Qur’ani Tukufu na roli yake katika kupanga mahusiano ya kibinadamu baina ya watu

  • | Sunday, 16 February, 2020
Qur’ani Tukufu na roli yake katika kupanga mahusiano ya kibinadamu baina ya watu

     Hakika Qur’ani Tukufu ndiyo msingi wa suala lolote linalofungamana na Dini ya Kiislamu, nayo ni mfumo ‎unaofaa kila wakati na mahali, na bila shaka kuwa Qur’ani kupitia dhana hiyo ‎thabiti inajumuisha kila linalohitajiwa na ummah wa Kiislamu katika mahusiano yanayofungamanisha baadhi ya wana wake kwa wengineo, bali uhusiano wa ummah wa Kiislamu kwa wengine katika hali mbalimbali. Vile vile Qur'ani Tukufu inaanzisha nyumba ya kiislamu ‎katika jamii ndogo ya mume na mke, na inaweka mipaka ya uhusiano ‎huo katika awamu zake zote na inazijaalia zinasimama juu ya makazi, upendo na huruma, kama alivyosema ‎Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na katika Ishara zake ni kuwa amekuumbieni wake zenu kutokana na nafsi zenu ili mpate utulivu kwao. Naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Hakika katika haya bila ya shaka zipo Ishara kwa watu wanao fikiri) (AR-RUM: 21). Na kauli yake Mtukufu: (Wala msisahau fadhila baina yenu. Hakika Mwenyezi Mungu anayaona mnayo yatenda) (Al-Baqara: ‏237‏).

Hii ina maana kwamba Qur'ani Tukufu haishughulika suala maalumu, mbali na suala lingine, bali inazungumzia masuala yote katika wakati wake maalumu, tunakuta aya zinazozungumzia nyumba ya Waislamu pamoja na masuala ya kijamii, ‎kisha baadaye mahusiano kati ya mataifa, na ile inayojumuisha baina ya viunganisho hivyo vyote na mahusiano baina ‎ya hizo ni hali halisi inayomlazimisha mwislamu aishi pamoja na hivyo, na kutendeana na watu wengi.

Tukiangalia uhusiano baina ‎ya taifa la Kiislamu na mataifa mengine, tunaona kwamba Qur'ani ‎imeuainisha kama yafuatayo: Taifa la Kiislamu ni lenye kuongoza na kulingania kwa Mwenyezi Mungu katika hali ya kwanza, hamu yake ya kwanza ni kuvutia mioyo kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu, na aliyekuwa na kazi kama hiyo, basi hawi kamwe mlinganiaji kwa mgongano na wengine, bali ‎hufanya kazi ili kuvutia mioyo kwa njia sawa, na kuna dalili nyingi kutoka Qur'ani Tukufu zinazobainisha hayo, kama vile: kauli yake Mtukufu: (Nyinyi mmekuwa bora ya umma waliotolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu. Na lau kuwa Watu wa Kitabu nao wameamini ingeli kuwa bora kwao. Wapo miongoni mwao waumini, lakini wengi wao wapotovu) (AL I'MRAN: ‏110‏).

Hapa, taifa la Kiislamu halikujitolewa, Bali lilitolewa kwa ajili ya kuwalingania watu kwa namna iliyo bora kwa Mwenyezi Mungu, na kauli ya Mwenyezi Mungu (Sema: Hii ndiyo Njia yangu - ninalingania kwa Mwenyezi Mungu kwa kujua - mimi na wanao nifuata. Na ametakasika Mwenyezi Mungu! Wala mimi si katika washirikina) (Yousuf: ‏108‏). Uma ni ‎wenye kulingania kwa Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, na mlinganiaji kwa Mwenyezi Mungu hawi na hatakuwa kamwe miongoni mwa walinganiaji wa kupiga vita.

Na miongoni mwa Sunna za Mtume (S.A.W.) kauli yake: "Hakika mlitumwa wenye kusahilisha sio wenye kushadidisha". Na hiyo kwa matini ni utume kwetu sisi waislamu, nao ni ‎utume unaofanana na utume wa manabii, basi pindi Uiislamu ulipokuwa ni baki, basi huo unabakia pamoja na walinganiaji wake. Na miongoni mwa Sunna ya mtume (S.A.W) ya kivitendo kwamba Mtume ‎ (S.A.W.) alikuwa na huruma pamoja na Mayahudi na Wakristo na makabila ya Kiarabu wanaojadiliana naye kwa lengo la kuwavutia, na hiyo tunaikuta ‎katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lilio sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu) (AL I'MRAN: 64‏)

Kwa njia hii iliyojazwa kwa huruma inayoonyesha kuwa msingi wa mahusiano baina ya Waislamu na wengineo ni ‎amani sio vita, na ulaini sio vurugu na malumbano sio mgongano. na maana hii ‎inathibitishwa na aya zingi katika Qur'an Tukufu, nazo hazihesabiwa. Na miongoni mwa aya hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: (Na wakielekea amani nawe pia elekea, na mtegemee Mwenyezi Mungu) (AL – ANFAAL: 61). Na Mwenyezi Mungu Mtukufu Anasema: ‎‎(Anaye kushambulieni nanyi mshambulieni, kwa kadiri alivyo kushambulieni) (Al-Baqarah: 194). Ama anayedai kuwa uhusiano baina yetu na makafiri ni uhusiano unaosimamika juu ya ‎kupigana na kugongana, basi huyu ni miongoni mwa wanaobadilisha dini na wapitao mipaka ambao ni lazima waelewea dini ‎yao au wajiebuke na kutoa fatwa ili wasikosea Uislamu kama inavyotokea ‎siku hizi.

Ama anayehojiana kwa kauli ya Mwenyezi Mungu: (Na piganeni na washirikina wote), basi amesahau kwa makusudi lengo na sababu za aya iliyopita, nazo ni kauli yake Mtukufu: (kama wao wnavyo pigana nanyi nyote), basi lengo la mapigano ni mapigano, na ikiondoka sababu na lengo, ikaondoka vile vile anayesababishana na mwenye kulengwa, pia ‎kuna dalili ya hayo kutoka Sunna ya Mtume (S.A.W.) na sera zake, mtume ‎(S.A.W.) alibakisha Wakristo wa Hajr na akashinda dini zao, aidha alibakisha majus wa ‎Oman na aliwaachia mila yao ya Umajusi.

Vile vile aya iliyomo katika sura ya An-Nisaa (Wanawake) imewajaalia watu wote ni wa tumbo ‎moja na nafsi moja ambayo juu ya msingi wake inasimamika kulingana na msingi wa mahusiano baina ya watu kwa misingi wa ushirikiano katika wema na uchamungu na kubadilishana manufaa ambayo inasimamisha ‎maisha ya watu, kama alivyosema Allah: (Enyi watu! Mcheni Mola wenu Mlezi aliye kuumbeni kutokana na nafsi moja, na akamuumba mkewe kutoka nafsi ile ile. Na akaeneza kutokana na wawili hao wanaume na wanawake wengi. Na tahadharini na Mwenyezi Mungu ambaye kwaye mnaombana, na jamaa zenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mwenye kuwaangalieni) (An-Nisaa: ‏1‏).

Na kutoka hapa tunaweza kusema ‎kwamba Qur'ani Tukufu ni msingi wa kila mahusiano yote baina ya watu sawa katika nyumba moja ambayo ni matofali ya jamii kubwa au kwa taifa la Kiislamu ‎na uhusiano wa baadhi ya watu wake na wengineo, au uhusiano wa taifa la Kiislamu kwa ‎mataifa mengine, na bila shaka kuwa kufuata kwetu kwa Qur'an kutendeana na viumbe vyote kwa maadili ya huruma, usamehe, na upole‏.‏

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
3.8

Please login or register to post comments.