1- Utukufu wa Uislamu unadhihirika wazi kwa kumtendea haki asiyekuwa mwislamu, na kwamba jirani yako ni kama nafsi yako haijuzu kumdhuru wala kumfanyia maovu.
2- Uislamu unakubali kuwepo kwa staarabu na tamaduni mbali mbali, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: "Na kama Mola wako angalitaka, angaliwafanya watu wote kuwa umati mmoja, Lakini hawaachi kukhitalifiana".
3- Mkataba wa Madina lilikuwa ndilo mfano bora katika historia ya kibinadamu, ambalo liliweka misingi imara ya kuishi pamoja kwa amani kati ya wafuasi wa dini mbali mbali na aina za watu kutokana na yale yaliyomo ndani yake.