Uislamu ndio ni dini ya amani na usalama

  • | Thursday, 13 February, 2020
Uislamu ndio ni dini ya amani na usalama

       Hakika dini ya Uislamu ni dini ambayo inahimiza watu wote wa waislamu  juu ya amani pamoja na wengine, kwani neno la Uislamu linamaanisha kwa kiarabu amani, basi usalama na Uislamu ni maneno mawili yanayoambatana, yenye mfungamano na yasiyotengana. Neno la usalama na minyambuliko yake ni neno lililotumiwa mara nyingi katika aya za Qur'ani tukufu, karibu aya 140 za kitabu hicho cha Mwenyezi Mungu.

      Allah katika kitabu chake anawaita watu kuja kwa maadili ya Uislamu, kama huruma, uvumilivu na amani vinaweza kufanyiwa kazi, basi Mwenyezi Mungu Mtukufu anasema katika aya 208 ya sura ya Al-Baqara:" Enyi mlio amini! Ingieni katika Uislamu kwa ukamilifu, wala msifuate nyayo za She'tani; Hakika yeye kwenu ni adui aliye wazi".

      kama inavyoonekana katika aya hii, Allah anaeleza kuwa usalama wa watu unaweza kuhakikishwa tu kupitia kutekeleza kwa vitendo maadili ya Qur'ani Tukufu. Vile vile Uislamu ni dini inayoeleza na kuhakikisha waziwazi uhuru wa kutafakari na maisha, imetoa maamrisho yanayozuia migogoro kati ya watu, kusemana na hata kuwadhania watu vibaya. Mwenyezi Mungu anasema katika aya 256 ya sura ya Al-Baqara: "Hapana kulazimisha katika Dini. Kwani Uwongofu umekwisha pambanuka na upotofu. Basi anaye mkataa Shet'ani na akamuamini Mwenyezi Mungu bila ya shaka amekamata kishikio madhubuti, kisicho vunjika. Na Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusikia, Mwenye kujua".

       Miongoni mwa misingi na kanuni zinazotawala jamii ya Kiislamu ni kuishi kwa amani na usalama na wasio waislamu. Kwa hakika, Uislamu ni dini ya amani na kuishi kwa usalama na wasio waislamu. Na kwa hiyo, huwezi kupata hata aya moja ya Qur'ani Tukufu inayowalazimisha watu wasio waislamu kukubali dini hiyo kwa vita na mabavu.

       Na hakuna shaka yoyote kwamba suala la kuishi kwa amani na usalama na wasio waislamu limesisitizwa zaidi katika aya za Qur'ani Tukufu na Hadithi za Mtume (S.A.W), na mwenendo wa Mtume wake. Na mtazamo wa Uislamu kuhusu wanadamu wasio waislamu ni wana heshima na utukufu wa kidhati na kimaumbile kutokana na kushirikiana kwao na waislamu katika maumbile na ubinadamu japo wanatofautiana katika dini na imani. Hakika hii inathibitishwa na mwenendo na maisha ya Mtume Muhammad (S.A.W).

      Mfano wa ukweli na wazi wa mwenendo huo wa Mtume kwa amani na wasio waislamu ni Suluhu ya Hudaibiyya yaliyofikiwa baina ya Mtume (S.A.W) na washirikina wa Makka. Basi, mtazamo wa Uislamu kuhusu suala la usalama na kuishi kwa amani na wanadamu wengine wenye itikadi na imani tofauti, ni jambo lenye thamani na umuhimu mkubwa.

        Na Uislamu ni dini iliyoteremshwa ili kujaa ulimwengu wote kwa maisha mema, uadilifu baina ya watu, utulivu na amani ambayo yana huruma isiyo na mwisho, mbali na kuwaua na kuwatisha watu bila ya hatia yoyote kama tunavyoona hivyo hivi sasa kupitia vikundi vya kikali na kigaidi katika ulimwengu wote.  Na Mwenyezi Mungu ameharamisha kuua watu wasio na hatia Kwa mujibu wa Qur'ani Tukufu, kwani kumuua mtu asiye na hatia ni moja ya madhambi makubwa mno, kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika aya 32 ya sura Al-Maida: "…aliye muuwa mtu bila ya yeye kuua, au kufanya uchafuzi katika nchi, basi ni kama amewauwa watu wote. Na mwenye kumuokoa mtu na mauti ni kama amewaokoa watu wote. Na hakika waliwajia Mitume wetu na hoja zilizo wazi. Kisha wengi katika wao baada ya haya wakawa waharibifu katika nchi".

      Na kama inavyoonekana katika aya hiyo kwamba wale wanaoua watu wasiokuwa na hatia wanaonywa na adhabu kali. Na pia, Allah anaeleza kuwa kumuua mtu mmoja ni uhalifu mkubwa mno kama kuua watu wote. Kwa hiyo, sisi sote tunawajibika kufanya jitihada kila siku na katika kila nchi kwa ajili ya kuimarisha amani na usalama. Mtume mtukufu wa dini hiyo, Muhammad bin Abdullah (S.A.W) alisema tangu mwanzoni mwa kutangaza ujumbe aliopewa na Mwenyezi Mungu kwamba lengo lake ni kusimamisha amani, usawa na uadilifu kwa wanadamu wote.

kuhusu suala la kuishi kwa amani na usalama na wasio waislamu katika ulimwengu wote, kituo cha Al-Azhar kwa kupambana na fikra kali kimesisitiza zaidi juu ya jambo hili kupitia ripoti zake mbali mbali kwa lugha ya kiarabu na lugha zingine, na kimebainisha pia kwamba mwislamu wowote aliyelelewa na maadili ya juu yaliyotajwa na Qurani Tukufu anatangamana na kila mtu japo anatofautiana naye katika dini na imani kwa upendo unaotumainiwa na Uislamu.

 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
4.7

Please login or register to post comments.