Kujitahidi katika Uislamu

  • | Thursday, 16 November, 2017

1- Kwa hakika Mwenyezi Mungu hakutunukia elimu na fiqhi watu fulani na kuwaacha wengine, au kwa muda fulani hasa. Na kwamba heri na baraka ziko katika umma wa Mtume Muhammad (S.A.W.) hadi siku ya kiyama.
2- Bila shaka utengenezaji upya katika maswala ya kifiqhi, na kutazama mambo mapya ya kisasa, unahitaji mtazamo, utambuzi, ufahamu wa kina, ushujaa na ujasiri maalumu.   
3- Mhusika wa utengenezaji upya anatakiwa kuwa na nia nzuri kwa ajili ya Mwenyezi Mungu jambo ambalo litamsaidia kupata fahamu nzuri na kuvumilia ukosolewaji na mishale mikali kutoka kwa wale walioifunga milango ya kujitahidi.
4- Kwa kweli kujitahidi katika Uislamu hakumaanishi kubadilisha misingi wala kuchafua na kupoteza nguzo za dini, bali kunamaanisha kuleta ufahamu na uelewa mpya kwa matini takatifu za dini miongoni mwa Qurani na Sunnah kwa kuambatana na mabadiliko ya enzi tulio nayo.
5- Bila shaka zoezi la kutolea ufahamu mpya wa matini za kidini linahitaji mazingira maalum ambapo kuna masharti ya kufanya hivyo kwani hilo ndilo zoezi hatari linaloweza kuokoa umma na kuapoteza mwingine.
 


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.