Tuhuma ya kuwasaidia na kuwaunga mkono makafiri na kuomba msaada wao

  • | Tuesday, 8 August, 2017
Tuhuma ya kuwasaidia na kuwaunga mkono makafiri na kuomba msaada wao

      Wanadai kwamba kuwasaidia na kuwaunga mkono makafiri ni haramu na ukafiri kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu:" na atakayewafuata (atakayetawaliwa nao) miongoni mwenu, basi ni miongoni mwao". Kwa hivyo atakayewasaidia kwa mali, silaha, neno au kwa mwili basi ni mkafiri na anastahiki kuuwawa   
Kuijibu tuhuma:
Tunasema kwamba: jumhuur ya wanachuoni wameafikiana kwamba inajuzu kuomba msaada kutoka makafiri wakati wa dharura, maana kama waislamu wakihitaji msaada kutoka makafiri katika vita yao dhidi ya adui inajuzu lakini kwa sharti ya kwamba mkafiri anakuwa mwenye rai nzuri kuhusu waislamu na ujasiri, na dalili ya hiyo kwamba Mtume (S.A.W) ameomba msaada kutoka makafiri katika vita ya Hunayn, na wametoka naye katika vita hiyo watu wasio waislamu kutoka Makkah ambao hawafuati Uislamu, miongoni mwao ni Safwaan Ibn Umayyah na Mtume (S.A.W) ameweka ngao yake ya chuma rahanini kwenye myahudi mmoja, na wengine wametoka pamoja na Mtume kabla ya kusilimu, basi hii ni dalili kuhusu uhalali wa kuomba msaada kutoka  wasio waislamu wakati wa haja au dharura, Ibn Al-Qayyim katika kitabu chake Zaad Al-Maad pamoja na kundi la wanachuoni wameafikiana kuhusu rai isimayo kwamba wakati wa dharura inajuzu kuomba msaada wa makafiri lakini kwa sharti mkafiri huyo  asiwe na madhara dhidi ya waislamu, kwani hao makafiri labda watawafaidisha waislamu kwa sababu wanajua siri za maadui na makafiri wengine na wanajua hali zao zaidi ya waislamu.  
Kwa upande mwengine hakika kuliangamiza kundi la Daesh miongoni mwa kumcha Mwenyezi Mungu na kutenda wema ulio bora zaidi, na Mwenyezi Mungu Amehimiza kusaidiana akisema: )na saidianeni juu ya kutenda wema na kumcha Mungu wala msisaidiane juu ya madhambi na uadui(, {Al-Maidah:2}. Na katika kitabu sahihi cha Al-Bukhari katika kisa cha suluhu ya Hudaybiyah pamoja na makafiri, Mtume (S.A.W) akasema: {naapa kwa yule ambaye nafsi yangu iko mikononi mwake hawatataka mpango wanatukuza yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, isipokuwa nataitekeleza}. 
Na miongoni mwa aliyoyataja Ibn Al-Qayyim katika kitabu chake Zaad Al-Maad (269/3) kwamba miongoni mwa faida za kifiqhi katika suluhu ya Hudaybiyah aliposema: kwamba makafiri na watu wa uzushi na madhaalimu wakitaka amri wanatukuza yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu, wakajibiwa na wakapewa na watasaidiwa, na hata wakizuia jambo lengine watasaidiwa juu ya kutukuza yaliyoharamishwa na Mwenyezi Mungu tu sio juu ya ukafiri wao. Kwa sababu kila anayetaka kusaidiwa kuhusu jambo linalomridhia Mwenyezi Mungu, atasaidiwa bila ya kujali dini au ukoo wake. Na suala la kuangamiza Daesh linahakikisha jambo linalotakiwa na sheria, nalo ni kuzilenda damu za waislamu na mali zao.


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika


 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.