Majibu ya Mawazo Makali

Mifano ya kuishiana baina ya Uislamu na dini zingine

3

  • | Sunday, 15 January, 2017

Kuishiana baina ya dini tofauti ndio kuishiana baina ya tamaduni na staarabu mbali mbali unaolengea kuyahudumia malengo ya juu ambayo mwanadamu daima hujitahidi kuyahakikisha. Tunaona kwamba msimamo wa Uislamu kuhusu kuishiana baina ya dini tofauti unadhihiri sana katika kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu: {Sema: Enyi Watu wa Kitabu! Njooni kwenye neno lililo sawa baina yetu na nyinyi: Ya kwamba tusimuabudu yeyote ila Mwenyezi Mungu, wala tusimshirikishe na chochote; wala tusifanyane sisi kwa sisi kuwa Waola Walezi badala ya Mwenyezi Mungu. Na wakigeuka basi semeni: Shuhudi- eni ya kwamba sisi ni Waislamu} (Al-Imran:64)

Na miongoni mwa sifa za kuishiana baina ya Uislamu na wafuasi wa dini tofauti ni kwamba Uislamu unawazingatia wafuasi wa uyahudi na ukristo ni watu wa kitabu, ingawa wao hawaamini utume wa Mtume Muhammad (S.A.W.), lakini Uislamu kwa juhudi zake za kuyarekebisha mambo na wito wake kwa kuishiana pamoja, ulikubali hitilafu hiyo yakiwemo mafundisho yanayorahisisha kuwasiliana na kuhurumiana baina ya watu japokuwa kutofautiana katika itikadi, kwa kila aina za tabia njema na adabu, basi kuwaamini Musa na Issa ni sharti mojawapo masharti za imani sahihi. Pia, miongoni mwa mifano ya kuishiana pamoja inayoonyesha hamu ya Uislamu juu ya kuishiana pamoaj kwa amani, ni kwamba mwislamu anaweza kumwoa mwanamke asiye mwislamu sawa sawa akiwa  myahudu  au mkristo, Mwenyezi Mungu Mtukufu Amesema: {Leo mmehalalishiwa kila vilivyo vizuri. Na chakula cha waliopewa Kitabu ni halali kwenu, na chakula chenu ni halali kwao. Na pia wanawake wema miongoni mwa Waumini, na wanawake wema miongoni mwa waliopewa Kitabu kabla yenu, mtakapowapa mahari yao, mkafunga nao ndoa, bila ya kufanya uhasharati wala kuwaweka kinyumba}(Al-Maidah:5)

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.