Kwa mnasaba wa kukaribia mwaka mpya wa masomo .. shule ina roli muhimu zaidi katika kupambana na siasa kali

  • | Thursday, 1 October, 2020
Kwa mnasaba wa kukaribia mwaka mpya wa masomo .. shule ina roli muhimu zaidi katika kupambana na siasa kali

     Jamii zetu katika enzi hii ya utandawazi zinashuhudia mabadiliko ya haraka katika nyanja za kielimu, kijamii, kiuchumi, kiutamaduni na kiufundi, na mabadiliko haya yakawa yana athari kubwa kwa vijana, jambo ambalo liliwafanya wengi wao waangukie kwenye wavu wa fikra kali.
     Zaidi ya hayo, mabadiliko haya yanalenga kuwapa vijana utamaduni ‎unaowalazimisha kuwa na utambulisho wa kisekula unaolenga kupigia debe usekula ‎katika kila nyanja ya maisha kiasi kwamba mtu atabakia tu kuwa Mwislamu kwa jina tu, lakini ‎ni msekula kifikra na kivitendo.
     Na bila shaka kuimarisha elimu na kulinda watoto wetu wasijiunge kwa makundi yenye siasa kali ni wajibu wa kidini na kiuzalendo ambao hatupaswi kuuacha. Kwa hivyo, ni muhimu sana kuwafahamisha watoto wetu kwa hatari ya makundi yenye siasa kali, na kuweka mikakati na mipango ya kupambana na ugaidi wa kifikra, hasa katika shule zetu, na kuwakinga vijana katika taasisi za kielimu kutoka kwa mawazo mapotofu kiitikadi na kimaadili, na kukuza usalama wa kimawazo wa wanafunzi kupitia ufahamifu wa vyombo vya habari, mitaala ya mafunzo, na walimu.
     Kwa mujibu wa hilo, Wizara ya Elimu - kupitia shule - lazima isisitize kutahadharisha na siasa kali ya kifikra na makundi ya kigaidi. Na msisitizo huu huwajibisha taasisi zote na watu wote kukuza mradi mkubwa wa kitaifa wa kukabiliana na picha za siasa kali, na chuki katika jamii ambazo wengine huzishika kwa ujinga na labda kwa ajili ya utekaji nyara wa kanuni thabiti za Uislamu na mafundisho yake ya usamehevu.
     Pamoja na familia, Shule inabeba mzigo mkubwa katika kukabiliana na siasa kali ya kimawazo ambayo imetumia teknolojia za kisasa katika kubadilisha dhana kadhaa za vijana na maadili yao, ambayo inahitaji uwezo wa hali ya juu katika kuwafahamisha akili za vijana hao, kuwahutubia kwa lugha ya wakati wao, na kuwaangazia kwa hatari ya siasa kali pamoja na hatari ya machafuko na vuruga. Hii inamaanisha kuwa shule (Idara, walimu, wasimamizi) inapaswa kufanya juhudi kubwa katika kupitisha mazungumzo ya wastani yanayosimamia mambo thabiti na kuhifadhi uzalendo wa vijana.
     Lengo kuu ni kuwalinda watoto wetu dhidi ya vitishio vya ugaidi katika maisha yao. Pia masomo aina hiyo yatawakinga kutokana na uwezekano wa kusajiliwa kwa mafunzo ya kigaidi. 
Kupitia kazi yake muhimu ya kufuatilia makundi ya kigaidi duniani, kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kwa kupambana na fikra kali kimegundua kwamba wanafunzi wa shule na vyuo vikuu wanashawishiwa na wafuasi wa makundi ya kigaidi kwenda kupewa mafunzo ya kigaidi hasa katika bara la Afrika. Vijana kama hawa hutumiwa na makundi ya kigaidi ili kupanga na kutekeleza mashambulizo ya kigaidi.
     Kwa hivyo basi, Kituo cha Al-Azhari kinaona kuwa ugaidi ni changamoto kubwa ambalo bara la Afrika ni lazima ibune suluhisho na mikakati ya pamoja dhidi ya uovu huo. Na kinasisitiza kwamba mataifa ya Afrika yanahitaji kuwa na mikakati thabiti ya kukabiliana na ugaidi, na pia kuweka mipango ya kuwasitisha, kuwarekebisha na kuwarudisha katika jamii wale wanaokuwa na mawazo na mafunzo ya kigaidi.


 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.