha kutekeleza wanayoyataka, wote wataangamizwa, ama wakiwazuia wote wataokoka".
Na sisi ni kama watu katika meli moja na jamii moja, tunapambana na hatari zinazotishia maishani mwetu, jamii, nchi na dini zetu zote, na tunataka kwa utashi wa pande mbili na kwa kunasibisha na hatima moja kuchangia katika uwanja wa kazi wa kikweli kuziokoka jamii na nchi yetu, na kurekebesha uhusiano wetu kwa ulimwengu ili tuzindue kwa wana wetu wa kike na wa kiume nafasi katika mustakbali nzuri, na maisha mwema.
Hakika wanaokutana hapa wakristo na waislamu wanaandika upya ahadi za udugu wao, na wanakataa majaribio yoyote yanayolengea kuleta uagawanyiko baina yao, au kudhihirisha kwamba wakristo wanafanyiwa ubaguzi nchini mwao, na sisi tunasisitiza kwamba ingawa magaidi wangalitekeleza vitendo vinavyolengea kulitusi jaribio letu la pamoja, na kulengea misingi ya maisha yetu katika jamii zetu hautaweza kutuzuia kuendelea kuishi pamoja, au kuisisitiza dhana ya uwananchi.
Na Mwenyezi Mungu - Aliyetakasika – Anajua makusudio yetu na Yeye Ndiye Anatutosha, naye ni Mbora wa kutegemewa.

Taarifa ya Al-Azhar mwishoni mwa mkutano wa kimataifa wa uhuru, uwananchi, kuishiana pamoja na kushirikiana, uliopangwa na Al-Azhar Al-Sharif na Baraza la Wakuu wa Waislamu, mjini Kairo, Feb. 28 - Machi 1 /2017.
 
Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrik
a
 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.