Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye Msikiti wa Al-Rawda

  • | Tuesday, 12 December, 2017
Hotuba ya Imamu Mkuu kwenye Msikiti wa Al-Rawda

     Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa Rehema Mwenye Kurehemu.
Sifa zote njema ni za Mwenyezi Mungu, swala na amani zimfikie bwana wetu Mtume Mohammad (S.A.W.), familia yake na maswahaba wake.
Hakika matakwa ya Mwenyezi Mungu yametaka kwamba tukio hilo la kigaidi litangulie ukumbusho wa kuzaliwa kwa Mtume (S.A.W.), tukio ambalo limetia uchungu moyoni mwetu sote, na zikatia huzuni hisia zetu, na hatutaweza kufanya chochote isipokuwa kusema: "Inna Lillahi …." hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwa kweli sisi tutarejea kwake mwishoni… na licha ya hayo yote tunajikumbusha nafsi zetu na familiya zetu, wana wa kijiji hiki ambao hawakupinga wala hawakukataa matakwa ya Mwenyezi Mungu kwa kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu: "Nashangaa sana kwa amri ya muumini, hakika hali zake zote zinakuwa kheri kwake, na hii haiwi isipokuwa kwa muumini tu, akipatwa na jambo zuri anashukuru, basi inakuwa kheri kwake, na akipatwa na jambo baya anasubiri, basi inakuwa kheri kwake". Na nyinyi enyi wenyeji wa kijiji hicho hamnahitaji kukumbushwa kwa daraja juu wanayopewa mashahidi peponi wakineemesha ndani yake, wala msidhani kwamba mashahidi wenu wameumiwa wakati walipopigwa kwa risasi kama  maumivu wanayoyapata watu wengine wanapokufa, imepokelewa kutoka kwa Mtume (S.A.W.) kwamba alisema: "kwa hakika shahidi hapatwi na maumivu ya mauaji, ila kwa kadiri ya maumivu ya mbu yanayompata mmoja wenu " .. na inatutosha inayotuzungumzia sheria ya Uislamu kwamba shahidi anakuwa katika daraja juu baada ya Manabii na watu wema.

Image


Ama wauwaji hao waliomwaga damu ya wana wenu katika nyumba takatifu "Msikiti" basi hao ndio Khawarij na waharibifu katika ardhi, na historia yao iliyo na matukio na jinai za kuwauwa waislamu na kuwahofisha wenye amani inajulikana kabisa.
Na Mtume (S.A.W.) Amewasifu watu hao kwa sifa maalumu ambazo tunaweza kuwatambua kupitia kwake, hakika amewasifu kwamba watakuwa wenye umri mdogo, na hilo linaashiria kwamba wao ni wajinga wasio na busara, matendo yao yanafanyiwa bila ya kutafakari na kwa haraka. Pia amewasifu kwa upumbavu wa akili na ubaya wa ufahamu, na ameonya kutoka kudanganyika kwa maumbo yao ya nje na wingi wa ibada zao, na kuhifadhi kwao kwa Qurani Tukufu, ambapo Mtume (S.A.W.) Amesema kwamba wao wanasoma Qurani bila ya kuifahamu wala kuielewa hata kidogo. Vile vile Mtume (S.A.W.) Amewasifu kwa kuvuka mipaka katika dini na kuwakufurisha waislamu kwa ajili ya kuhalaisha kuwauwa, kuzibakua mali zao na kuvunja heshima zao. Pia Mtume (S.A.W.) Ameamrisha kwa kuwauwa na kuwatafutia magaidi hao, akitoa ahadi ya kwamba atakayewauwa magaidi hao, basi atapata thawabu siku ya Qiyama. Hakika limekuja katika hadithi sahihi kwamba Mtume (S.A.W.) Amesema: "Watajitokeza mwisho wa zama, watu ambao umri wao ni mdogo, wajinga wasio na busara, wakitoa dalili kutoka hadithi za Mtume, watasoma Qurani, ilhali Qurani haipita kwenye koo zao (hawana imani, ufahamu wala uelewa kwa aya za Qurani na hukumu zilizomo ndani yake), wanatoka kutoka dini kama mshale unavyotoka katika kiwindwa, basi popote mnapowakuta wauweni, kwani katika kuwaua kuna malipo makubwa kwa atakayewaua siku ya Qiyama".

Image

 

Na Mwenyezi Mungu (S.W.) Amebainisha hatima yao mbaya katika Qurani Tukufu katika aya maarufu isemayo: "Basi malipo ya wale wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawania kufanya uchafuzi katika nchi, ni kuuwawa, au kusalibiwa, au kukatwa mikono yao na miguu yao kwa mabadilisho, au kutolewa nchi. Hii ndiyo hizaya yao katika dunia; na katika Akhera watapata adhabu kubwa" [Al-Maidah:33]
Na kutoka hapa, basi watawala ni lazima watekeleze hukumu ya Mwenyezi Mungu kwa haraka dhidi ya  magaidi hao wanaompiga vita Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kufanya uchafuzi katika ardhi ili walinde roho za watu, mali zao na heshima yao..
Na inawajibikia wenyeji wa Sinai, eneo hilo tukufu kutoka ardhi ya Misri, wanaoteseka sana kwa sababu ya ugaidi huo zaidi ya wengine, bali inawajibika juu ya wenyeji wote wa Misri na taasisi zake zote kulazimika kutekeleza majukumu yao kwa ajili ya kupambana na ugaidi huo wa kikatili, na Misri -Insha’Allah- inaweza kumaliza jambo hilo na kujiokoa kutoka kwa ugaidi, ambapo historia yake, juhudi za wana wake, jeshi na polisi wake- ndizo dalili ya kutosha kwamba nchi hiyo ina uwezo wa kupitia kutoka kipindi hiki kigumu na kuangamiza ugaidi huo ulio haufungamani kabisa na imani ya nchi hiyo na fikra za vijana wake na itikadi zao.
Mwishoni mwa hotuba yangu hii nawaambia wana wa kijiji hiki kizuri kwamba: "Tulikuja hapa kwa ajili ya kusisitiza kwamba sisi sote tunasikia yale mnayoyasikia, na tunaumwa kama mnavyoumwa, na hivyo hivyo Al-Azhar Al-Shareif iliyokujieni kwa Mashekhe wake, wana wake ili kutoa rambirambi na ili kujaribu kupunguza athari za msiba yenu, na pia ili kusaidia kuchangia katika kukiendeleza kijiji hicho katika nyanja za kielimu, kiafya na kijamii.. nikifahamu vizuri kwamba dunia nzima  haitaweza iwe badala ya mtu mmoja kutoka watu hawa wazuri waliokufa, lakini jambo hilo ni kitu kidogo kati ya haki zenu..
Mwenyezi Mungu Awarehemu mashahidi wetu watukufu, na aikinga Misri na nyinyi kutoka fitina, shida na shari, Ameen.


Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.