Kuwalazimisha wasio waislamu kujiunga Uislamu

  • | Sunday, 6 August, 2017
Kuwalazimisha wasio waislamu kujiunga Uislamu

     Swali: je, wasio waislamu wanalazimishwa kufuata Uislamu kwa mujibu wa kauli ya Mwenyezi Mungu ) Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipokutoeni  (, {Al-Baqarah:191}?
Jibu la swali
Kwanza: fikira ya Qurani ya kugawanya viumbe kwenye waumini kwa Uislamu na makafiri kwa Uislamu inakuwepo kweli katika Qurani tukufu, lakini fikira hii inashirikiwa na sheria na dini zote, basi haipo dini ambayo inakiri akida yake pamoja na akida za dini nyingine katika wakati moja , ugawanyiko huu ni ugawanyiko wa wasifu, basi ikiwa Uislamu unalingania  kufuata kundi la akida, ibada na tabia, ni kawaida kwamba hukubaliwa na  baadhi ya watu hukufuriwa na baadhi nyingine.

Pili: kukata matini kutoka muktadha wake kunapelekea kukata maana na kubadilisha  makusudio ya aya kabla ya kukatwa kutoka maana yake kamili.
Na hilo linadhihirisha katika kutoa dalili iliyotajwa katika swali kwamba Uislamu huamrisha  kuwapigania wasio waislamu kwa mujibu wa  kauli ya Mwenyezi  Mungu: ) Na wauweni popote mwakutapo(, lakini tukisoma matini ya  Qurani mwanzoni mwake itadhihirika kwetu ufahamu mbaya wa aya za Qurani, pale ambapo inadhihiri kwamba Qurani inahimiza kutumia nguvu, Mwenyezi Mungu Anasema: ) Na wauweni popote mwakutapo, na muwatoe popote walipokutoeni kwani fitina ni mbaya zaidi kuliko kuuwa. Wala msipigane nao kwenye Msikiti Mtakatifu mpaka wakupigeni huko. Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni. Na hivi ndivyo yalivyo malipo ya makafiri Lakini wakiacha basi Mwenyezi Mungu ni Mwenye kusamehe Mwenye kurehemu. Na piganeni nao mpaka pasiwepo fitina, na Dini iwe ya Mwenyezi Mungu tu. Na kama wakiacha basi usiweko uadui ila kwa wenye kudhulumu (, {Al-Baqarah:190.193}. 
Licha ya uwazi wa aya hizo na kutokuwepo haja ya kueleza zaidi, lakini yumkini tuangalie kwamba imepa maana mbali na maana iliyokatika kutoka matini katika tuhuma hii, basi aya ya kwanza imetilia mkazo ulazima wa kupigana vita anayewapigana waislamu vita tu, na imekataza kwa namna  wazi kushambulia, kwani kushambulia kunakuwa kwa ajili ya kutetea tu, na kama adui aking'ang'ania kutekeleza uhalifu wake, basi aya ya pili imefafanua njia ya kuamiliana naye na inajaribu kupunguza mapigano  ilipokataza kupigana vita ndani ya  msikiti mtakatifu madamu adui hakung'ang'ania kupigana vita ndani yake, na sharti iliyopita imekaririwa mara nyengine ) Wakikupigeni huko basi nanyi pia wapigeni (, kisha aya hizo mbili zinaeleza kwamba vita inakuwa ni dharura ni lazima iachwe haraka wakati mshambuliaji anapoacha moja kwa moja. 
Tatu: kudai kwamba Uislamu unalazimisha wasio waislamu kufuata uislamu kwa nguvu ni kosa kwa dalili ya Qurani inayokadhibisha katika pahala kadhaa, Mwenyezi Mungu Anasema ) Zimekwisha kukujieni hoja wazi kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anayeona ni kwa faida yake mwenyewe, na anayepofuka basi ni khasara yake. Nami si mtunzaji wenu. Na namna hivyo tunazisarifu Aya, na wao wakwambie: Umesoma. Na ili tuyabainishe kwa watu wanao jua. Fuata uliyofunuliwa kutoka kwa Mola wako Mlezi. Hapana mungu ila Yeye. Na jitenge na washirikina. Na lau Mwenyezi Mungu angelipenda, wasingelishiriki. Na Sisi hatukukufanya wewe uwe mtunzaji wao. Wala wewe si mlinzi juu yao. Wala msiwatukane hao wanao waomba badala ya Mwenyezi Mungu, wasije na wao wakamtukana Mwenyezi Mungu kwa jeuri bila ya kujua. Namna hivyo tumewapambia kila umma vitendo vyao. Kisha marejeo yao yatakuwa kwa Mola wao Mlezi, naye atawaambia waliyokuwa wakiyatenda (,{Al-Anaam:104.108}.
Na Mwenyezi Mungu anasema pia ) Sema: Enyi watu! Haki imekwisha kukujieni kutoka kwa Mola wenu Mlezi. Basi anayeongoka anaongoka kwa faida ya nafsi yake, na anayepotea anapotea kwa khasara ya nafsi yake. Na mimi si mwakilishi juu yenu. Na wewe fuata yanayofunuliwa kwako kwa wahyi. Na vumilia mpaka Mwenyezi Mungu ahukumu, na Yeye ndiye mbora wa mahakimu (,{Al-Anaam:104.108}.
Hiyo ni mifano miwili ya aya ya qurani inayoondosha mashaka na pia  haimkalifisha Mtume (S.A.W) juu ya uwezo wake, kwani wote wanarejea kwa Mwenyezi Mungu )Na wakipuuza, basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao. Si juu yako ila kufikisha Ujumbe tu(, {Ash-Shura:48}. Mwenyezi Mungu hakumwamrisha Mtume wake kwa kusema: (wakipuuza uwapigane nao au uwalazimishe waamini) bali Amesema: ) basi Sisi hatukukupeleka ili uwe mwangalizi wao(, je, makundi haya yanayowalazimisha watu wafuate Uislamu yana haki zaidi ya Mtume kwa Uislamu. 
Na tunasema kwamba kukata aya kutoka matini zake ni sababu kuu katika kutokea upotovu mbali na mfumo wa Uislamu sahihi.


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.