Uraia

  • | Tuesday, 21 November, 2017
Uraia

       Aghlabu ya wanazuoni wanaoona kwamba uraia ni badala ya mkataba wa dhima, wanakubaliana kwamba hati ya kwanza iliyoandikwa na Mtume (S.A.W) ni (hati ya Al-Madinah) inayozingatiwa kuwa ni dalili ya kiislamu iliyo nguvu zaidi kwa dhana ya uraia wa kisasa, na historia ya hati hiyo ni kuukuu sana zaidi kuliko barua iliyoandikwa na Mtume (S.A.W) kwa kabila ya Najran na nyingine miongoni mwa makabila ya waarabu, pia ilikuwa chemchem kwa wanazuoni kuhusu kutunga sheria na kueleza masuala yanayohusiana na watu wa dhima.
     Basi Mtume (S.A.W) kabla ya kuzungumza kuhusu kuingia makabila katika ahadi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na kwamba wao wamepewa amani kama amani ya waislamu, amethibitisha katika hati ya Al-Madinah baada ya kuhama kwake moja kwa moja kwamba" waislamu kutoka Quraysh na Yathrib na waliokuhama baada wao na wakapigana Jihadi pamoja nao, basi wao ni umma mmoja, vile vile mayahudi wa Bani Auf ni umma mmoja pamoja na waislamu, mayahudi wana dini yao na waislamu wana dini yao".
     Hivyo Mtume (S.A.W) ameimarisha msingi wa usawa katika haki na wajibu baina ya waislamu na mayahudi katika kuanzisha dola yake ya kwanza, na hapa ni wito wazi kwa ajili ya kurudi tena kwa yaliyothibitishwa na Sunna ya Mtume (S.A.W) wakati alipoanzisha dola ya Al-Madinah, na amewazingatia wananchi wake ni sawa kama umma moja. Basi kutekeleza dhana ya uraia maana yake ni kwamba hakuna mtu katika ahadi ya mtu au katika ulinzi wa mtu mwingine (hata ikiwa namna ya ahadi ilivyoelezwa na Fiqhi ya kiislamu ni kwa ajili ya mieleweko bora zaidi  yaliyojulikana na ulimwengu hivi sasa kuhusu kukubali mwingine).
     Na akiwa mwingine anashiriki katika ujenzi wa nchi na ulinzi wake, bali anashiriki katika uongozi wa nchi, basi usawa baina ya watu katika nchi unabaki madamu hakuna dalili inayothibitisha kwamba mtu fulani amekhini nchi yake, na hapa pia usawa itakuwa baina ya mwislamu na wanaofuata dini yoyote  nyingine.
     Hati ya Al-Madinah ambayo baadhi ya wanachuoni wameiita desturi ya kwanza ya Al-Madinah itabakia kuwa ni msingi thabiti na dalili ya kitendo inayojengwa juu yake msingi wa uraia, na pamoja naye aya zote za Qurani zilizotaja mifano zinazoita -wakati jambo linalohusiana na kuamiliana pamoja na wanaohitilafiana katika itikadi duniani kama washiriki katika ubinadamu, wadugu katika ubinadamu bila ya kushambulia- kwa kuweka mbali njia zote zinazokosoa na kukufurisha na kutishia wenye itikadi potovu.


D. Mohammad abd-Elfadil abd-Elrahim

 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.