Uislamu na Suala la Kutendeana na Wasio Waislamu

  • | Tuesday, 16 January, 2018
Uislamu na Suala la Kutendeana na Wasio Waislamu

     Mwenyezi Mungu Amemtukuza mwanadamu bila ya kujali asili, dini na itikadi yake, Mwenyezi Mungu Amesema {Na hakika tumewatukuza wanadamu} (Al-Israa, 70). Na mafundisho ya Uislamu yamewahimiza waislamu waheshimu utukufu wa wanadamu na kuuhifadhi. Basi Uislamu haukuwamirisha waislamu siku moja kuwalemeza wanaotofautiana nao, na kuzichukua haki na mali zao, au kuvunja heshima yao. Kuhusu suala hilo historia ya kiislamu ni wazi kabisa zaidi kuliko nyingie, na pia kuna hati nyingi za kihistoria kuhusu kutendeana na wasio waislamu kama vile, inayojulikana na hati ya Umar Ibn Al-Khattab kwa watu wa Jerusalem "Baitul-Maqdis". Pia kuna dalili nyingine nayo ni kubaki mahali pa ibada kale pa kihistoria kwa mayahudi na wakiristo na wengineo katika nchi za kiislamu hadi siku hizo.   
Uislamu umedhamini haki zote za kibinadamu, na umeanzisha jamii kwa kutegemea misingi muhimu kama vile: uadilifu, usawa, kufanya wema na hisani. Mwenyezi Mungu Amesema: {Hakika Mwenyezi Mungu anaamrisha kufanya uadilifu, na hisani} (Al-Nahl, 90), na Amesema pia, {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu} (Al-Mumtahnah: 8) na Amesema: {Enyi mlio amini! Kuweni wasimamizi madhubuti kwa ajili ya Mwenyezi Mungu mkitoa ushahidi kwa haki. Wala kuchukiana na watu kusikupelekeeni kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu. Hivyo ndio kuwa karibu mno na uchamngu. Na mcheni Mwenyezi Mungu. Hakika Mwenyezi Mungu anazo khabari za mnayoyatenda} (Al-Maida: 8). Aya zote hizo zinatuamrisha kuwatendeana na watu wote ambao hawafanyi uadui na waislamu bila ya kujali itikadi yake, na kwa mujibu wa aya hizo zimewajibika juu ya waislamu haki nyingi kwa wasio waislamu -hasa wakristo- kwa uadilifu, na kufanya wema na hisani. Na huyo Mtume Mohamed (S.W.A.) amewausia masahaba wake kuwatendea wema na wakristo, ambapo Alisema: "mkiingia Misri basi wafanyie wema wakristo wake kwani wana ahadi na ukoo" katika hadithi hiyo neno "ahadi" linamaanisha kwamba wakristo wana haki na heshima, na neno ukoo linamaanisha kuwa Bibi Hagar "mama wa Ismail" (A.S) kutoka kwa Misri na kuwa Mariyya "mama wa Ibrahim" pia kutoka kwa Misri.

Image



     Kwa hivyo, miongoni mwa hisani na kufanya wema kwa wakristo ni kupongezana nao katika Idi zao kwa maneno yasiyopingana na itikadi ya kiislamu, na jambo hilo halitoki mbali na dini kama wanavyodai baadhi ya watu wenye fikra kali na wasijui kuwa matini ya kisheria ni matini yanayokamilina na kila matini yanaafikiana na tukio maaluma, aidha Mtume (S.W.A) Amekubali zawadi za wasio waislamu, akafanya ziara kwa wakongwa wao, akawatendeana nao, akawaomba msaada wao katika hali ya usalama na ya vita na amesameheana nao, kila hayo yanaingia chini ya usamehevu wa waislamu na wasio waislamu. Zaidi ya hayo, Mwenyezi Mungu hakutofautisha kuhusu kuamkia baina ya waislamu na wasio waislamu Aliposema: {Na mnapoamkiwa kwa maamkio yoyote, basi nanyi itikieni kwa yaliyo bora kuliko hayo, au rejesheni hayo hayo…} (Al-Nisaa, 86) na hongera ya Idi sio isipokuwa aina ya maamkizi.
Na kwa upande mwingine wakristo ni jirani yetu nchini Misri na wana haki zote za jirani, na Mtume (S.A.W) ametuusia kutendeana na jirani kwa kheri sawa sawa akiwa mwislamu au asiye mwislamu; imesimuliwa kutoka kwa Mujahid kwamba mbuzi amechinjwa kwa ajili ya Abdullah Ibn Amr (R.A), basi alipoingia nyumbani akasema: "je mmempa jirani yetu myahudi? mmempa jirani yetu myahudi? Nimesikia Mtume (S.A.W) anasema "Jibrili ameendelea kuniusia kwa jirani mpaka nikadhani kwamba atampa urithi" imepokelewa na Abu Dawood na al-Termedhi.
Hitimisho, kutendeana na wasio waislamu kusamehena nao na kupongezana ni misingi asili ya kidini ambayo waislamu ni lazima waitekeleze.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.1

Please login or register to post comments.