Al-Azhar Na Kupambana Na Mawazo Makali Afrika

  • | Wednesday, 3 July, 2019
Al-Azhar Na Kupambana Na Mawazo Makali Afrika

     Katika wakati ambapo nchi kubwa na mashirika ya kimataifa hazikuwepo na mgogoro wa Afrika, na matukio ya vurugu yaliyongozeka hayakuathirika nao, Al-Azhar Al-Sharief haikusimama bila ya kufanya kitu chochote mbele ya hali hii mbaya, lakini imefanya jaribio la kusaidia la kupambana na makundi ya kigaidi ambayo yanatishia usalama na amani ya wananchi.

Kwa mfano nchini Nigeria, kundi la “Boko Haram” limekuwa na hatari kubwa na limeongezeka wafuasi wake, mpaka likawa kundi chenye umwagaji damu zaidi duniani kuliko kundi la Daesh; kundi hilo lililoshughulisha jumuiya ya kimataifa kufuata habari zake na kuunda muungano ili kupigana na kufanya mashambulizi mbalimbali ya kijeshi kwa lengo la kuiondoa katika vita kali ambavyo vimesababishia kufa maelfu ya watu wasiokuwa na hatia na mamilioni ya watu waliokimbia makazi yao. Hatari ya kundi la Boko Haram kwa usalama imezidi kwa njia kubwa katika eneo lote la Magharibi ya Afrika, sio tu Nigeria.

Na katikati ya matukio hayo yanayofuata na mfululizo wa kigaidi, Al-Azhar, inasimama mbele ya makundi hayo ya kigaidi, ambapo iliingia katika kupambana fikra ya makundi hayo, vita vimekuwa na Al-Azhar Al-Sharif kupitia kituo chake kwa kupambana na fikra kali, ambapo kilichukua juu yake chenyewe jukumu la kuchunguza na kukanusha madai ya Boko Haram na kujibu kile kilichotolewa na wafuasi wake kutoka tuhuma za uongo na madai ya batili, na baadaye kutoa nasaha yenye faida kubwa na ufahamu muhimu kwa ajili ya vijana ambao kundi hilo linawalenga ili kuwajiunga safu yake, kwa njia hiyo walikuwa wamezidi mapato yao; nao kuwapotea vijana, na kuwatumia shauku yao kwa ajili ya kuwakinaisha na mawazo yao ya kikali na kufikia malengo mabaya, hayana uhusiana wowote wa kusimamisha kwa dini au kutumia kwa sheria, na wakati wa vita hivi kali, Kituo cha Al-Azhar kimefanya mfululizo wa taarifa ili kugundua batili ya kundi hilo na kubainisha uhakika wake, na kufafanua Uislamu katika picha yake ya usamehevu na misingi yake ambayo inatoa wito kuhifadi mwanadamu na heshima yake, sio kama wanafanya watu wenye msimamo mkali kupunguza heshima ya mwanadamu.

Jambo lenyewe limetukia kuhusu kundi la Al-Shabab la Somalia, ambalo limekuwepo kwa kiasi kikubwa katika nchi za Afrika ya Mashariki na eneo la Pembe ya Afrika, ambapo Al-Azhar na kituo chake havitengana na matukio, lakini vilikuwa katika tukio lenyewe, husaidia walioathirika na huwafariji walioteswa na kuwafahamisha vijana ambao wanalengwa na kundi hili, hasa huko Kenya na Somalia, kwa hatari zinazofika kwao wanapojiunga kundi hilo, na hiyo kwa kupitia kubainisaha makosa na upotovu wa kundi hilo na kueleza msimamo wa Uislamu kuhusu kundi hilo na uhalifu wake katika zaidi ya tukio moja na zaidi ya makala na repoti, na kwa hakika Al-Azhar kupitia kituo chake inaendelea katika kuchunguza madai ya kundi la Al-Shabab na kulinda akili za vijana kutoka mawazo mabaya yanayoenezwa na kundi hilo kwa lengo la kupotosha vijana na kuwajiunga kwao chini ya visingizio cha kusimamisha sheria na hukumu kwa mujibu wa aliyoteremsha Mwenyezi Mungu.

Na kituo cha Al-Azhar kwa kupambana mawazo makali kinaendelea kufuatilia matukio yote yanayofanya katika mashariki na magharibi mwa bara, kwa ajili ya kufuatilia, kuchambua, kukataa, na kujibu juu ya shubha hizo, na ili pia Al Azhar daima ipo katikati ya matukio, pamoja na watu wa bara la Afrika, ikiwaunga mkono kwa hoja nguvu na kuwasaidia kwa uongozi bora na kuwapa ulinzi muhimu kutokana na mawazo mabaya.

Hakika mtazamaji kwa historia ya Al-Azhar haihisi vigumu au taabu katika kutambua michango ya taasisi kubwa hiyo na athari yake nzuri ndani na nje ya Misri; ambapo Al-Azhar imejalia kwa kuinua thamani ya ubinadamu na kueneza utamaduni wa amani na ushirikiano duniani kote. Na kwa sababu zote hizo tunaweza kusema bila ya upendeleo kwamba Al-Azhar – kwa kweli – ni mojawapo ya taasisi kubwa duniani ambazo zinajaribu kwa njia kubwa kuokoa ubinadamu kutoka ulimwengu ambao umejazwa kwa vurugu na ugaidi, pamoja na mazoea ya chuki na ubaguzi na yote yanayopigana na misingi ya kibinadamu, hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.

 

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.