Ugaidi wa kielektroniki (ugaidi wa cyber) na ulazima wa kusisitiza usalama wake

  • | Sunday, 12 January, 2020
Ugaidi wa kielektroniki (ugaidi wa cyber) na ulazima wa kusisitiza usalama wake

     Hatari ya kutumia vyombo vya habari vya kielektroniki kama ni zana ya kueneza fikra kali iko katika kutegemea vyanzo vya habari na njia za kielektroniki katika wakati huo huo kw ajili ya kushawishi akili za wanaopokea, kwani mifumo ya kielektroniki na miundo mbinu ya habari ni moja wapo ya njia muhimu kwa magaidi.

Wakati ISIS ilipotawala mji wa Mawsil mnamo Juni 2014, halikutosha kwa kuchukua maeneo tu, lakini liliasisi kampeni ya vyombo vya habari kwenye “Twitter” kupitia kutoa hashtag #AllEyesonISIS), inayomaanisha “macho yote yanaangalia Daesh” na katika masaa machache, picha zinazoonyesha ukatili wa kundi hilo zilieneza ulimwenguni wote ili kuimarisha hofu ndani ya mioyo.

Kutokana na hayo, vikosi vya jeshi la Iraq huko Mawsil, vilivyokuwa zaidi ya wapiganaji wa ISIS kwa mara tano vilijitenga na kukimbia, kwa hivyo zaidi ya wapiganaji 2000 wa Daesh waliudhibiti mjia wa Mawsil, ambao idadi ya wakazi wake wanafika milioni 1,5. Na hii inazingatiwa njia isiyo ya moja kwa moja katika jambo la kuwavutia ISIS kwa vijana na njia ya kueneza mawazo ya uwongo yenye kupotosha na kueneza vumi kwa lengo la kudhibiti maeneo mengi na kuwavutia vijana zaidi.

Na “ugaidi wa kielektroniki” unahitilafiana –kwa masikitiko- na aina nyingine za ugaidi kuhusu kasi yake (haraka yake), kufichwa kwake, na kuvuka kwake kwa nchi na mabara, kwani hakuna kundi lolote la kigaidi linaweza kutekeleza vitendo vyake vya kigaidi bila ya kutumia intaneti. Aidha, mashambulizi ya kielektroniki (ugaidi wa cyber) yanayokabili kwa mitandao mingi ya kiserikali na ya kibinafsi, yanatakia kuimarisha juhudi za usalama wa kielektroniki katika njia zote za kiteknolojia ulimwenguni wote, hasa baada ya kudhihiri makundi ya kigaidi, na vitisho vyake kwa kutekeleza mashambulizi ya kielektroniki.

Nchi za ulimwenguni zimeteseka na bado zinaendelea kuteseka kuhusu matumizi ya kimfumo kwa makundi ya kigaidi kwa intaneti, ambapo wenye fikra kali waliweza kupitia kawake kushawishi (kuathirika) makundi mengi ya vijana ulimwenguni kote kupitia njia tofauti, kila kundi kwa mujibu wa hali yake ya kijiografia, kijamii na kwa mujibu wa tofauti hali ya kisaikolojia na ya kifikra kwa sehemu iliyo kubwa ya vijana.

Na mistari zifuatazo zinaonyesha namna ya athiri za intaneti kwa vijana na vipi imeweza kuwavuta na kuwa wanamgambo katika nchi kupitia mifano kwa baadhi ya nchi, miongoni mwake:

Kuhusu Uhispania

Licha ya kutokuwepo vyombo vya habari vinavyotamka kwa lugha ya Uhispania vinavyofuata kwa makundi ya kigaidi isipokuwa baadhi ya mitandao yanayosambaza katika baadhi ya wakati kwa ujumbe ulioandikwa au picha kwa lugha ya kiarabu au kingereza yanayoambatana na ufasiri kwa lugha ya Uhispania , au vitisho wazi kwa lugha ya Uhispania kupitia mmoja wa wapiganaji wake wa kihispania, lakini kundi la Daesh limeweza kuwavuta wengi wa vijana katika Uhispania katika miaka ya hivi karibuni, na mazoezi ya kuwavuta bado yanaendelea kupitia njia tofauti za mawasiliano ya kijamii kupitia akaunti za kibinafsi, au kupitia programu ya Whats App na Telegram. Pia zoezi la kuwavuta lilikuwa kutumia kupitia makundi ya wanamgambo wanaojificha yaliyokuwa yanakamatwa na serikali, wanamgambo hao waliweza kusaidia makundi ya kigaidi kwa mali na kwa kuwatuma wapiganaji mapya katika maeneo ya mgogoro huko Syria na Iraq.

Na kwa mujibu wa baadhi ya ripoti zinazohusiana na suala la vyombo vya habari vya makundi ya kigaidi, basi lugha ya Uhispania inakuwepo katika namba ya kumi na tatu kati ya lugha zinazotumika na makundi kwa ajili ya kueneza fikra na mikakati yake.

Kuhusu Afrika

Makundi ya kigaidi barani Afrika kama kundi la “AL-Shabab” nchini Somalia, na kundi la “Boko Haram” nchini Nigeria, na kundi la “Nusrat Al-Islaam wa Al Muslimiin” nchini Mali, na makundi mengine ya kigaidi yameelekea kutumia vyombo vya habari katika kueneza malengo yake na kuvitumia katika kudanganyifu Idara za usalama, na kueneza habari za mashambulizi ya kigaidi wanayoyatekeleza, pia makundi hayo yalielekea kufuata mkakati wa “udanganyifu wa kihabari” unaotegemea kuharibu maelezo na kuyatoa kwa mpokeaji kwa njia ya ubaya, na labda jambo linafika kwa kusema uongo kwa mpokeaji, maana  kuunda maoni fulani kuhusu ukweli maalumu kwa ajili ya huhudumu maslahi ya makundi hayo na kuhakikisha malengo yake. Hiyo ni mbali na vita ya kisaikolojia vinavyoendeshwa na makundi hayo kwa ajili ya kushawishi wapinzani wake , na hayo ilidhihirika kwa njia wazi katika baadhi ya machapisho yanayosambazwa na vyombo vyake vya habari na mitandao yanayoyafuata.

Inakumbuka kwamba kuna mitandao mengi yaliyofunguliwa baada ya kueneza fikra kali. Na kwa upande mwingine, makundi ya kigaidi yalitoa wafuasi wake dhidi ya mitandao yanayoyapinga na yamefaulu katika kufunga ukurasa wa Facebook unaofuata sehemu ya lugha za kiafrika kwa lugha ya kiswahili katika kituo cha uangalizi cha Al-Azhar ili kuzima sauti hiyo iliyokuwa inayoyafichua na kubainisha madai yao batili na itikadi yao potovu, lakini kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kimeweza kuurejea ukurasa huo na kuendela kazi yake tena.

Kuhusu Uingereza

Tangu mwaka wa 2015 na baada ya kundi la kigaidi la Daesh limetekeleza mashambulizi mengi ya kigaidi, usimamizi wa “Facebook”, “Twitter”, “Youtube” umefuta kitu (data) chochote kinachohusiana na kundi la kigaidi na kuweka vizuizi kuhusu kusambaza kitu maalumu kinachohusiana na makundi kama hayo; kwa hivyo kundi limeelekea kutumia baadhi ya mitandao ya mawasiliano ya badala ya kijamii yatakayomwezesha kusambaza yanayotaka bila ya kuweza serikali kufuata hayo, na miongoni mwa mitandao hayo ni programu ya “Telegram”, “Justpaste.it”, “Surespot”, na “TikTok”, pia kundi limeelekea kwa kutumia njia ya Hashtag, na ambayo inaruhusu kwa wanamgambo wake na wanaolipenda kwa kufuata habari za kundi moja kwa moja kila wiki kwa kutumia maneno ya utafiti kama                 #Khilafa News the Friday of Supporting ISIS #Calamity Will Befall the US#. Pia kundi lilielekea mwishoni kwa kutumia inayojulikana kama "Deep Web", ambayo inazingatiwa moja wapo ya teknolojia isiyoweza kufuatwa kwa mchapishaji na msomaji.

Jukumu la serikali katika kupambana na ugaidi wa cyber

Hakika serikali nyingi ulimwenguni zimetanabahi kwa hatari ya "fikra kali na ugaidi wa kielektroniki"; kwa hiyo zimefanya juhudi kubwa na bado kuendelea ili kupambana na makundi hayo ya kigaidi yanayoeneza fikra zake kupitia intaneti na hasa mitandao ya mawasiliano ya kijamii, hasa baada ya mashambulizi ya kigaidi yaliyotekelezwa ulimwenguni mwishoni, ambapo serikali na taasisi za kimataifaza  zimetafuta njia za ushirikiano wa daima, na uwezekano wa kuweka hatua mpya zinazolenga kulinda uhuru wa kutoa maoni pamoja na kuweka mipaka kwa kueneza maelezo ya kigaidi kupitia intaneti, kwa lengo la kufanya intaneti yenye amani zaidi kwa ajili ya kuepusha hatari za “ugaidi wa kielektroniki” na kupambana naye.

Kwa mfano, baada ya mashambulizi mawili yaliyotekelezwa dhidi ya misikiti miwili mjini wa “Crist Tchirsh” nchini “New Zealand” mwezi wa Machi 2019, Raisi wa Ufaransa “Imanuel Makron”, na waziri mkuu wa New Zealand “Gasinda Ardirin” pamoja na vingozi wa ulimwengu na wahusika wakuu wa taasisi za Teknolojia, walitoa kutoka Paris kampeni “Wito wa Crist Tchirsh” kwa ajili ya kupambana na suala la fikra kali kupitia intaneti.

Pia naibu wa kifaransa “Latitia Afiya” - mwanachama wa chama cha Jumhuri kwa mbele - ameunda Infografik pamoja na ripoti yake kuhusu kanuni aliyeitangulia kwa Bunge la Ufaransa, katika 3 mwezi wa Julai 2019, na kanuni hiyo ni miongoni mwa kanuni za kifaransa zinazolenga kupambana na “ugaidi wa kielektroniki”, na kujaalia taasisi kuu za intaneti kuweka adhabu kali na wazi dhidi ya watu wnaoeneza fikra kali kupitia intaneti.

Na katika Ujerumani, wizara ya mambo ya ndani inafanya hatua za marekebisho zinazohusiana na kupambana na ugaidi kupitia intaneti, ambapo ofisi ya kupambana na halifu imeimarishwa kwa watu wahusika katika suala hilo na kuanza kuiunda mara tena. Pia itaanza kuanzisha taasisi ya kitaifa kwa kupambana na halifu za uchuki kupitia intaneti na ambayo itafanya kwa kuangalia intaneti daima kwa kushirikiana na wanaotangulia huduma na njia ya mawasiliano ya kijamii kwa kuandikwa anuani ya “IP” inayohusiana na kila mtumiaji ndani ya wigo wa programu ya kuhifadhi maelezo, na ofisi hiyo itakuwa ofisi mkuu kwa kufuatilia halifu za intaneti inayofuata ofisi wa kupambana na halifu, na hiyo kwa kushirikiana na Polisi na ofisi mbili wa usalama wa kimataifa.

Pia mpango huo ndani ya wigo wa marekebisho yaliyopangwa, unafanya juu ya kulazimisha waendeshaji wa mitandao na njia za mawasiliano ya kijamii kwa kufikisha halifu za uchuki na uchochezi kupitia intaneti kwa taasisi ya kupambana na halifu badala ya kuzifuta kama ilivyokuwa kutokea hapo awali, na hatua hiyo inakuja katika mwelekeo sahihi kuhusu kuimarisha uwazi na ushirikiano kati ya watoaji wa huduma za mtandao na utawala wa usalama.

Na katika Pakistan, na katika wakati ambapo kuna watu wengi wanaoita kwa ulazima wa kuweka udhibiti na hata kupiga marufuku kila kinachochapishwa kwenye mitandao hiyo, pia kuna watu wengine wanaopinga suala hilo, na wanazingatiwa kwamba kila marufuku yoyote itakayofanywa kama ni kuzima kutoa maoni na uhuru wa kueleza. Ambapo mwandishi mmoja wa habari anaona kuwa ni nzuri kuchukua hatua dhidi kila mtu anayezungumza kwa chuki kwa ajili ya kupunguza kuenea kwa fikra kali ya kidini na ugaidi, lakini katika wakati huo huo haifai kutumia suala hilo kwa ajili ya kukandamiza wanaokosoa serikali.

Kulingana na yaliyosambazwa na baadhi ya magazeti, serikali ya “Umran Khan” ilitoa kampeni dhidi ya hotuba ya uchuki, na dhidi ya matumizi mbaya ya njia za mawasilano ya kijamii, na hiyo kwa ajili ya kuwazuia wengine kueneza fikra kali wa kidini na ugaidi, ambapo serikali ilitangaza kuunda kikundi cha wawakilishi kutoka FBI na vyombo vingine vya usalama kwa ajili ya kupanga mitandao ya mawasiliano ya kijamii, na kufanya kwa ajili ya kufuatilia mitandao hiyo na kuondosha akaunti bandia, na kushtakia kila anayekiuka kanuni zinazopanga kwa intaneti huko Pakistan.

Aidha kamati ya jumuia ya kitaifa ya Teknolojia ya maelezo na mawasiliano (The National Assembly Standing Committee on Information Technology and Telecommunication) iliambia kwa uwezekano wa kuzuia matumizi ya njia ya mawasiliano ya kijamii kama vile: Twitter, Facebook na YouTube katika ofisi za kiserikali wakati wa kazi ili kupunguza kutoa habari rasmi kwa watu.

Ama India, serikali yake ilitangaza katika Oktoba 2019, kupitia hati ya kisheria iliyoitangulia kwa Mahakama Kuu kwamba inaamua kutekeleza misingi ya kudhibiti njia ya mawasiliano ya kijamii; na hiyo kutokana na uwezekano wa kuidhuru hali ya kiujumla huko India, nayo inahitaji miezi mitatu kwa ajili ya kuweka misingi inayopanga kazi ya mitandao hiyo; kwa lengo la kupunguza kutoka kueneza habari bandia, vumi, na vitisho vinavyozidi dhidi ya haki za kibinafsi kwa mtu, na kwa ajili ya usalama wa taifa na huhifadhi utawala na ushikamano wake.

Mbali na yaliyotangulia, basi mtandao wa "Twitter" imetangazwa kwamba kuna takriban milioni 1.3 taghrida zina maana ya chuki katika miezi sita iliyopita. Pia mtandao wa "Facebook" ilifuta jumla ya milioni (4) chapisho katika robo ya kwanza ya 2019, na milioni (3.3) katika robo ya mwisho ya 2018, na milioni (2.5) katika robo ya kwanza ya 2018. Aidha, mtandao wa "YouTube" katika robo ya mwisho ya mwaka wa 2018 ilifuta kituo (16,600), na (49,600) kanda za video zenye picha za kikatili, na kanda za video (18,950) zenye maudhui ya chuki, nazo ni nambari zinaonyesha kuongezeka wazi kuhusu jambo hilo.

Mapendekezo

Hakuna shaka kwamba makundi ya kigaidi yanajaribu kufaidikia fursa zote  kwa lengo la kuwavutia wanachama wapya, na kwa ajili ya kukabiliana na suala hilo, jamii ya kimataifa ikiwa serikali, taasisi za kiraia, taasisi za kidini na za kisiasa, zinapaswa kuanzisha kuchukua hatua mbali mbali zinazoiwezesha kuwalinda vijana na wasichana dhidi ya fikra potovu zinazoenezwa na kundi hilo la kigaidi. Na kwa upande wa vyombo vya habari, kielektroniki, kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kinatoa wito wa umuhimu wa:

Kutekeleza sheria za kupambana na halifu za kielektroniki kwa ajili ya kukauka chemchem ya fikra kali.

Kuunda timu kubwa ya wataalamu kwa ajili ya kufanya kazi daima kwa kuangalia na kufuatilia mitandao inayoeneza fikra na maoni ya kali, kisha kuwasiliana na taasisi za kuhusika kwa ajili ya kuondosha mitandao hiyo kwa ajili ya kuwalinda vijana wetu kutokana na fikra kali.

Kutilia mkazo kueneza jumbe kinyume cha fikra kali kwenye mitandao ya mawasiliano ya kijamii kwa ajili ya kudhihirisha uwongo wa jumbe zinazoenezwa na makundi hayo ya kigaidi.

Kutoa kampeni za kielektroniki pamoja baina ya vituo vinavyohusika na kupambana na fikra kali zina (picha, video, hashtag, kura ya maoni, majadiliano) kupitia mitandao ya kielektroniki zinajumuisha jumbe zinazobainisha upotovu wa mifumo ya makundi ya kigaidi na uwongo wake.

Kufanya kazi ya kutoa filamu za sinema zinazoeneza fikra za kiutamaduni na njia za kimwenendo sahihi zinazotegemea misingi ya kuishi kwa pamoja katika amani na upendo baina ya wananchi.

Kuhimiza jamii ya kiraia kwa kufanya jambo lenyewe ili tuweze kujaza nafasi ya kielektroniki na ya habari inayotumiwa na makundi hayo ya kigaidi.

Kuendeleza mfumo wa kielimu unaofanya kwa ajili ya kueneza utamaduni wa usamehevu na kukubali mwingine na unaruhusu kwa kuwepo vijana wenye akili za kukosoa na utamaduni zaidi zinazowalinda dhidi ya fikra kali.

Kuongeza programu za vyombo vya habari zinazoimarisha maadili mazuri ya kidini na kueneza utamaduni wa usamehevu na kukubali mwingine kwa kushirikiana na taasisi za kidini, na taasisi za kiraia na vyombo vya habari.

Kufanyika semina ya kielimu na kuwafahamisha kwa vijana wa vyuo vikuu kwa ajili ya kubainisha upotovu wa propaganda ambayo ISIS inajaribu kuieneza.

Lazima serikali zinafanya kuanzisha programu za marekebesho na kuwarejesha watu wanaotuhuma na kesi za ugaidi, na kujaribu kusuluhisha vyanzo vya maelezo kwa njia kamili.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
3.0

Please login or register to post comments.