Uislamu huheshimu haki za wasio waislamu wanaoishi chini ya utawala wa waislamu

  • | Thursday, 19 December, 2019
Uislamu huheshimu haki za wasio waislamu wanaoishi chini ya utawala wa waislamu

     Mwenyezi Mungu (S.W.) amemwumba mwanadamu akampa maumbile yaliyo mazuri zaidi na akamtukuza akampa neema zilizo dhahiri na zilizofichika, akaufanya ulimwengu kwa viumbe vyote vilivyomo ndani yake kati ya neema za mbinguni na ardhini vimsaidie mwanadamu yule pasipo na kutofautisha baina ya mwamini na mkafiri katika hayo, ambapo neema za Mwenyezi Mungu ni za kijumla kwa wanadamu wote bila ya kujali dini zao, na hali hii ni rehema kutoka Mwenyezi Mungu na utukuzaji wa waja wake.

Vile vile, miongoni mwa mambo yaliyopitishwa na Mwenyezi Mungu ulimwenguni mwake kutofautiana kwa imani na dini baina ya watu, jambo lisilotukia ila kwa matakwa ya Mwenyezi Mungu na uwezo wake ulimwenguni mwake, ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu akitaka kuwafanya watu wote wawe ummah mmoja atafanya hivyo, kama alivyosema (S.W.): {Yeye ndiye aliye kuumbeni. Miongoni mwenu yupo aliye kafiri, na yupo aliye Muumini. Na Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda} (Attaghabun: 2), na neno lake Mtukufu: {Angeli taka Mola wako Mlezi wangeli amini wote waliomo katika ardhi. Je, wewe utawalazimisha watu kwa nguvu mpaka wawe Waumini?} (Younus: 99).

Mwenyezi Mungu (S.W.) amebainisha ukweli na yaliyo sahihi katika kitabu chake kitakatifu, akampa mwanadamu uhuru wa kuchagua baina ya kuwa mwamini au mkafiri, ambapo kila mwanadamu atahesabiwa na kulipizwa katika siku ya Kiyama kulingana na uchaguo wake, na Mwenyezi Mungu (S.W.) atapitisha hukumu baina ya wanadamu siku hiyo, akampa mfanyaji mema thawabu na kumwadhibisha mfanyaji maovu, na kupambanua baina ya wafuasi wa dini tofauti akadhihirisha mkweli na mkosa, Mwenyezi Mungu Mtukufu amesema: {Hakika walio amini, na ambao ni Mayahudi na Wasabai na Wakristo na Majusi na wale walio shiriki -hakika Mwenyezi Mungu atawapambanua baina yao Siku ya Kiyama. Hakika Mwenyezi Mungu ni Shahidi wa kila kitu} (Al-Hajj: 17).

Kutokana na misingi hiyo iliyowekwa na Uislamu, Mwenyezi Mungu amewatukuza wanadamu bila ya kujali itikadi au imani zao, akawapa haki zao kamili, kama vile haki ya kufanya ibada, kuishi, kuwa na uhuru na usawa, hata wakiwa ni miongoni mwa wageni walio wachache wasio waislamu wanaoishi katika nchi za kiislamu, kwa hiyo Uislamu ulihifadhi haki zote kwa watu hao, ukatangulia nchi zote za ulimwenguni ulipozifaradhisha haki zao tangu karne kumi na nne zipitazo.

Ambapo ukawapa haki zao za kufanya ibada, kujenga majumba ya kufanya ibada zao na kuwa na madaraka ya kisiasa, ukaharamisha aina zote za kuziangamiza nafsi za wasio waislamu au kuvunja heshima yao na mali zao, madamu hawakumwudhi au kudhulumu mwislamu ye yote, kwa mujibu wa kauli yake (S.W.): {Mwenyezi Mungu hakukatazini kuwafanyia wema na uadilifu wale ambao hawakukupigeni vita, wala hawakukutoeni makwenu. Hakika Mwenyezi Mungu huwapenda wafanyao uadilifu}(Al-Mumtahinah: 8), na hadithi ya Mtume (S.A.W.) isemayo: "Ye yote atakayemwua (asiye mwislamu ambaye) mwenye ahadi hatasikia harufu ya peponi, na kwa hakika harufu ya peponi husikika kutoka umbali wa miaka arobaini". Imesimuliwa na Ibnu Majah kutoka hadithi ya Abdullah Bin Umar.

Basi haikubaliki kuushutumu Uislamu kwa kuwadharau wageni walio wachache wasio waislamu, na vipi huwadharau wakati ambapo Mwenyezi Mungu (S.W.) amewaumba, akawatuzuku, akawapa neema na ukarimu, huruma kwa ubinadamu wao japokuwa kutofautiana kwa itikadi na imani zao, na historia ya kiislamu ni dalili lililo wazi zaidi ili kuthibitisha kwamba waislamu huwaheshimu haki zote za wageni walio wachache wasio waislamu wanaoishi pamoja nao jamii moja, ambapo wachache hao wameweza kufanya ibada zao wakajenga majengo ya kutekeleza ibada zao katika nchi za kiislamu pasipo na ulazimisho au vitisho.

Jambo hilo ni jambo la kawaida hasa baada ya Mtume (S.A.W.) amesimama kwa jeneza ya maiti mmoja wa kiyahudi ilipompitia kwa ajili ya kueleza heshima yake kwa nafsi ya kibinadamu bila ya kujali imani yake, akitoa mfano mzuri wa kuigizwa wa kuiheshimu nafsi ya kibinadamu na kuufundisha ulimwengu wote haki za wageni walio wachache, kwa kweli dini hii ni dini iliyo nzuri kabisa!!

Naye Al-Farouk Umar ambaye amewafundisha wanadamu wote kuheshimu haki za wageni walio wachache alipokataa kusali ndani ya kanisa moja ilipofika wakati wa swala, ili kuwazuia watu wasiigeuza kanisa hiyo iwe msikiti baada yake kusali ndani yake kwa dai la kusema kwamba hapo ndipo alisali Umar, je kuna dalili ya kuziheshimu ibada za wasio waislamu lilio wazi zaidi ya hilo?, tunatmai kuwa wasio waislamu wafahamu vyema mifano mizuri hiyo katika historia ya kiislamu ili wasikie raha na wasiwe na woga chini ya utawala wa waislamu.

Na kwa upande wake Kituo cha Uangalizi cha Al-azhar kwa kupambana na siasa kali inasisitiza umuhimu wa kufanya kazi kwa ushirikiano wa dini zote, ili kudumisha amani na usalama wa kijamii na kufikia masilahi ya pamoja katika huduma ya wanadamu wote.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.