Kudai kwamba anayekanusha baadhi ya mambo ya dini basi atakuwa ni mkafiri

  • | Thursday, 10 August, 2017
Kudai kwamba anayekanusha baadhi ya mambo ya dini basi atakuwa ni mkafiri

Kwa mujibu wa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu: )Je! Mnaamini baadhi ya Kitabu na mnakataa baadhi yake? Basi hana malipo mwenye kutenda hayo miongoni mwenu ila hizaya katika maisha ya duniani, na Siku ya Kiyama watapelekwa kwenye adhabu kali kabisa. Na Mwenyezi Mungu si mwenye kughafilika na yale mnayo yatenda(, {AL-Baqarah}.
Suala la "kukanusha baadhi ya mambo ya dini linazingatiwa ni ukafiri", linaonyesha ujinga ulio wazi. Basi Al-salaf na Al-khalaf wamekubaliana kwamba dini siyo kitu moja, maana mtu anayekanusha swala si kama mtu anayekanusha adhabu ya kaburi, kwani anayekanusha swala ni mtu amekanusha nguzo miongoni mwa nguzo za Uislamu, na huyo si kama mtu anayekanusha adhabu ya kaburi ambapo wanazuoni wa kiislamu hawakusema kwamba atakayekanusha adhabu ya kaburi ni mkafiri, kwani labda anafuata maana.
Basi kabla ya hapo ingawa Al-Mua'tazilah wamekanusha adhabu ya kaburi, isipokuwa hakuna mwanachuoni wa kiislamu yeyote amesema kuwa kundi hilo la watu ni makafiri, kwa hivyo wenye elimu wanawazingatia Al-Mua’tazilah kama ni waislamu sio waasi-imani. Basi si kila mwenye kukanusha jambo miongoni mwa mambo ya dini hazingatiwi kama ni mkafiri isipokuwa akikanusha kitu kinachojulikana katika dini kuwa ni dharura. Na zaidi ya hayo aya hiyo wanaoitumia kama ni dalili iliyoteremshwa katika mayahudi kwani walivunja ahadi na wamekwenda mbali na mafundisho ya Taurati, Mwenyezi Mungu Akawatishia kuwapa adhabu. Ama anayehitilafiana katika fiqhi, kufuata maana na kujitahidi si miongoni mwa wanaoamini kwa baadhi ya Kitabu na wanakataa baadhi yake.


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.