Kumkafirisha Mwingine

1

  • | Monday, 2 January, 2017

Sheria ya kiislamu inataka kuwakomboa watu kutoka aina yoyote miongoni mwa sura za utumwa, isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu (S.W.) Ambaye Amelifanya suala la imani na ukafiri ndilo siri baina ya mja na Mola wake tu….kwa hakika Mtume (S.A.W.) ametufundisha kuamiliana na watu kwa mujibu wa matamshi yanayotolewa na ndimi zao, na tusitoi hukumu kuhusu mioyo ya viumbe, na tusitafuti na kuwagawanya watu kwenye makundi ya waumini na makafiri, kwani hakuna ye yote anayejua yaliyomo mioyoni isipokuwa Mola wa ulimwengu…. Tunawahukumia watu kulingana na yanayodhihiri, na Mwenyezi Mungu Anajua yanayofichwa moyoni, yeye peke yake Atawapa waja wake malipo yao.
Ama yanayotolewa sasa na makundi ya kigaidi kuhusu ukafirishaji wa kila mwenye kuwapinga au anayetofautiana nao, na kila asiyefuata mbinu yao yenye kumwaga damu basi hii ndiyo upotofu mkubwa mno usio na uhusiano wo wote na dini ya Mwenyezi Mungu, wakati ambapo watu hao wanavunja mafundisho yote ya Uislamu yaliyo wazi kuhusu jambo hilo, na kwa hakika Mtume (S.A.W.) ametahadharisha kutoka mwislamu mmoja kumkafirisha mwenzake, au kumhalalisha damu yake, mali yake na heshima yake.
Makundi ya ukafirishaji yamezoea kutoa istilaha ya ukafiri na kuritadi juu ya waislamu wote wanaokwenda kinyume cha rai zao potovu kwa ajili ya kuhalalisha kuwaua na kuziharibu nyumba zao! Basi kutoka wapi watu hawa wamepata mafundisho yao haya?! Ilhali Mtume (S.A.W.) Amebainisha imani katika hadithi sahihi wakati Jibril (A.S.) alipomwuliza akisema: “Ewe, Mtume niambie kuhusu Imani!” akasema Mtume: “Imani ni kumwamini Mwenyezi Munguu, Malaika wake, vitabu vyake, mitume wake, siku ya mwisho na kadari kheri yake na shari yake”. (imepokewa na Bukhari na Muslim). Na wanazuoni wa kiislamu wamekubali kwamba imani ni tendo la moyo, yaani mtu hawi mkafiri isipokuwa akikanusha mojawapo (sababu/nguzo) za kumfanya mumini. Mtume (S.A.W) amesema: {Mtu yeyote anayemwita mwenzake kuwa ni mkafiri basi tuhuma hiyo itapata moja wao}. (Sahihul-Bukhari, 2264/5).

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.