Dhana ya Hijabu na Masharti yake ya kisheria

  • | Friday, 7 August, 2015
Dhana ya Hijabu na Masharti yake ya kisheria

Kwa hakika Uislamu umezigatia mavazi ni kiwakilishi cha maadili, tabia nzuri ambazo jamii ya kiislamu inaziamini, na kwamba Mwenyezi Mungu ametupa neema kubwa sisi  wana wa Adam (Banu Adam) kwa mavazi yanayofunika miili yetu, ukatuombea tujumuishe baina ya mavazi ya kumcha Mungu, imani, stara, ustahivu, twahara na mavazi ya nje yanayofunika miili yetu ili tuwe picha halisi ya heshima ambayo tumepewa na Mwenyezi Mungu.
Uharamisho wa ufasiki wa mwanamke na kuonyesha fitina za mwili wake – na kufananisha jambo hilo na ufasiki wa Jahiliya ya kwanza (zama za Jahili kabla ya ujio wa Uislamu) – ili kuimarisha tabia njema ambayo Uislamu ulikuja ili kuzitimiza na ili kziba nafasi za kujitokeza ufisadi ambao unasababishwa na ufasiki huo, na kwa ajili ya kuhakiksha lengo lake la kimsingi ambalo ni kusimamisha maisha safi ya kijamii ambapo tabia njema na matukio mema yatakua katika maisha hiyo.
Kwa hiyo Uislamu ulizingatia sana mavazi ya mwanamke na umbo lake ukamlazimisha avae mavazi yasiyo na utongozaji (ujanja) na fitina yakionyesha heshima na stara inayolengwa na Uislamu, lakini Uislamu wakati huo huo hauzingatia mavazi ya nje ukiacha yaliyo ndani (mambo yanayofichika kwa kila mwanadamu), vile vile hautilia mkazo mavazi ya kutoka nje ya nyumbani na ukamnyima mwanamke haki yake kuonyesha valio zuri yake mbele ya mume wake ndani ya nyumba yake hapana, kwa kweli Uislamu mwanzoni unazingatia kuthibitisha imani na ibada katika nafsi na nyoyoni, na hiyo iliyokusudiwa na Qurani Takatifu katika kauli yake: { Na nguo za uchamngu ndio bora } Al-Araf: 26. Kisha unamruhusu kupata anasa ya ndoa ambapo anaweza kuonyesha valio yake kwa mume wake apendavyo pasipo na matatizo yo yote wala vizuizi lakini akitoka uwanja wa nyumbani na maharimu wake ukamwombea atoke na heshima na stara.

Masharti ya Hijabu:
-    Mavazi yafunike mwili wote.
-    Yawe mapana sio tarakiki yaliyobanwa mwilini.
-    Yasibainishe yaliyo chini (yasiwe uraka).
Dalili ya hayo ni kauli ya Mwenyezi Mungu: { Na waambie Waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasionyeshe uzuri wao isipokuwa unao dhihirika. Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao, wala wasionyeshe uzuri wao ila kwawaume zao, au baba zao, au baba wa waume zao, auwatoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, auwana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawakewenzao, au iliyo wamiliki mikono yao ya kuume, auwafwasi wanaume wasio na matamanio, au watoto ambaohawajajua mambo yaliyo khusu uke. Wala wasipige chinimiguu yao ili yajuulikane mapambo waliyo yaficha. Natubuni nyote kwa Mwenyezi Mungu, enyi Waumini, ilimpate kufanikiwa.} An-Nour: 31.
Aya imebainisha mwanzoni mwake mambo mawili makuu ambayo inapaswa kuyahifadhi nayo ni: la kwanza: kuinamisha macho maana nafsi na moyo pia, la pili: kuhifadhi tupu, na Uislamu unaamini kinga na unazingatia kuzuia sababu za fitina na kuzuia ufisadi, vile vile aya imekataza kuonyesha valio kwa kuwa jambo hilo linaweza kusababisha utongozaji ili kumtazamia yule mwanamke aliyeonyesha valio yake na kuombea kutanabahi.
Mwenyezi Mungu amesema: {Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao } An-Nour: 31.

Shungi: ni wingi wa shungi nayo ni ile inayofunika kichwa. Na vifua (mifuko): ni wingi wa kifua (mfuko) nayo ni mahali palipokataliwa kutoka mkono na shati, na imetokana na Jawb nayo ni kukata basi Mwenyezi Mungu akaagiza kuangusha shungi juu ya shingo na kifua ikaashiria hiyo ulazimisho wa kuzifunika, na sifa ya hiyo ni mwanamke aangushe shungi yake juu ya kifua chake ili kufunika kifua, Bukhari amesimulia kutokana na Bibi Aisha (R.A) amesema: "Mwenyezi Mungu awarehemu wanawake wa Muhajirat wa kwanza, ilipoteremshwa aya ya: { Na waangushe shungi zao juu ya vifua vyao } wakakata kitambaa cha kufunika migongo yao wakaviangusha juu ya vifua vyao" .  

 


    Tafsiri ya Qurtoby: juzuu ya 12, ukurasa wa 230.

 

Print
Tags:
Rate this article:
4.6

Please login or register to post comments.