Imamu Mkuu: Tunakataa kabisa uamuzi dhalimu wa Tramp, na matatizo ya waarabu na waislamu hayawapa ruhusa ya kupuuza suala la kunusuru Jerusalem “Al-Quds” ya kiarabu kwa haraka haraka

  • | Thursday, 7 December, 2017
Imamu Mkuu: Tunakataa kabisa uamuzi dhalimu wa Tramp, na matatizo ya waarabu na waislamu hayawapa ruhusa ya kupuuza suala la kunusuru Jerusalem “Al-Quds” ya kiarabu kwa haraka haraka

     Mheshimiwa Imamu Mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif Profesa; Ahmad Al-Tayyib ameonya kikali kutoka kwa matokeo mabaya yanayoweza kutukia kufuatia uamuzi wa Marekani kwa kutambua mji wa “Al-Quds” kama ni mji mkuu wa Israel na kubadilisha makao ya ubalozi wake nchini Israel kwenda mji huo, kwani kuchukua hatua kama hii ni dhuluma dhahiri kwa haki iliyo thabiti ya kipalestina na ya kiarabu katika kujiunga kwa mji huo mtakaktifu sawa kwa waislamu au wakristo, ambapo mji huo unajumuisha Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa ambayo ndiyo Qebla ya kwanza na Msikiti Mtakatifu wa tatu, na mahali pa kutembea kwa Mtume wetu Mohammed (S.A.W.) kwenye safari ya Al-Israa na Al-Miiraj, licha ya mamilioni wa wakristo waarabu ambao nyoyo zao zinafungamana na makanisa ya kihistoria ya “Al-Quds”.
Vile vile, Imamu Mkuu amesisitiza sana kuwa mji wa Al-Quds unaokaliwa na utambulisho wake wa kiarabu na wa kipalestina, inapaswa kuwa ndilo suala lililo muhimu zaidi kwa watu wote wanaohimiza kuenea amani na kupitisha usalama, ili wapalestina na mamilioni wa waarabu na waislamu wasikose imani yao kuhusu umuhimu wa mashirika ya kimataifa na mifumo ya kiutawala. Na magaidi wasipata nafasi na kisingizio cha kuhalalaisha vurugu na uadui, zaidi ya kuchocheza hisia za chuki na kuwasha fitina na mizozo ya kimataifa, mashariki ya ulimwengu na magharibi mwake.

Image

 

Imamu Mkuu anashadidisha kwamba matatizo na migongano ambayo waarabu na waislamu wanayoyatesa, haikubaliki kuwa sababu ya kupuuza uamuzi dhalimu huo, pasipo na kuanza taharuki ya kikweli inayolengea kumaliza ukaliaji na kurudisha haki kwa wapalestina kwa kutangaza kuwa Palestina ni nchi huru na mji wake mkuu ni Al-Quds Al-Shreif. Akiomba mashirika ya kimataifa na pande husika kuchukua hatua ya haraka kwa ajili ya kufuta uamuzi huo na kudhibiti mambo na kuchangia haki za wapalestina.
Na kipindi cha maendeleo yenye hatari hayo, Imamu Mkuu anatoa wito kwa wanachama wa Bodi kuu la Wanavyuoni wa Al-Azhar Al-Shareif na Baraza la Wakuu wa Waislamu kwa ajili ya kufanya kikao cha dharura kwa lengo la kutafiti jambo hilo, pia Imamu Mkuu anatangaza kufanya mkutano wa kimataifa kuhusu suala la Al-Quds, kwa kushiriki kwa wanavyuoni wakuu wa waislamu na wakristo pamoja na baadhi ya mashirika ya kimataifa na ya kinyeji yanayohusiana na suala hilo, ili kutafiti kuchukua hatua za haraka na za kimatendo kwa kuwaunga mkono wapalestina na kuthibitisha kukataa uamuzi dhalimu huo ambao unawanyima haki yao thabiti katika nchi yao na mahali pao pa kitakatifu.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Fikra Kali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.