Hijrah Ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) “Mafundisho na Mafunzo”

  • | Friday, 14 September, 2018
Hijrah Ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) “Mafundisho na Mafunzo”

   Wasomaji wetu waheshimiwa!!!

Jueni Zaidi Kuwa Kalenda ya Hijriy imeanzia pale Mtume Muhammad (s.a.w.), pamoja na Maswahaba wake, walipohama Makkah na kwenda Madinah, kukimbia dhuluma za makafiri.

Vile vile! Hijrah inatukumbusha vipi Mtume (s.a.w.) na Maswahaba wake walivyodhulumiwa, walivyoteswa, na walivyonyanyaswa, na makafiri wa Makkah, na hatimaye wakapanga kumwua Mtume (s.a.w.) ili waizime nuru ya Uislamu. Lakini vitimbi vyao hivyo vikashindwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu Akamnusuru Mtume wake (s.a.w.) kwa kumpa amri ya kuhama Makkah na kukimbilia Madinah. Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: “Ikiwa nyinyi hamtamnusuru Mtume, basi Mwenyezi Mungu alikwisha mnusuru walipo mtoa walio kufuru, naye ni wa pili katika wawili walipo kuwa katika pango, naye akamwambia sahibu yake: Usihuzunike. Hakika Mwenyezi Mungu yu pamoja nasi. Mwenyezi Mungu akamteremshia utulivu wake, na akamuunga mkono kwa majeshi msiyo yaona, na akalifanya neno la walio kufuru kuwa chini, na Neno la Mwenyezi Mungu kuwa ndilo juu. Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye nguvu Mwenye hikima”. (At-Tawba: 40).

Miongoni mwa mazingatio na mafunzo muhimu yanayotokana na Hijrah ya Mtume wetu Muhammad (S.A.W) ni yafuatayo:

- Hijrah inatupa funzo la wazi kuwa Waislamu ni wadugu, bila ya kujali kabila, taifa, rangi n.k.

- Ni muhimu sana, katika wakati huu, Waislamu kuwa na umoja na mshikamano, na wanashauriana katika mambo yao yote.

- Ni lazima kwetu tuyahame yale maovu yote tuliyoyatenda huko nyuma, na kusababishia katika hali hii duni tuliyo nayo hivi sasa. Tusisahau kuwa Mtume wetu (s.a.w.) alipohama Makkah kwenda Madinah ndiyo akapata nusura ya Allah (s.w.).

- Ni muhimu kuweka mipango tunayotaka kuyafanya kabla ya utekelezaji.

- Kama waislamu wakashindwa kupata mazingira yatakayowawezesha kuishi katika kila vipengele vya maisha, hawana budi kuhama kwenye eneo lingine katika ardhi ambapo wataweza kumwabudu Mola wao vilivyo.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.3

Please login or register to post comments.