Hatari za Kuwaondoa Askari wa Marekani nchini Somalia

  • | Thursday, 11 February, 2021
Hatari za Kuwaondoa Askari wa Marekani nchini Somalia

     Katikati ya vitendo vya kigaidi ambavyo Somalia inashuhudia, na mashambulio yanayofanywa na kundi la Al-Shabaab nchini dhidi ya sekta zote za jamii, na watu wote hata wakiwa raia au wanajeshi, vijana au wazee, au hata watoto. Somalia ilipata pigo lenye uchungu kwa sababu ya kujiondoa kwa vikosi vya Marekani vilivyokuwa hapo.
Hii ilikuja ndani ya mpango wa Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump, kwa lengo la kupunguza vikosi vya Marekani ulimwenguni kote na kuwaondoa kutoka maeneo ya vita. Pentagon ilitangaza kukamilisha kuondolewa kwa vikosi vyake vya kijeshi kutoka Somalia, ambavyo ni kati ya wanajeshi 600 hadi 800.
Mtu anayechunguza suala la Somali anatambua kuwa, hakuna vikosi vya Marekani au Jumuiya ya Ulaya vilivyowekwa au vilivyowekwa kwenye kituo kikuu, lakini kuna wataalam kadhaa wa kijeshi kwa ajili ya msaada na msaada wa vifaa(kilogesti), pamoja na baadhi ya Wanajeshi wa Marekani wanaohamia karibu na pwani za Somalia, na wanafanya mashambulizi ya haraka kwa makao ya Al Shabab.
Na kwamba vikosi vyenye ushawishi ni walinda amani, ambao wanaundwa na vikosi vya Uganda, idadi yao inafikia zaidi ya 10,000 na wamepewa vifaa, vifaa vya vita na silaha za kutosha ili kushinda wakati wa kutokea makabiliano na Al-Shabaab, vikoso ambavyo baada yake ni majeshi ya Burundi yanayokadiriwa kwa 5,000 askari, ambao hawana silaha ndogo zaidi kuliko vikosi vya Uganda. Ama Hatari halisi iko katika kuondolewa kwa vikosi hawa au kukoma kwa msaada kutoka Umoja wa Mataifa na Jumuiya ya Ulaya.
Hakuna shaka kuwa kuondolewa kwa majeshi ya Marekani kunaleta changamoto kubwa ya usalama na kuuweka utulivu wa Somalia hatarini, Hasa  wakati Wasomali walijishughulisha na uchaguzi  . Hii inawawezesha Al-Shabaab kurejesha shughuli zao na kuongeza udhibiti na upanuzi wa miji na maeneo mapya nchini Somalia.
Jambo linalostahiki kutajwa kuwa Al-Shabaab  wametumia faida ya uondoaji huu na waliongezeka mara mbili shughuli zake, ambazo zilifuatiliwa na kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali  mwezi Januari jana. Katika mwezi huu, kundi la kigaidi la "Al-Shabab" lilizindua operesheni karibu za (38) kigaidi, ambapo takriban watu 120 waliuawa na wengine 139 walijeruhiwa. Hiyo ni, zaidi ya mara mbili ya shughuli zake kabla ya kujiondoa
Na Kituo cha Al Azhar cha kupambana na fikra kali  kinaamini kuwa uondoaji huu hauzingatiwi  mzigo kwa Somalia, ikiwa vikosi vyote nchini Somalia vitajiunga na nguvu ili kuziba pengo lililoachwa na uondoaji wa Marekani, kupitia upangaji mzuri pamoja na uratibu na vikosi vya umoja wa kimataifa vilivyopo hapo.
Kituo cha Al Azhar pia kinatoa wito kwa serikali ya Somalia kutafuta njia mbadala za kukabiliana na tatizo hilo, na njia hizi zinaweza ziwe, kutafuta washirika wapya katika vita dhidi ya ugaidi kupitia Baraza la Usalama la UN, kuinua uwezo wa kupambana wa vikosi vya Somalia, na kuimarisha majukumu ya ujumbe wa walinda amani wa Kiafrika nchini pamoja na uratibu Na nchi jirani.
 

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
3.0

Please login or register to post comments.