• Ukhalifa katika lugha ni kutoka tamko la خلفه يخلفه kwa maana ya alimfanya nyuma yake basi yeye ni خليفة naye ni yule anayefuata aliyemtangulia.
• Na katika Istilahi Ukhalifa ni; kuendesha mambo ya dunia na kuwachunga waja kwa mujibu wa sharia za Mwenyezi Mungu (S.W.).
• Jukumu la kimsingi la Ukhalifa ni kuendesha mambo ya dunia kwa mujibu wa mafunzo ya dini na kuhifadhi dini na kuichunga, basi ye yote akidai kuwa alijitangaza ukhalifa pasipo na kujilazimika majukumu ya khalifa basi yeye ndiye mwongo dhahiri.
• Ukhalifa katika Uislamu ni mfumo wa kisiasa haukusuduwi kwa maana dhahiri yake bali hukusudiwa kwa madhumuni yake hata ukiitwa kwa jina jingine mbali na Ukhalifa.
• Tamko la Khalifa katika lugha huitwa kwa kila mtawala anayekuja baada ya mtawala mwingine kabla yake, na katika istilahi tamko hilo haliitwi ila kwa yule aliyemfuata Mtume (S.A.W.) katika siasa ya kuendesha dunia kwa mujibu wa dini.
Attirmidhiy alisimulia katika kitabu chake cha Sunan na Annasaaiy na Abu Daudi na Ahmad katika kitabu chake cha Musnad kwa matamshi yanayofanana ya kauli yake Mtume (S.A.W.): "Ukhalifa utakuwepo katika ummah wangu kwa miaka thelethini, kisha itakuwa mfumo wa ufalme baada ya hapo" maana ukhalifa utakuwepo katika zama za utawala wa makhalifa waongofu Abu Bakr, Omar Bin Al-Khattab, Othman, Ali Bin Abi Talib na Al-Hassan Bin Ali (R.A.), ambapo mifumo yote ya kisiasa iliyokuja baada ya watawala hao ndiyo ufalme na utawala kwa maana ya kiistilahi sio ukhalifa wa kidini kutoka kwa Mtume (S.A.W.) bali mahakimu na watawala walipewa jina la khalifa kwa kuzingatia maana ya kilugha ambapo walifuata watawala waliowatangulia.