Daesh: linadai kwamba kujiunga na kundi lao kunamrahisishia mwislamu kutekeleza ibada za Uislamu kwa uhuru !

  • | Thursday, 16 November, 2017
Daesh: linadai kwamba kujiunga na kundi lao kunamrahisishia mwislamu kutekeleza ibada za Uislamu kwa uhuru !

      Hakika Uislamu unajumuisha mawazo yote ya kibinadamu ambayo hayapingani na dini hii tukufu, na Uislamu wenye wanamgambo hauhitaji vurugu na ukatili wa makundi yenu, bali unahitaji mwendo wastani wa Mtume (S.A.W) unaosomeshwa katika msikiti wa Al-Azhar, na ambao wafuasi wa makundi hayo hawajui chochote kuhusu mwendo wa Mtume (S.A.W)! hakika Mwenyezi Mungu Hajamwainisha mmoja awe msimamizi wa nyoyo za watu wala awe kama upanga juu ya mashingo yao, lakini Mwenyezi Mungu Amewaamrisha waislamu wawe na upendo, huruma, usamehevu, uadilifu, na ubinadamu.
      Hakika mwislamu anayeishi kwa utulivu, amani na anatekeleza ibada zake za kidini bila ya kuvunja haki za watu, kuwakufurisha au kuwaua haiwezikani kukubalika katika jamii yoyote isipokuwa katika hali chache, ama ikiwa Uislamu katika mtazamo wa wanamgambo hao unahalalisha kuwaadhibu, kuwaua, na kuwapasua watu na kuwavunja heshima ya nchi na cheo chake kwa kubeba silaha dhidi ya wananchi wenye amani na utulivu, basi ni lazima wajue kwamba kupambana na wanamgambo hao ni wajibu kwa mujibu wa mizani ya kibinadamu na mizani ya sheria.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.