Falsafa ya adhabu ya mipaka katika Uislamu

  • | Friday, 7 August, 2015
Falsafa ya adhabu ya mipaka katika Uislamu

Mipaka katika Uislamu imepitishwa kama adhabu zilizotajwa katika matini na zilizoainishwa na Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuhifadhi mahitaji ya kimsingi ya mtu ambayo maisha na kuwepo kwake yanayategemea, kama vile nafsi, nasaba, mali na akili, nazo zinazingatiwa kutokana na sheria ya kiislamu mambo makuu ambayo maisha ya mtu hayasimami ila kwa mambo hayo, Mwenyezi Mungu amesema: " Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba " ( Al-Israa- Aya 70 )
Kwa mujibu wa haki ya watu inazaliwa haki ya  urekebisho  na ulinzi, na kutokana na kanuni hii, Mwenyezi Mungu amepitisha mipaka ili kulinda mtu huyu katika mambo yake makuu ambayo yakikamilika na yakiambatanika mtu huyo atakuwa na umbo lilio bora kabisa.
Kutokana na hiyo ukiuaji wa nafsi unazingatiwa uharibifu kwa kujenga kwa mwanadamu uliofanywa na Mwenyezi Mungu na maangamizi ya kuwepo kwake, ikabidi kupitisha uadilifu kupitita kulipiza kisasi ili wanadamu wote wawe sawa katika haki ya kuwepo na kuwa na uhai.
Pia upotevu wa nasabu kwa sababu uzinzi inazalisha kizazi muokotaji kisicho na nasabu maalumu, jambo ambalo linazidisha suala la watu ambao hawana nasabu maalumu katika jamii za kibinadamu, suala hilo linaathiria vibaya kibinadamu na kijamii, licha ya gonjwa zinazoambukiza zinazozalishwa na kjamiana zaidi ya mwanamume mmoja na mke mmoja kwa njia ya uzinzi, basi ukali katika adhabu ya uzinzi kwa ajili ya marudi na kulinda nafsi na jamii na siyo kwa kisasi.
Adhabu katika uislamu ilikuwa njia na siyo lengo.
Ama kuharibu mali kwa kuziiba, au kuzipokonya au kuzipora, basi ni aina ya ukiuaji na uharibifu wa mali.
Basi aliyepora haki ya mtu katika mali ambayo anaitumia katika maisha yake, na anaitegemea katika kubaki maishani, basi ameharibu maisha yake, ameharibi njia ya ukaaji wake, basi adhabu katika mali ilikuwa kwa ajili ya kuzuia watu wa kurefuka na dhuluma na kushutumu kwa wanaofanya uharibifu katika ardhi.
Kwa hiyo adhabu yenye mpaka katika sheria ya kiislamu si lengo bali ni njia kwa kulinda mali na ubinadamu.
Dalili ya kuwa njia na siyo lengo kwamba mipaka katika Uislamu inabatili kwa kuwepo tuhuma katika kuithibitisha kwa kauli yake Mtume (S.A.W.) "Mjieupusheni kuwapitishia waislamu adhabu zenye mipaka mnavyoweza basi (mshtakiwa) akiwa na sababu (hoja au dalili) ya kutoadhibiwa basi mwachilieni na imamu akikosea kusamehe (mhalifu) ni bora zaidi kukosea kupitisha adhabu (asiye na hatia)".
Hadithi imeashiria kuwa sheria ya kiislamu inafanya tuhuma njia ya kubana katika kupitisha adhabu ya mpaka, nayo ni adhabu inayojulikana na jina la mipaka (Huduud) licha ya kubana kuithibitisha.
Masharti magumu zilizowekwa na sheria ya kiislamu ili kuthibitisha hatia aghalabu ni ngumu kutekeleza mipaka kwa sababu ya ugumu wa masharti hayo, basi kwa kadri ya ukali wa adhabu – kama wanavyodai baadhi ya watu - kwa kadri ya ulali katika kuithibitisha, masharti ya kuitekeleza, hata kwamba sheria ya kiislamu imemrhusia mshtakiwa kukana ukiri wake bada ya kuupitisha kwa kutoroka adhabu, katika mpaka kati ya mipaka mikali kama vile uzinzi, sheria imefanya sharti ya kutekeleza adhabu hiyo kuambatana kwa watu wanne kuwa wao wote wameangalia na wameona hali ya uzinzi, na hiyo ni ngumu sana kwa sababu usiri na kuficha wakati wa kufanya tukio hilo.
Mtu mmoja tu miongoni mwa wanne hawa akitofautiana na watatu wenigine katika usifu wa tukio, basi shahada inabatili, na adhabu inafutwa, na watu wengine walioshuhudi watapata adhabu, na hiyo ni daraja juu zaidi ya kumlinda mhalifu wakati wa kutekeleza mipaka ya kisheria.
Aidha miongoni mwa dhamana ya kutekeleza adhabu kwa mujibu wa masharti ya kisheria ni kwamba jukumu la kuthibitisha uhalifu na kutekeleza adhabu inahusiana na utawala wa nchi ikiwa kwa kutoa hukumu au utekelezaji, na hii ni dhamana kubwa zaidi kwa uadilifu katika kutekeleza.
Mmoja wa watu wala makundi hawana haki ya kuthibitisha au kutekeleza adhabu bila ya kurejea kwa utawala wa nchi, na kama wakifanya hivyo basi watakuwa wamevunja mipaka ya utawala wa nchi, jambo linalowajibika kuwaadhabisha na kuwafanyia vikwazo kwa mujibu wa utawala wa ujaji.
Kwa hiyo imethibitishwa yakini kwa dalili kwamba sheria ya kiislamu haina hatia yo yote kutokana na kila kinachomaanisha kuwepo tuhuma ya jeuri na ukatili katika hukumu zake.

Print
Tags:
Rate this article:
2.0

Please login or register to post comments.