Uislamu umetekwa nyara na IS {kundi la Daesh}

Gazeti la Al-Jumhuriya chini ya anuani:

  • | Monday, 15 June, 2015

 

 

Kundi la waandishi wa habari wa Itali wamemwuliza Mheshimiwa Imamu mkuu baadhi ya maswali:

*Katika wakati wa sasa ulimwengu umeathiriwa na vita kali, ambapo kuna kundi ambalo jina lake lenyewe linalibeba taifa la kiislamu, ili kusaidia katika kufsiri kiini cha dini yenu ya kiislamu ambacho ni karibu zaidi na kweli,vipi utajibu mheshimiwa mkuu?

Bila shaka, mimi sikubali uwasifu wa nchi ya kiislamu: makundi haya yenye silaha yako nje ya Uislamu, na yanazingatiwa kikwazo kikubwa kwa fikra zote za kiislamu.

Sisi katika Al-Azhar ni taasisi ya kielimu: tunataka kuwaunga mkono vijana si kupitia kuwapa silaha lakini kupitia kusoma gazeti la Uislamu (mafunzo ya kiislamu)

*Kivutio kwa lengo la kushindana baina ya dini na siasa katika ulimwengu wa kiislamu ni moja ya sababu zinazochangia kuchnaganya.

Ewe, mheshimiwa mkuu je, unafikiri kwamba itawezekana kutenga baina yao?  

'Tayari kuna njia mbili tofauti. Katika uwanja wa siasa mara nyingi maslaha inaainisha maamuzi, lakini kuhusu dini tabia haiwezekani kuachwa.

Tukizungumzia siasa ya juu, ambayo tunaitaka kufikia uadilifu na kuwalinda maskini – wanyonge - hapa tunasema ndiyo, dini inavamia uwanja wa siasa na pia inaingia ili kuunga mkono maamuzi ya kisiasa kwa kuzingatia maadili kuu yenye msamaha.

*Nchi ya Uturuki ni mfano wa kushindana kati ya dini na siasa. Je, unafikiri nini kuhusu matokeo ya uchaguzi? Una maoni gani kuhusu matokeo ya uchaguzi?

Mimi sijui nitajibuje kwa kweli mimi sishughulii kwa siasa, hivyo siwezi kutoa jibu' lakini linalosisitizwa ni kwamba inayoonekana leo ni lazima kuichunguza katika mfumo wa msimamo mmoja wa mashariki na magharibi ambapo inaonekana kwamba kuna aina ya mkutano wenye mvutano baina ya ustarabu wa magharibi na ustarabu wa mashariki.

'Mahusiano na kanisa la Papa Franshesko yanaendelea vipi?

Papa Franshesko ni mtu anaye heshima moyoni mwake kwa dini nyingine na matatizo ya masikini. Na kuna makubaliano kamili na maafikiano  baina ya malengo ya Al-Azhar na mwelekeo mpya wa kanisa . 

 

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.