Uislmu ni dini ya Rehema

  • | Tuesday, 12 December, 2017
Uislmu ni dini ya Rehema

     1.    Kwa kweli huruma ya Uislamu imewazingatia wagonjwa na wajeruhiwa; ambapo Uislamu umewahimiza wafuasi wake watembelee wagonjwa, na ukawafanyia malaika waombe maghfira kwa anayemtembelea mgonjwa, pia umewaondoshea wale wagonjwa mashaka katika kutekeleza ibada, vile vile, umeruhusia mgonjwa asali akiketi.
2.    Huruma ya Uislamu imejumuisha hali zote za maisha ya waislamu hata katika vita, ambapo Uislamu ukaweka adabu maalumu katika vita; kwa kuwaelimisha waislamu kuwa vita vimehalalishwa kwa ajili ya kuitetea nafsi, dini, nchi kutoka uadui, lengo lake si kuzipokonya mali za wengine na kupomoa nyumba zao. Pia  Uislamu umeharamisha mauaji ya watoto, wanawake, watawa katika pahali pa ibada.
3.    Uislamu haukupuuza wanyama kutoka huruma; ambapo uliwahimiza wafuasi wake watendeane na wanyama vizuri, pia umezuia kuwaudhi au kuwataabisha kwa kazi nzito, kwa hiyo Mtume (S.A.W.) alituambia katika hadithi kwamba mwanamke aliingia moto kwa sababu ya paka; kwani alimfunga, na hakumletea chakula wala hakumwacha aende zake ali kutoka nyasi za ardhi, ilhali mwanamume aliingia peponi kwa sababu ya kumnyewesha mbwa hupumua na kutoa ulimi alipopatwa na kiu kali.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.