Uadilifu kati ya mwanamume na mwanamke

  • | Wednesday, 22 November, 2017
Uadilifu kati ya mwanamume na mwanamke

     1- Dini yetu inakataza kuwadhulumu au kuwapunguza haki za wanawake, bali imewahimiza waumini wawe na uadilifu na kutotenganisha baina ya msichana na mvulana, ikizingatia kwamba kufanya hiyo ni njia kubwa ya kupata ridha ya Mwenyezi Mungu, kwa hivyo Mtume (S.A.W.) amesema "ye yote atakayekuwa na binti na hajamzika akiwa hai na wala hajamdhulumu na wala hajampendeleza mwanawe zaidi kuliko kwake, basi Mwenyezi Mungu atamwingiza peponi".

2- Mtume (S.A.W) Ameusia kuwakirimu na kuwatendea wema wanawake katika hadithi kadhaa, na katika hadithi takatifu aliyoipokea Mtume (S.A.W) kutoka kwa Mola Mtukufu Anasema: "Niridhishieni kupitia madhaifu wawili, mwanamke na yatima".

3- Uislamu umesawazisha baina ya mwanamume na mwanamke katika mambo maalumu, na umetofautisha baina yao katika mambo mengine kwa kadiri inayoafikiana na tabia ya kila mmoja, basi ukasawazisha baina yao katika thamani ya kibinadamu, na kwa upande mwingine ukatofautisha baina yao katika baadhi ya hukumu za kishiria.   

4- Kwa hakika Mwenyezi Mungu Amemwumba mwanamume na mwanamke, na Ameweka baadhi ya hitilafu za kimwili na za kimaumbile, na kwa hivyo Mwenyezi Mungu Amesema: "Na mwanamume si sawa na mwanamke".

5- Kufanya uadilifu na mwanamke haimaanishi kumsawazisha na mwanmume katika pande zote za maisha, kwani usawa inamaanisha kumpa mmoja wa wawili haki hadi kumsawazisha na mwenzake, ama uadilifu maana yake ni kumpa kila mtu haki yake.

6- Ingawa maana dhahiri ya istilahi ya "Usawa" kati ya mwanamume na mwanamke ni nzuri, lakini ni lazima ibainishwe kiwazi wazi, ili watu wajue vipi watatekeleza usawa huo na nini mahitaji yake?!

 

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali

Kitengo cha Lugha za Kiafrika

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.