Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu kwenye Chuo kikuu cha kiislamu cha kiserikali cha Maulana Malik Ibrahim nchini Indonisia

  • | Thursday, 25 February, 2016
Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu  kwenye Chuo kikuu cha kiislamu cha kiserikali cha Maulana Malik Ibrahim nchini Indonisia

 

Dondoo za hotuba ya Imamu Mkuu

kwenye Chuo kikuu cha kiislamu cha kiserikali cha Maulana Malik Ibrahim nchini Indonisia

Katika sherehe kubwa ya kirasmi na ya kitaifa

  • Indonisia imtunza Mheshimiwa Imamu Mkuu shahada ya uzamifu wa sharafu...

Naye asisitiza kwamba:

  • Ujumbe wa Al-Azhar ni kushikamana na mfumo wa madhehebu ya kisunna na Jamaa kwa kuzingatia matawi yake yote

 

Kwa uzingatio na ukaribisho rasmi na wa kitaifa mkubwa….Chuo kikuu cha kiislamu cha kiserikali cha Maulana Malik Ibrahim nchini Indonisia kimemtunuka Mheshimiwa Imamu Mkuu Profesa; Ahmad Al-Tayib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar na mkuu wa baraza la wakuu wa waislamu shahada ya uzamifu wa sharafu, katika sherehe kubwa iliyofanyiwa kwenye makao makuu ya chuo kikuu hicho mjini Malang mkoani Gawa wa mashariki.

Sherehe hiyo imehudhuriwa na wakuu wa vitivo na maprofesa na wanafunzi wa kiandonisia, wakati ambapo mamia ya watu wamesimama barabarani kwa ajili ya kumkaribisha na kumwadhimisha Mheshimiwa Imamu Mkuu.

Na katika hotuba yake aliyoitoa katika sherehe hiyo Mheshimiwa Imamu Mkuu amesisitiza kwamba elimu na maarifa ni kiokozi cha umma kutoka upotofu na utangaji, akibainisha kwamba ujumbe wa  Al-Azhar Al-Shareif ni kushikamana na mfumo wa madhehebu ya Sunna na Jama'ah pamoja na kuzingatia matawi yake yote, vile vile amebainisha kwamba ufundishaji ni ujumbe na uhai, na maulamaa inawatosha sharafu ya kutekeleza jukumu la Manabii.

Yule mheshimiwa aliashiria kwamba Al-Azhar Al-Shareif inalazimika kwa jukumu la pande mbili za ujumbe wa Uislamu kisayansi na ulinginiaji, ambapo hotuba ya Al-Azhar inasifika kwa uwastani katika itikadi ambapo iambatane na wafuasi wa Salaf wanaojiweka mbali na kufanana na mitengo ya tafsiri, akiongeza kuwa Al-Azhar Al-Shareif inafuata katika uelewaji wa ujumbe wa Uislamu na kuufundisha na kuulingania mfumo wa Ahlu-Sunnah na Al-Jama'ah, ambapo sifa inayopambanua mfumo wa Al-Azhar ni uchambuzi wa kimatini na wa yakini kwa mafundisho ya kale, akibainisha pia kwamba hotuba ya Al-Azhar ya kiwastani inakukubalika ndani ya ulimwengu wa kiislamu na nje yake kwani hotuba hiyo huchanganya baina ya fikira za kisayansi na Roho ya kisufi katika hali ya uwastani na usawa.

Na kuhusu utoto wake, Mheshimiwa Imamu Mkuu Amesema: nilipata malezi katika mazingira ya kiarabu na ya kiroho katika nyumba ya elimu na dini, chini ya ulezi wa baba mzuri sana amenipa mambo mazuri mengi sana, akielezea furaha yake kwa sherehe hiyo ambayo na sawa na kutunuka kwa undugu baina ya Misri nchi ya Al-Azhar na Chuo kikuu cha Maulana Malik Ibrahim cha kiislamu na cha kiserikali nchini Indonisia.

Na mwishoni mwa hotuba yake, Imamu Mkuu amesisitiza kufurahika kwa Al-Azhar na Chuo kikuu hicho, akieleza kwamba Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kusaidia Chuo kikuu hicho kwa kukiagiza maprofesa na wanavyuoni.

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.