Adhabu za kisheria katika Uislamu

6

  • | Wednesday, 15 February, 2017

Kwa kweli adhabu za kisheria zimewekwa katika Uislamu kwa ajili ya kupatiliza (kutotenda makosa) na kuilinda jamii, sio kwa ajili ya kulipiza au kuadhibuu, Je! Kuna nchi yo yote katika wakati uliopita au wa kisasa haitungi sheria na kupitisha adhabu kwa ajili ya kuilinda jamii yake kutokana na maovu ya wahalifu wanaovunja sheria hizo? Basi adhabu za kisheria katika Uislamu sio isipokuwa njia mojawapo njia za kuhifadhi mambo muhimu ya mwanadamu asiyeweza kuishi pasipo nayo, kama vile; nafsi yake, nasaba yake, na mali yake, kwa hivyo adhabu za kisheria zinazingatiwa kuwa ni ulinzi kwa mwanadamu aliyetukuzwa na Mwenyezi Mungu Aliyesema: {Na hakika tumewatukuza wanaadamu, na tumewapa vya kupanda nchi kavu na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewafadhilisha kwa fadhila kubwa kuliko wengi miongoni mwa tulio waumba} [Al-Israa:70].

Kwa hakika Uislamu ambao ni dini ya Uadilifu na Huruma, ulipopitisha adhabu za kisheria unaweka sharti ambazo aghalabu zinatekelezwa kwa nadra sana, kwa hivyo basi, kutia masharti magumu ya kuthibitisha uhalifu, kubatilisha adhabu kwa shaka hata ikiwa ndogo kabisa, au kwa kukana kwa mhalifu baada ya kukiri kwake … zote ni njia za kumwokoa mtuhumiwa au mtu anayedhaniwa kufanya uhalifu kutoka adhabu za kisheria, kwani Mtume wa Rehema (S.A.W.) amesema: “Zuieni adhabu za kisheria na mzitie mbali na waislamu kama mwezekanavyo, basi mtuhumiwa akiwa na sababu  au dalili ya kujiokoa mwachilieni, kwa hakika Imamu (Kadhi) akikosa akamwachilia huru mtuhumiwa ni bora zaidi kukosa katika kupitisha adhabu”  

Kwa hiyo, Uislamu haukuacha kupitisha zile adhabu za kisheria - ikiwa kuna dharura zitekelezwa ــ kwa mtu ye yote au kundi lo lote hata likifika cheo cha juu zaidi, bali umeziweka adhabu chini ya utawala wa nchi. Kwa hivyo ye yote anayejipatia haki ya kutekeleza adhabu za kisheria sawa ni mtu binafsi au kundi fulani, basi huwa ni mhalifu anayekwenda kinyume na sheria ya Mwenyezi Mungu.

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.