Mkutano wa Imamu Mkuu na Rais wa Somalia

  • | Monday, 21 August, 2017
Mkutano wa Imamu Mkuu na Rais wa Somalia

Mheshimiwa Imamu Mkuu wa Al-Azhar Profesa; Ahmad Al-Tayyib alimpokea leo Bwana Mohammad Abdullah Farmajo Rais wa Somalia aliyeanza ziara rasmi nchini Misri leo. Mwanzoni kabisa Imamu Mkuu alimpongeza Bwana Farmajo kwa ushindi wake katika uchaguzi wa urais, akimwelezea matamanio yake kwa Somalia serikali yake na raia wake kwa utulivu na amani, akisisitiza kuwa Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kuisaidia Somalia kwa upande wa ulinganiaji na elimu, kwa ajili ya kuchangia kutekeleza matarajio ya nchi hiyo kupata maendeleo na ustawi.
Pia, Imamu Mkuu alibainisha kuwa miongoni mwa juhudi za Al-Azhar nchini Somalia kuendesha misafara miwili ya matibabu na kutoa mawidha mema ili kuwafundisha vijana wa Somalia mawazo yaliyo sawa na kuwatahadhrisha kutoka mawazo makali na fikira walizozieneza magaidi na wenye misimamo mikali, na pia kutoa misaada ya matibabu kwa wasomalia wanaohitaji misaada, aidha yule Mheshimiwa alieleza kuwa Al-Azhar iliwapokea maimamu kadhaa wa kisomali waliokuja ili kupata mazoezi kupitia programu hasa inayotarajiwa kuwasaidia kupambana na masuala ya ugaidi na mawazo makali, akafahamisha kwamba Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kuwapokea wanafunzi na maimamu kadhaa wa kisomali na kuzidisha idadi ya tuzo ya mafundisho kwenye Al-Azhar kwa wasomalia pamoja na kuanzisha kituo cha kufundisha lugha ya kiarabu katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu.

Image

 

 Kwa upande wake, Rais Mohammad Abdullah Farmajo alisisitiza kuwa Sheikhi mkuu wa Al-Azhar ndiye Imamu wa waislamu wote duniani, na kwamba Al-Azhar Al-Shareif ina uwezo wa kupambana na mawazo makali yaliyoenea ulimwengu kote na hasa nchini Somalia, kwani taasisi hiyo ya kiislamu ina cheo cha juu sana baina ya wasomalia na waafrika wote, akiongeza kwamba mawazo makali yanapaswa kukabiliwa na mawazo yaliyo sawa.
Vile vile, Rais Farmajo aliashiria kwamba nchi yake ina haja kubwa kwa Al-Azhar Al-Shareif kuisaidia katika vita yake dhidi ya ugaidi hasa wa kundi la Al-Shabab, na kueneza dhana sahihi za Amani na kuishi pamoja, akisisitiza kuwa Uislamu ndio dini inayotoa wito wa kuleta uelewano baina ya wafuasi wa dini zote tofauti na unakataa vurugu, umwagaji damu na kuwahofisha wananchi wasio na hatia.

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na mawazo makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Categories: Habari
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.