Uislamu na Usekyula

Swali la Kwanza: Usekyula na msimamo wa Uislamu kuhusu yake

  • | Friday, 28 August, 2015

Kabla ya kuanza kujibu tunataka kusema: ilikuwa ni lazima usekyula na wafuasi wake waulizwe kuhusu Uislamu na msimamo wao kuhusu Uislamu kiakida, kisheria na mbinu ya maisha, na baada ya kubainisha msimamo wa usekyula kuhusu Uislamu kwa pande hizo zote wakati huu inaweza kueleza msimamo huo wa usekyula kwa Uislamu, na tunaweza kubainisha maoni ya usekyula kuhusu Uislamu na uliyoyajia kati imani, sheria, mwenendo na mbinu ya maisha, baadaye tunaweza kuuuliza Uislamu swali:  je, msimamo wako nini kuhusu usekyula?
Baada ya kubainisha hayo Uislamu unaweza kutoa jibu wazi la swali hilo, na swali kama hilo inawezekana kusababisha kujuana baina ya pande hizo mbili (Uislamu na Usekyula), ambapo usekyula unazingatiwa siku hizi ni madhehebu maalum, inayo itikadi yake hasa, mwono wake wa kijumla, vyanzo vyake vya kimafunzo, mbinu zake za maisha, basi ni dini iliyotungwa na mtu wa kisasa ili iwe badala ya dini iliyotungwa na kuteremshwa na Mungu, mbali na mwanadamu, inayowalazimisha wanadamu kwa hali maalum ya lazima kuhusu itikadi yake, maoni yake ya kijumla, mbinu za maisha yake, mifano ya kuigwa ya maarifa yake, na madhehebu hiyo inafungamana na tafsiri ya matukio, mawazo, maoni, mielekeo na vitendo. Haya yote yanamlazimisha muulizaji atupe maoni hayo, lisije swali kinyume na muktadha wake, na likatumiwa mbali na mazingira yake.
Hakika wenye kutoa dhana na maelezo hawakuweza kuafikiana kuhusu dhana maalum ya usekyula, wakataja kwamba usekyula ina zaidi ya dhana kumi na sita, kila dhana kati ya dhana hizo inaieleza kwa upande fulani ikipuuza pande nyingine, kwa hiyo anayewauliza waislamu juu ya msimamo wa Uislamu kuhusu usekyula anapaswa kutubainisha aina ya usekyula ambayo anataka Uislamu uukubali na kutangaza kuambatana nao, kabla ya kuomba kueleza msimamo wetu kuhusu madhehebu hiyo, na vipi tunaweza kuandaa jibu la kutosha linalostahiki lipate ridhaa ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake.
Ili tusiliacha mlango u wazi kwa mizozo kuhusu jambo hilo tunahakikisha kwamba watafiti wakubwa zaidi waliosoma usekyula na walifuatilia historia yake wamefikia matokeo yafuatayo: usekyula uliopo unamaanisha kuwepo uhamiaji kutoka hali ya kibinadamu kwenda hali ya kimguso, kwa maana ya uhamiaji kutoka kuhusiana na mwanadamu kwenda kuhusiana na mazingira, maana uahmiaji kutoka kumfanya mtu kama ni mungu na unyenyekevu wa mazingira kwa kuifanya mazingira yenyewe ni mungu na kwamba mwanadamu anapaswa kuwa mnyenyekevu kwake na kanuni zake, maana usekyula huu ni kujishughulikia falsafa ya mambo ya mguso.
Na kwamba usekyula unagawanyika katika mafungu mawili, usekyula hasa na usekyula wa kijumla.
1-    Usekyula hasa: ni maoni hasa kuhusu hali halisi bila ya kutendeana na mambo ya kijumla na ya kimafundisho, kwa hivyo hauwi wa kijumla, na maoni hayo yanaelekea kuwajibika kutengana baina ya dini na siasa, nap engine uchumi pia, jambo linaloelezwa kwa ibara ya "kutenga dini na siasa", na maoni hasa kama hayo hayahusiani na nyanja nyinginezo maishani, na wala hayakani kuwepo mambo ya kijumla au tabia au kuwepo kwa mitafizikia, na inaweza kuuita "usekyula waenye tabia" au "usekyula wa kibinadamu".
2-    Usekyula wa kijumla: nayo ni maoni wa kijumla kwa hali halisi yanayojaribu kwa bidii kuambatanisha baina ya dini, maadili ya kijumla na mambo yasiyoonekana katika nuanja zote za maisha, na kutokana na maoni hayo mitazamo inayozingatia mambo ya mguso kuhusu ulimwengu na kuwa maarifa ya mambo ya mguso ni chanzo cha kipekee cha tabia na kwamba mwanadamu huwa na tabia ya kupendeleza mambo ya kimguso sio ya kiroho, yanayoitwa "Usekyula wa kimguso".
Tofauti iliyopo kati ya linaloitwa "Usekyula hasa" na linaloitwa "Usekyula wa kijumla" inazingatiwa ni ile ile tofauti iliyopo baina ya vipindi vya kihistoria vya maoni hay ohayo, ambapo usekyula ulisifika kwa kujishughulikia nyanja mbili za kiuchumi na kisiasa wakati ambapo mabaki ya maadili ya kikristo ya kibinadamu yamebakia, na pamoja na kuingiliana kwa nchi na mashirika yake na maisha ya kila siku ya kila mmoja nchi inayofuata madhehebu ya usekyula imejihusisha na kuunda maoni ya kijumla ya maisha ya binadamu mbali na mambo yasiyoonekana, baadhi ya watafiti wamezingatia kwamba "usekyula wa kijumla" ni alama wazi ya linaloitwa "usaliti wa nchi juu ya dini" .
Basi usekyula hasa unafungamana na linaloitwa kutenga dini na kanisa katika historia ya Ulaya, na usaliti wa nchi juu ya pesa za kanisa, na kuzigeuza pesa hizo ziwe za jamii nzima, na kutokana na yanayopitishwa na viongozi wa kisiasa na kiuchumi, na jambo hilo linajumuisha masuala mengi, yanayohusiana na siasa na uchumi, na kwa ajili ya mwanachuoni wa fiqhi na mwana sheria watoe maoni yao kuhusu mambo hayo ni lazima yatolewe kupitia kwa maswali madogo madogo na ya moja kwa moja ili mwana fiqhi na mwana sheria waweze kuyajibu jibu lililo sawa, wakibainisha yanayokubalika na yanayokataliwa kati ya hatua hizo, na tunaweza kusema umma wetu wa kiislamu labda hauteseki ila katika uwanja wa kundi la kishiia, kwani washiia wanalipa khumsi, zaka, michango na sadaka kwa wanaowafuata kati ya maimamu wao wa kidini, na baada ya muda maimamu hawa wanaweza kuunda vituo vyenye nguvu vya kutosha kusumbua serikali kwa sababu ya usaliti na pesa zake, na uwezo wake unaoambatana na pesa, juu ya kupitisha matakwa yake juu ya watawala, ama kwa upande wa sunna hakuna cho chote kati ya mambo hayo, yaliyotajwa hapa ni kuhusu usekyula hasa.
Ama kuhusu usekyula wa kijumla basi ni kama tulivyodokeza ni madhehebu nyingine, na dini kamili inayojitokeza kuwa hivyo kuanzia mwono wa kijumla, mbinu, na kanuni, ambapo mwanachuoni mwislamu wa fiqhi hawezi kukiri kwa umbo hilo la kijumla, na lazima kugusia baadhi ya maelezo ya ziada.
Lakini usekyula katika nchi za magharibi umeendelea sana, hatukujua kwamba umepata maendeleo kama hayo mbali na mifumo ya kidemokrasia ya magharibi. Na hayo ni kwa sababu zisizofichika kama vile kuwa wamagharibi wanautekeleza usekyula kimatendo, na wanaweza kugundua moja kwa moja kasoro na dosari zilizopo katika falsafa na fikira za kisekyula na hatua zinazotokana na fikira hiyo, pia misimamo yao inawezekana kubadilika kwa urahisi, kuhusu dini, utaifa, maendeleo na dhana zote za kimsingi ambazo zinaliwaza akili ya kisasa.
Pamoja na hayo, usekyula umekua katika mazingira ya kisiasa na kiuchumi nyingine inayotofautiana na mazingira yetu, ambapo umekua barani Ulaya ukiambatanishwa na mgongano mrefu baina ya kanisa na nchi ulioendelea kwa vipindi virefu, mawazo ya kisekyula yakaanza kujitokeza barani Ulaya mnamo karne kumi na sita, kwa ajili ya kuyatatua matatizo hayo.
Jamii zetu za kiislamu zina haja ya kuwabinishia walinganiaji nyanja za kazi yao kwa makini, ili wazielekea na kujishughulikia nazo, na wazihudumu dini na jamii kupitia kwa kazi hiyo, na hilo ni jambo ambalo serikali za kiislamu zinaweza kulifanya mara kwa mara, ili kuirekebisha hali, ikitokea ufisadi wa aina yo yote.
Basi matendo ya nchi yanatengana na matendo ya daawa, na badala ya kujitaabisha na kuingia mashaka kuhusu dhana hatukuhusiana na namna ya kuziunda, na hazikujitokeza nchini mwetu, wala hatukushiriki katika kuziunda kwa bongo zetu, basi ni jambo lisilostahiki tujishughulikia nalo, tukazidisha sababu za kuzuka migogoro katika jamii zetu.
Na Mwenyezi Mungu Anajua zaidi

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.0

Please login or register to post comments.