Nigeria baina ya ugaidi na waliotoroka gerezani

  • | Saturday, 10 April, 2021
Nigeria baina ya ugaidi na waliotoroka gerezani


     Kwa kweli, siku hizi,  Nigeria inakabiliwa na changamoto kadhaa. mwangalizi katika mambo ya Kiafrika, hasa katika nchi za Afrika Magharibi, ataona kwamba, nchini Nigeria, inakabiliwa na changamoto nyingi zinazoilemea. Miongoni mwa changamoto muhimu zaidi ni "uzushi wa ugaidi".
Nigeria iko chini ya mwogofyo wa kundi la kigaidi ambalo ni mmoja ya vikundi vya kigaidi maarufu zaidi barani Afrika, pia ni maarufu duniani. kundi hili ni Boko Haram. 
Tangu kuanzishwa kwake, kundi hili "Boko Haram" halijasita kutekeleza vitendo vya kigaidi dhidi ya raia wasio na hatia, au jeshi na vikosi vya polisi nchini. Imefanya mauaji mabaya kabisa dhidi ya raia, na ilifanya mambo yote haramu. Kama vile, biashara kwa watu, dawa za kulevya, silaha ...nk.
Kwa kweli, Nigeria imezoea changamoto hizi na sasa inachukua kila njia kuzizuia na kuzikabili na pia kupunguza na kumaliza kuenea kwao.
Lakini kilicho kipya katika suala hili ni kile ambacho kimetangazwa  katika vyombo vya habari hivi karibuni juu ya kutoroka kwa wafungwa karibu 2000 kutoka gereza  mmoja la Nigeria, linaloitwa Owerri katika Jimbo la Imo kusini mashariki mwa Nigeria, baada ya watu wenye silaha kushambulia kwa vilipuzi na mabomu na kurusha roketi. Hii inaongeza saizi ya changamoto dhidi ya Nigeria, na inasababisha kuongezeka kwa idadi ya magaidi nchini. Inatarajiwa kwamba mzunguko wa vitendo vya kigaidi utaongezeka mwezi huu ikilinganishwa na Machi iliyopita.
Kupitia Kituo cha Al-Azhar cha Kupambana na fikra kali, shughuli za vikundi vya kigaidi barani Afrika zilifuatiliwa. Miongoni mwa vikundi hivi kulikuwa na Boko Haram nchini Nigeria, ambalo lilikuwa kundi lenye umwagaji damu zaidi barani Afrika, wakati limefanya karibu (25) operesheni  mnamo Machi, kuua takriban (100) Kuuawa. Hii ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na Februari iliyopita, wakati kikundi kilifanya operesheni (16) tu.
 Kwa kuongezea, kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali  inaamini kuwa kushambulia gereza na kusafirisha idadi hii kubwa sio chochote bali ni hatua ya kikundi cha "Boko Haram" kujibu matamshi ya Rais wa Nigeria "Bukhara"  na ahadi yake ya kumalizia kundi hilo katika mwaka mmoja.
Kwa hiyo, kituo cha Al-Azhar cha kupambana na fikra kali inatoa wito kwa wigo wote wa kisiasa na kijamii nchini Nigeria kuungana mikono na kuweka mipango muhimu ya kuwakamata watororoki hawa na kuwarudisha kwenye gereza yao, na kuchukua hatua zote muhimu ili kuepuka kutokea kwa tukio kama hilo baadaye, na vile vile kubuni mikakati mipya ya kulikabili kundi hili na kuzuia kuenea kwake.

Print
Categories: Makala
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.