Katika mkutano wake na Mkuu wa Bunge la kifaransa (Baraza la Seneti)

  • | Friday, 27 May, 2016
Katika mkutano wake na Mkuu wa Bunge la kifaransa (Baraza la Seneti)

Imamu Mkuu:

* Tuna hamu kubwa ya kupambana na mawazo makali..na tuko tayari kuanzisha kituo cha kiutamaduni mjini Paris kwa lengo la kufundisha mawazo sahihi ya dini.

* Inabidi kuanzisha bodi inayohusiana na kusimamisha misikiti iliyopo nchini Ufaransa…na hatuna dhiki kuwapa maimamu matayarisho bure.

Mkuu wa Bunge la kifaransa:

* Hakuna suluhisho jingine linalofaa zaidi isipokuwa mazungumzo baina ya mashariki na magharibi…na hotuba yako Ewe Mheshimiwa inaanzisha mazungumzo yanayotarajiwa kuleta matokeo mazuri.

* Tuna matatizo mengi kuhusiana na maimamu wa misikiti nchini mwetu…na tuna tama kwamba Al-Azhar itatusaidia kuyatatua. 

Mheshimiwa Imamu mkuu profesa; Ahmad Al-Tayib, Sheikhi mkuu wa Al-Azhar Al-Shareif na mkuu wa Baraza la wakuu wa waislamu, alisisitiza leo Alhamisi kwamba Al-Azhar ina hamu kubwa kupambana na mawazo makali ulimwenguni kote, akielezea kuwa Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kuanzisha kituo cha utamaduni wa kiislamu kitakachoendeshwa na Al-Azhar mjini Paris kwa ajili ya kueneza mawazo sahihi kuhusu ukweli wa dini na dhana zake zilizo sawa na kuwakinga vijana wa kiislamu kutoka mvutano wa makundi ya kigaidi.

Yule Mheshimiwa alisema katika mkutano wake na Gerard Larcher, Mkuu wa Bunge la kifaransa (Baraza la Seneti), kwamba Al-Azhar Al-Shareif iko tayari kushirikiana na Ufaransa katika uwanja wa kuwapa maimamu wa kifaransa mazoezi mjini Kairo na kwamba Al-Azhar itagharamia mazoezi hayo yote ili kuwafundisha maimamu hao kutokana na mbinu ya kiwastani ya kiislamu ambayo inafundishwa katika Al-Azhar Al-Shareif.

 Mheshimiwa Imamu Mkuu aliongeza kwamba kwa mujibu wa kufundisha Uislamu kutokana na mbinu ya kielimu ya kiwastani jambo lililowakinga wasomi wa Al-Azhar wa hivi sasa na wa zamani wasijiunge na kundi lo lote la kigaidi hata mmoja, akisisitiza kuwa Uislamu haihusiani kabisa na wale wanaofanya jinai kwa jina la dini ilhali dini haihusiani na jinai hizo hata kidogo.

 Pia, Mheshimiwa Imamu mkuu aliashiria kwamba tatizo la waislamu wa kifaransa linatokana na kwamba maimamu wa nchi hiyo wametoka nchi mbali mbali wakibeba fikira tamaduni tofauti zisizoafikiana na mbinu ya kiwastani ya Uislamu, kwa hiyo inabidi kuanzisha bodi latakalosimamisha misikiti na maimamu nchini Ufaransa, na litakalodhibiti hotuba na mafunzo yanayotekelezwa misikitini.

Kwa upande wake Mkuu wa Bunge la kifaransa (Baraza la Seneti) Gerard Larcher, alimkaribisha Mheshimiwa Iamamu mkuu akielezea furaha yake kwa ziara hiyo ya Imamu mkuu zaidi duniani wa waislamu, akielezea heshima yake kwa Al-Azhar Al-Shareif na imamu waku mkuu.

Vile vile, Larcher aliisifu hotuba ya kimataifa aliyoitoa Imamu Mkuu mjini Paris kwa mataifa wa barani Ulaya na waislamu wa ulimwengu wote, ile hotuba iliyosisitiza umuhimu wa mazungumzo na kuishi pamoja kwa waislamu wa kifaransa katika jamii yao na kuhakikisha maadili ya kusameheana na kuishi pamoja, pia aliusifu mkataba wa ushiriiano uliotiwa saini

baina ya Chuo kikuu cha Al-Azhar na Chuo cha Kikatholiki ambacho kinazingatiwa sehemu ya historia ya Ufaransa.

 Larcher alibainisha pia kwamba kuna baadhi ya matatizo kwa maimamu wa kifaransa, akielezea matarajio ya nchi yake kushirikiana na Al-Azhar Al-Shareif kuyatatua matatizo hayo kupitia kueneza mawazo yaliyo sawa na kupigania vita vurugu na ugaidi.

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.