Hali ya mwanamke chini ya utawala wa kundi la kigaidi la Daesh ikilinganishwa na hali yake katika Uislamu

  • | Friday, 7 August, 2015
Hali ya mwanamke chini ya utawala wa kundi la kigaidi la Daesh ikilinganishwa na hali yake katika Uislamu

Hakika Qurani Tukufu inapozungumzia chimbuko la binadamu, imemfanya mwanamke mshiriki pamoja na mwanamume katika chimbuko hilo. Qurani tukufu ikafanya hayo ni neema juu ya mwanadamu inayostahiki shukrani.
Maana ya hayo ni kwamba hakuna tofauti baina ya mwanamke na mwanamume kwa upande wa ubinadamu, na kwamba pendeleo baina ya wanadamu inategemea sifa nzuri ambazo zinachangia kutakasika kwa ubinadamu.
Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi" {Suratt Al-Nisaa aya 1}.
Hakika Uislamu umethibitisha pia kukidhi silika ambayo mwanamke anaumbuwa nayo ni "utu wenye akili na ufahamu" na kwamba mwanamke ana jukumu la pekee mbali na jukumu la mwanamume, ambapo yeye ni mhusika wa nafsi yake, ibada zake na nyumba yake na jukumu la mwanamke halipunguzi na jukumu la mwanamume, na kwamba daraja yake katika thawabu na adhabu mbele ya Mwenyezi Mungu inafungamana na matendo yake mema au maovu.
Mwanamke anahesabiwa mwenywe, na mwanamume anahesabiwa mwenyewe, na jukumu la mwanamke sio jukumu hasa juu ya ibada tu, bali ni jukumu la kijumla katika kukidhi wajibu zake za kijamii kuhusu kuagiza mema na kukataza maovu na roli yake ya kijamii kwa mujibu ya masomo yake.
Lakini baada ya kujitokeza kundi la kigaidi la Daesh, baadhi ya mawazo makosa na ufahamu mbaya kwa dini ya kiislamu zimejitokeza.
Miongoni mwa mawazo hayo wazo la kundi hilo kuhusu mwanamke na namna ya kutendeana naye ambapo zilijitokeza fatwa kadhaa pamoja na kujitokeza kwa kundi hilo zinazoruhusu kuwateka wanawake na watoto wasio waislamu, na kutendeana na wanawake kama miliki wa mkono wa kulia na pia kuruhusu kuwauza na kuwapa kwa wengine kama tuzo.
Na tukiangalia wazo hilo tunajua kwamba kundi la kigaidi la Daesh linafahamu dini ya kiislamu kikosa, ambapo miongoni mwa malengo ya dini ya kiislamu ambayo hakuna anayeweza kuyakana ni kuondoa utumwa kwa namna zake zote, ambapo Uislamu umefuata mbinu ya pekee katika kuondoa vyanzo vyote vya utumwa na kwa upande mwingine umefungua milango ya ukombozi kutoka utumwa na umeufanya kafara ya dhambi kupitia kwa kuwapa uhuru watumwa, isitoshe bali umezidisha thawabu ya anayampa watumwa uhuru wao kwa ajili ya kujikaribisha na kuamini kwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu amesema "Lakini hakujitoma kwenye njia ya vikwazo vya milimani. Na nini kitakujuvya ni nini njia ya vikwazo vya milimani?. Kumkomboa mtumwa" {Suratt Al-Balad aya 11-13}.
Na miongoni mwa mawazo makosa ya kundi hilo kuhusu mwanamke, pamoja na vitendo visivyo vya kibinadamu wanavyovitendea mwanamke; ni kupitisha vikwazo juu yake kama; kuwazuia wanawake kuvaa nguo za rangi, kuzuia kuonyesha macho licha ya uso, na kuwapiga wanawake marufuku ya kutoka nje ya nyumba zao.
Na tukiangalia mawazo hayo tutagundua kuwa kundi hilo la kigaidi na wanachama wake hawajui cho chote kuhusu heshima inayopewa na Uislamu kwa mwanamke ambaye alipewa nafasi ya juu Uislamu, ukamfanyia karama kinyume na dini nyinginezo; ambapo wanawake katika Uislamu ni washiriki wa wanaume, na watu wema zaidi ni watu walio wema kwa familia zao, kwa hivyo mwislamu wa kike ni mpenzi na moyo wa wazazi wake na ndugu zake.
Na mwanamke akiwa mkubwa basi yeye ni mheshimiwa, na waliy wake anamhofia, na anamlinda, na hataki kupatwa na adha yo yote, kwa mkono, ndimi au macho.
Na akiolewa basi hayo inakuwa kwa neno la Mwenyezi Mungu, na ahadi yake nzito; basi inakuwa nyumbani mwa mume wake katika urafiki ulio bora zaidi, na inapaswa kwa mume wake kumheshimu na kumtendea kwa upendo, na kumzuia madhara.
Na akiwa mama, basi utiifu wake ulikuwa unafungamana na haki ya Mwenyezi Mungu na kumwasi na kutomtii kulikuwa unafungamana na kumfanyia Mwenyezi Mungu mshiriki, na ufisadi ardhini.
Na akiwa dada, inalazimu kumheshim, kumkirimu na kumhifadhi.
Na akiwa mjomba amekuwa kama mama kuhusu kumtii na kumkirimu.
Na jamii za kiislamu bado zinazingatia kabisa haki hizo, jambo hilo limemfanya mwanamke mwenye thamani na heshima kinyume na jamii zisizo za kiislamu.
Kisha mwanamke katika Uislamu ana haki ya umiliki, kukodesha, uuzaji, ununuzi na mikataba mingine, na ana haki katika kupata elimu na kujifunza pasipo na kuvuka misingi ya dini.
Bali mwanamke ana haki kama mwanamume ila katika baadhi ya mambo ambayo yanamhusu kinyume na wanaume au yanayowahusu wanamume kinyume naye kati ya haki na hukumu ambayo yanaambatana na kila mmoja wao kama itabainishwa katika mahali pake.
Vile vile, miongoni mwa mawazo mabaya ya kundi hilo kuhusu jihadi ya kijinsia, maana yake ni kwamba wanachama wa kundi hilo wanafanya mkataba wa ndoa pamoja na wanawake kwa muda mdogo sana pengine haudumu zaidi ya saa moja kisha baada ya saa hii wanawatalaka kwa ajili wanachama wote wa kundi hilo wanapata furaha, na dalili zao ni baadhi ya fatwa zisizo za kawaida ambazo zisizoambatana na Uislamu, na wanavyuoni wanajibu suala hilo kwamba ni zinaa wazi na ni haramu, na pamoja na mawazo mabaya hayo ya kundi hilo la kitakfiri kuhusu mwanamke ila kwamba kundi hilo halikuweza kupeana kwa mwanamke katika pande nyengine, bali wanawake wana majukumu mbalimbali katika kundi hilo miongoni mwa majukumu yao ni  wanaharakati wa mtandao ili kuwavutia wanamgambo na kulinda mali, na pia wana majukumu ya kijeshi ambapo wanafuatiliaji na uhamisho wa taarifa na wa silaha na ukaguzi kwa wanawake na usimamizi wa wafungwa wa kike.
Na kundi hilo lina vikosi viwili vya kike, vinaitwa "Al-Khansaa" na "Om Al-Rayan" lakini hakuna idadi wazi kwa vikosi hivyo…
Kwa hivyo uhusiano wa Daesh pamoja na mwanamke ni utata, na uhusiano huo umekataliwa na Uislamu kwani sio halali na hauna sambamba na utu wa mwanamke kama Mungu alitaka.   

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.