Al-Azhar na Al-Quds (Jerusalem) .. Misimamo kupitia Historia

  • | Wednesday, 17 January, 2018
Al-Azhar na Al-Quds (Jerusalem) .. Misimamo kupitia Historia

      Kwa hakika suala la Kipalestina lilikuwa na linaendelea hadi hivi sasa kupata shime kubwa kwa upande wa Al- Azhar Al-Shareif ambayo inashikilia kuunga mkono kwa Al-Quds na Al-Aqsa katika wakati wote, Al-Azhar daima inasisitizia kuwa suala hilo ni la itikadi, sio suala la nchi iliyokaliwa na mamlaka ya kizayuni tu, bali ni suala la mahali patakatifu ya Kiislamu na ya Kikristo. Suala hilo pia si suala la kitaifa la Palestina tu, lakini ni suala la nchi za Kiarabu, na kwamba waislamu wakati wanapopigana ili wakomboe kutoka ukaliaji wa Kizayuni, basi wanatakiwa wathibitishe utakatifu wa suala la Al-Quds, na hii inapasa kuhamasishwa na watawala wote wanaohusiana na suala hilo lenye utakatifu ili wamalize ukaliaji wa Israeli na wakatae majaribio ya kubadilisha utambulisho wa Al-Quds kutoka uarabu kwenda uzayuni.
Vile vile jambo linalojulikana kwa wote ni kwamba juhudi za Al-Azhar Al- Sharief kuhusu suala la Palestina na Al-Quds Al-Sharief zilianza tokea mwaka wa 1348 AH / 1929, na jukumu la Al-Azhar lilikuwa maarufu hasa baada ya tangazo lililoitwa "Nchi ya Israeli" mwaka wa 1948, ambapo Al-Azhar Al-Sharief ilichukua hatua nyingi na ikafanya mikutano mingi ya Kiislamu katika ndani na nje ili ipambane na tangazo hilo.
Na misimamo ya Al-Azhar kupitia historia yote kuhusu masuala ya kipalestina kama vile: kukataa majaribio ya kubadilisha utambulisho wa Al-Quds Al-Sharief, uthibitisho wa Uarabu wa Al-Quds kama nchi ya Kiarabu inayotawaliwa na wapalestina na kuwa Al-Quds ndiyo ni mji mkuu wa nchi ya Palestina, inajulikana kwa wote. Na miongoni mwa misimamo hiyo:
Fatwa ya Sheikh Al- Azhar ya zamani Sheikh Abdul Majied Salim, ambaye ametoa fatwa inayoharimishia mtu yeyote kuuza ardhi yake kwa Wayahudi, kwani Waislamu kwa ujumla na wapalestina wamejifunza kwamba jambo hilo linawasaidia Wayahudi kufikia matakwa yao ya kumiliki nchi ya Palestina na kubadilisha utambulisho wake.
Na baada ya tangazo la Umoja wa Mataifa katika Novemba 29 mwaka 1947 kuhusu uamuzi wa kugawanya Palestina, wanachuoni wa Al-Azhar walitoa taarifa yao ya kukataa uamuzi huo na wameeleza kuwa uamuzi huu ni “uamuzi wa wasiomiliki na unazingatiwa ni batili, kwani nchi ya Palestina ni ya Waarabu na ya Waislamu ambao wamejitoa nafsi zao na damu zao zenye kutaharisha kumwagawa kwa ajili ya kutetea suala la nchi hiyo.. na hakuna mtu yeyote anayeweza kuwashindana nao”.

Image

 

Na katika mwezi Aprili mwaka 1948, mkutano ulifanyika katika kumbi kuu huko Al-Azhar Al-Shareif chini ya usimamizi wa Sheikh Al-Azhar na kujumuisha idadi kubwa ya wanachuoni wa Al-Azhar ili kujadili suala la Palestina, na Wameafikiana kuwa uokoaji wa Palestina ni wajibu wa kidini kwa Waislamu wote duniani, na ili kufikia jambo hilo ni lazima serikali zote za kiislamu na kiarabu ziunge mkono na zichukue hatua zingi kwa ajili ya  kuokoa Palestina, na ni lazima kila mwislamu au mwarabu atoe fedha na nafsi kwa ajili ya kusaidia serikali katika jambo hilo.
Sheikh Muhammad Maamoun Al-Shennawi alikuwa ni Sheikh wa Al-Azhar wakati wa vita vya 1948, na ametoa fatwa yake ya kuruhusu jihadi ambayo ilikuwa ni  kama kichocheo kikubwa kwa majeshi wa Misri walioshiriki pamoja na majeshi ya Kiarabu katika vita hivyo ili nchi ya kipalestina ipate uhuru wake baada ya tangazo lililoitwa "kuanzisha dola ya Israeli".
Sheikh Abdul Haliim Mahmoud pia alitoa fatwa yake kuhusu suala hilo, ambapo amebainisha kwamba "Waarabu wa Palestina walifukuzwa kwa nyumba zao bila ya haki, walitawanyika na waliondoka. Na Waarabu waliobakia wanatesa sasa. Na wajibu wa nchi zote za Kiislamu zichukue hatua haraka haraka na zifanye juhudi kubwa kwa ajili ya kurudisha Palestina iwe Kiarabu, kwani vita vya sasa ni vya utetezi wa matakatifu.. na wale ambao wanakimbia nyuma, basi hao si waaminifu”.

Image

 

Katika mkutano wa pili wa halmashauri ya Utafiti wa Kiislam mwaka wa 1965, washiriki walitakia watu wote waache kukiri kuwepo kwa Israeli, na kwamba nchi za Kiislamu ni lazima ziache kushirikiana na Israel, na wanasisitiza kwamba suala la Palestina ni suala la Waislamu wote na hakuna mapumziko mpaka nchi takatifu ya Al-Quds Al-Sharief irudi kwa watu wake, kwani kuwepo kwa Israeli kunazingatiwa kama ni tishio kwa Msikiti wa Al-Aqsa na kama ni njia ya kufikia misikiti miwili takatifu na kaburi la Mtume (S.W.A).
Vile vile Al-Azhar ilitoa taarifa yake kabla ya vita vya Juni 1967 kuhusu shambulio la shambulio la Israeli kwa Palestina, ambapo imebainisha kwamba “ shambulio la Israeli na kuwepo kwake ndani ya nchi Takatifu ya Al-Quds Al-Sharief ni hatari kubwa kwa makao matakatifu ya Kiislamu na kunazingatiwa kama ni tishio kwa Msikiti wa Al-Aqsa na njia ya kufikia misikiti miwili mitakatifu, na imetoa wito kwa Waislamu wote kushiriki katika vita na anayeacha kushirika katika vita hivyo basi ni mwenye dhambi”.
Na Al-Azhar Al-Shareif hakuacha kuunga mkono na Wapalestina na kuwanusuru ili wapate haki yao na walinde maeneo matakatifu huko Palestina. Kwa mfano, wakati wa Sheikh Gad al-Haq, nchi ya Marekani ilihamisha ubalozi wake kutoka Tel Aviv kwenda Al-quds (Jerusalem) mwaka 1995. Basi, Al-Azhar ilitoa taarifa yake ya kukataa uamuzi huo na iliuita kama ni "msaada kwa wasio haki". Na Al-Azhar imezingatia kuwa Uamuzi wa Baraza la Mashauri ya Marekani kama ni wa kuthibitisha ukaliaji wa Israeli kwa Al-Quds.
Na taarifa hiyo iliongeza kuwa: "Al-Azhar Al-Sharief inakataa uamuzi huo usiofaa kutoa kwa upande wa dola la Marekani linalotafiti kukamilisha kazi ya amani, ambapo uamuzi kama huo ulithibitisha kwamba wawakilishi wa amani wamekuwa wa uongo na khiyana, na kuwa wawakilishi hao wanatafiti ili kuharibu ardhini".
Na kwa upande wa Sheikh Gad Al-Haq, aliyekuwa ni Sheikh wa Al-Azhar Al-Sharief, basi suala la Al-quds lilichukua shime kubwa ya akili na moyo wa Imamu mkuu marehemu huyo, na amesisitiza katika nafasi zake zote na misimamo yake yote kwamba Al-quds itabakia Kiarabu na Kiislam hadi siku ya kiama.
Pia, imamu marehemu Sheikh Gad Al-Haq alikuwa na msimamo wazi na imara anapokataa kupokea Rais wa Israeli Ezer Weizman wakati wa ziara yake Kairo baada ya kufanyika makubaliano ya Oslo ya 1993, jambo ambalo lilisababisha mashaka makubwa kwa serikali ya Misri na Rais wa kizayuni. Imamu wa marehemu pia aliyakataa yaliyosemwa kwamba Israeli itapata maji ya Nile kupitia mradi wa mfereji wa amani. Na alisema kauli yake maarufu zaidi ya kuwa: "Ufikiaji wa maji ya Nile kwa Israeli ni jambo muhali sana".
Wakati wa Dk. Tantawi, Sheikh Al-Azhar, alisisitiza juu ya nia yake ya kwenda kwenye mji wa Al-quds ikiwa hali ya usalama na hali ya kisiasa inaruhusu, ikiwa ni faida kubwa ya kutatua suala la Palestina. Tantawi aliziita nchi za kiarabu, za Kiislamu na za heshima duniani ili zisimame pamoja na Palestina na kupiga kura kuhusu kuanzisha nchi ya Palestina na kuwa Al-quds kama ni mji mkuu wake, na alitoa wito kwa ulimwengu usimame dhidi ya uamuzi wa Marekani baada ya imetangaza kutumia haki yake ya kupiga kura ya veto, kwani Palestina ina haki ya kuishi kwa amani na utulivu kama ni hali ya nchi zingi.
Dk. Tantawi pia alisisitiza kwamba upendeleo kamili wa Marekani kuhusu masuala muhimu zaidi ni wa suala la Palestina na mamlaka dhalimu ya Kizayuni, ambao umeongeza hali ya chuki na kukata tamaa kuhusu haki ya utawala wa Marekani, na utaongeza msimamo wa Al-Azhar Al-Sharief kuhusu kuunga mkono na kusaidia watu wa Palestina ili waanzishe nchi yake huru na kuwa Al-quds kama ni mji mkuu wake.
Uamuzi wa Rais wa Marekani Donald Trump ya kutangaza kwamba Al-quds kama ni mji mkuu wa mamlaka dhalimu ya Kizayuni, umefanya hali ya kukataa zaidi katika ulimwengu wa Kiarabu na wa Kiislamu, kwa viwango vyake viwili vya wananchi na vya serikali. Na wakati huo huo, Imamu Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharief Profesa Ahmad Al-Tayyib alitoa majibu ya haraka ya kuhimiza hisia za wanachuoni wa umma Kote ulimwenguni ili waelekee kulinusuru suala la Al-Quds.
Taarifa ya Shiekh Al-Azhar imekuja baada ya kukataa kwake kumpokea makamu wa Trumb Mike Bens, akisisitiza kwamba yeye hatakutana na wanaobadilisha historia, akisema: Inakwaje, nikutane na walioyapa wasiyoyamiliki kwa wasioyastahiki? akisisitiza kwamba Trumb anapasa kufuta uamuzi huo usio wa kisheria na wa kanuni. Pia kuna amuzi zingine ambazo kuchukuliwa na Imamu Mkuu Ahmad Al-Tayyib kwa ajili ya kusaidia kunusuru suala la Palestina kama vile tangazo la kufanyika mkutano wa Al-Azhar na wakuu wa waislamu unaofanyika tarehe 17-18 januari.
Na kwa sababu hiyo, Al-Azhar Al-Sharief itabakia kupitia enzi zote kuwaomba watu wote wa ulimwengu kuinusuru haki ya Kiarabu na kujitahidi katika ukombozi wa Al-quds na kurejesha haki ya Wapalestina.

Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na Mawazo Makali
Kitengo cha Lugha za Kiafrika

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.