Katika hotuba msikitini mwa Al-Azhar huko Jakarta .. Imamu Mkuu ailinda itikadi ya watu wa Sunna huko Asia ya kusini kwa kuanzisha kumbi za kufundisha sheria

  • | Thursday, 25 February, 2016
Katika hotuba msikitini mwa Al-Azhar huko Jakarta .. Imamu Mkuu ailinda itikadi ya watu wa Sunna huko Asia ya kusini kwa kuanzisha kumbi za kufundisha sheria

Mheshimiwa Imamu Mkuu profesa; Ahmad Al-Taiyb, Sheikhi Mkuu wa Al-Azhar Al-Sharief, Mkuu wa Baraza la Wakuu wa Waislamu, ametoa hotuba katika msikiti wa Al-Azhar Al-Sharief katika mji mkuu wa Indonisia Jakarta akiwatoa shauri wanafunzi kwa umuhimu wa kushikaman na mbinu ya kiwastani ambayo ni ujumbe wa Al-Azhar; Msikiti na Chuo kikuu.

Yule Mheshimiwa amesema kwamba Al-Azhar Al-Sharief kwa zaidi ya miaka elfu moja ndiyo mlinzi wa utamaduni wa ummah na imani yake, akibainisha kuwa siri ya kubaki kwa Al-Azhar Al-Sharief ni kuwajumuisha waislamu wote, ambapo imepata upendo mkubwa na kuheshimiwa na waislamu wote pande zote duniani mashariki na magharibi.

Na Imamu Mkuu ameongeza kwamba Al-Azhar Al-Sharief daima hufanya umoja wa waislamu ni lengo lake kuu katika wito zake zote, ambapo haiashirii mtu hasa kwa kutoa wito ya undugu na kuishi pamoja baina ya waislamu wote, Al-Azhar Al-Sharief ilikuwa na ingali inajaribu kuwaunganisha waislamu juu ya lengo moja, kwani nyezo za waislamu si chache zaidi kuliko zile za wanachama wa Umoja wa Ulaya ambao, licha ya kutofautiana kwao katika lugha na imani na mengineyo, lakini wameafikiana juu ya malengo na maslahi ya pamoja, kwa hiyo basi, tunahitaji umoja katika lengo na kutoa mfano wa kipekee katika ushirikiano wa pamoja.

Yule Mheshimiwa ametamani kuwa msikiti huu ــ ulioitwa kwa msikiti wa Al-Azhar ــ unakwenda sambamba na mtaala wa Al-Azhar Al-Sharief uliopo nchini Misri; ukalingania katika njia ya Mwenyezi Mungu juu ya msingi wa ufahamu na kuimarisha fiqhi ya kuishi pamoja kati ya wananchi wa Indonisia ambao kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ni wananchi wanaopendelea amani na utulivu, wananchi hao waliowez kwa juhudi zake na kulishikamana na dini kutoa mfano mzuri wa kuigwa kwa zile tabia anazotakiwa mwislamu wa kisasa awe nazo akiwa anakusanya baina ya uhalisi na upya kwa pamoja na maelewano.

Na Mheshimiwa Imamu Mkuu amewapendekezea wasimamizi wa msikiti huu kuanzisha kumbi tofauti za kufundisha taaluma za kisheria: ukumbi wa kufundisha fiqhi ya Imamu Malik, ukumbi wa kufundisha fiqhi ya Imamu Shafei, ukumbi wa kufundisha fiqhi ya Imam Abu Hanifa, ukumbi wa kufundisha fiqhi ya Imamu Ahmad. Pia Yule Mheshimiwa ametoa shauri kuhusu umuhimu wa kuanzisha ukumbi wa kusoma Sahihi ya Al-Bukhari kimafunzo na kimasimulizi, na ukumbi mwingine wa kufundisha sera ya Mtume Muhammad (S.A.W), akawaahidi wale wasimamizi wa msikiti kuwasaidia kwa maprofesa bingwa kwa ajili ya kufundisha katika kumbi hizo, ambazo Mwenyezi Mungu Akitaka zitachangia kuhifadhi itikadi za wasunni wa Asia ya Kusini na kulinda umma kutoka wito zote za uharibifu.

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.