Kumtusi Mtume (S.A.W) kwa madai ya uhuru wa maoni ni Silaha hatari ya Wamagharibi ya kueneza Islamophobia

  • | Sunday, 31 January, 2021
Kumtusi Mtume (S.A.W) kwa madai ya uhuru wa maoni ni Silaha hatari ya Wamagharibi ya kueneza Islamophobia

     Baada ya shambulio la kigaidi lililotokea 11 Septemba 2011 huko nchini Marekani, vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) viliongezeka sana barani Ulaya na katika ulimwengu wa kimagharibi kwa ujumla. Kuvunjiwa heshima Qur’ani, Mtume (S.A.W), na matukufu mengine ya Kiislamu kama Kaa’ba na kadhalika yaliwekwa katika ajenda za chuki dhidi ya Uislamu za tawala na vyombo vya habari vya kimagharibi.

Na kwa ajili ya kuhalalisha matukio hayo ya kuvunjia heshima Uislamu, Wahusika walifanya hima ya kuuonyesha kwamba Uislamu ni dini ya misimamo mikali na ambayo inaeneza vitendo vya vurugu na mauaji, na kusema kuwa makundi yenye misimamo mikali yanayojinasibisha kwa Uiislamu kama “Qaeda, Taliban, Daesh, Boko Haram, Al-Shabab” ndiyo ‎yanayoendesha kampeni hiyo chafu dhidi ya dini yao kwa sababu ya vitendo vyao vya kigaidi.

Kwa hivyo, imetangazwa katika mazingira yachukizayo ya kimagharibi kwamba adui ya kweli kwa Magharibi ni Uislamu - kwa mujibu wa maoni yao bandia - na imeandaliwa kimorali na kinyenzo kwa kusudi hili, na kupangwa mikakati, ili majibu yawe katika mfumo wa nadharia za kitamaduni, vita vya kijeshi, na mapambano ya vyombo vya habari (MEDIA) yanayojumuisha njia za mawasiliano, sinema na sanaa kwa jumla, bali jambo limewahi kwa kuathiria watoto na watu wazima kupitia vibonzo na katuni.

Na tukichunguza historia, tunakuta kwamba chuki dhidi ya Uislamu imechukua aina mbalimbali, kati yake kushambuliwa na kuvunjiwa heshima wanawake wanaovaa vazi la hijabu, au kukejele vijana waliokuwa wakielekea au kutoka msikitini. Vile vile kuchoma moto misikiti na hata kuandika maandishi ya kibaguzi katika kuta za misikiti. Aidha Kuchoma moto au kutiwa najisi Msahafu Mtukufu wa Qurani au kukata karatasi zake.

Lakini Chuki dhidi ya Uislamu (Islamophobia) katika nchi za Magharibi zimeongezeka mno katika nyakati za hivi karibuni, hasa wimbi la vitendo vya utumiaji mabavu na kuvunja heshima ya Mtume wa Uislamu (S.A.W). mara hii imejaali nchi kadhaa za Kiislamu na Kiarabu kulaani kitendo hicho, na kutoa mwito wa kusisiwa bidhaa za Ufaransa katika nchi hizo ukishika kasi.

Lakini hii si mara ya kwanza kwa Magharibi kumtusi Mtume mtukufu wa Uislamu, Karibu miaka 30 iliyopita “Salman Rushdie” mwandishi raia wa Uingereza mwenye asili ya India aliandika kitabu dhidi ya Uislamu cha "Aya za Shetani" ambacho ndani yake aliandika mambo ya kumtusi na kumvunjia heshima Mtume (S.A.W) na masahaba zake.

Mwaka 2005 na katika hatua iliyochukuliwa kwa shabaha maalumu, kwa mara ya kwanza jarida moja linalochapishwa nchini Denmark lilichapasisha vikatuni vya kumvunjia heshima Mtume (S.A.W) Mwaka mmoja baadaye, mtengenezaji filamu mmoja wa Uholanzi alivitumia vikatuni hivyo vya kumvunjia heshima Mtume vilivyochapishwa Denmark, kuwa maudhui kuu ya filamu aliyoamua kutengeneza.

Mwaka 2012 jarida la “Charlie Hebdo” lilichapisha vibonzo ilivyodai ni Mtume Muhammad ‎‎(S.A.W) kitendo kilicholeta mhemko mkubwa kwa Waislamu duniani ambapo mwaka ‎‎2015 ofisi zake zilishambuliwa na kupelekea kuuwawa watu 12.  Tayari wanawake wa ‎Kiislamu nchini humo wamekuwa wakinyanyapaliwa kwa kuvaa niqab.‎

Mnamo mwaka 2015 jarida la Kifaransa la “Charlie Hebdo” liliughadhibisha Ulimwengu wa Kiislamu na kuziungulisha nyoyo za Waislamu kwa machungu lilipochapisha vikatuni vya kumtusi na kumvunjia heshima Bwana Mtume Muhammad (S.A.W).

Lakini kama vile haitoshi, jarida hilo katika 2020 limeamua kurudia tena kitendo hicho cha kishenzi; na mara hii rais “Emmanuel Macron wa Ufaransa ameunga mkono na kuutetea uovu huo kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza na kutoa maoni.

Wataalamu wengi wa mambo wanasema kwamba lengo hasa la madola ya Magharibi kutumia nguvu zao zote za kupambana na Uislamu ni hofu kubwa walionayo kutokana na dini hiyo kuzidi kupata wafuasi katika nchi zao. Kwa hiyo wanajitahidi kufanya kila kitu kwa kuzuia dini hiyo ya kiislamu kueneza. lakini hujuma hizo hazijasaidia chochote kwani watu wanaosilimu na kuingia katika Uislamu katika ulimwengu wa Magharibi wamekuwa wakiongezeka kila leo. Hii ni kutokana na kuwa, mafundisho ya Uislamu yamejengeka juu ya akili, mantiki, maumbile na hali ya kati na kati.

Mwishowe, kituo cha uangalizi cha Al-Azhar kwa kupambana na fikra kali kinasisitiza kwamba kutoa maoni juu ya jambo lolote ni haki iliyodhaminiwa kwa yeyote, lakini liwe ndani ya mipaka. Na Al-Azhar Al-Sharief kinakataa kiumbo na kimadumuni kumvunja heshima Mtume wa Uislamu (S.A.W) na Manabii wote wa Allah kwa kisingizio cha uhuru wa kujieleza, ikiongeza kuwa ni kosa kubwa kumvunja heshima ya Mtume (S.A.W) kwani Mwenyezi Mungu ‎Mtukufu Mwenyewe Ametangaza kuwa yupo katika tabia njema. Na kituo cha Al-Azhar kinatoa mkazo mkubwa kuwa Uislamu ni dini ya amani na upendo na inayopinga kuwaua watu wasio na hatia yoyote, kuporwa mali zao, au kudhulumiwa mtu, na kwamba Uislamu unajitenga na kuwa mbali na makundi hayo ya kigaidi na katu hautetei wala kuunga mkono vitendo vinavyofanywa na makundi hayo ya kigaidi. 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.