Damu ya mkafiri ni halali!

  • | Monday, 14 August, 2017
Damu ya mkafiri ni halali!

Imekuja katika makali:
“ Uislamu ni dini ya misingi ya kibusara ambao umejengwa juu yake uadilifu wa kweli na utukufu . mmoja wa misingi hiyo kuwa ni lazima kupambana  na watu wote hadi wafuate Uislamu au wawe chini ya utawala wake (kupitia kutia saini mkataba wa kisheria pamoja  na waislamu). Msingi huo huharimisha kumwaga damu ya mwislamu na asiye mwislamu, mwenye ahadi na waislamu na anayehalalisha damu  ya wasio waislamu na wasiofungamani na waislamu kupitia mkataba wa kisheria. wamepokea  Bukhari  na Muslim toka kwa Ibn Omar (R.A) kwamba Mtume (S.A.W) Amesema: {Nimeamrishwa nipigane vita na watu mpaka washahidie kwamba hakuna Muabudiwa wa haki ila Allah  na kwamba Muhammad ni Mtume wa Allah, na wasimamishe Swala na watoe Zaka.  Watakapofanya hivyo, watakuwa wamepata himaya Kwangu ya damu zao, na mali zao isipokuwa  kwa haki ya Uislamu, na hesabu yao itakuwa kwa Allah Ta’aalaa(, na huo ni ufahamu usio sahihi kwa hadithi ya Mtume (S.A.W) ambao umejengwa juu yake mtazamo usio sahihi  unaohalalisha kuwapiga vita watu wote ila mwislamu au aliyepewa ahadi nao.
Kujibu fikra hiyo isiyo sahihi inakuwa  kwa kubainisha kwamba tamko la “watu” lililokuja katika hadithi ni tamko la kijumla linalokusudia watu maalumu kama ilivyokuja katika Qurani tukufu: {Al-Hajj:27} je watu wote ni waislamu ili waende  kuhiji Makkah ? hapana, basi neno “watu” linahusiana na waislamu tu. 
(na anazungumza na watu utotoni…) je Nabii Isa (A.S)  Amezungumza na  watu  wote? Hapana ,bali  alizungumza na  banii Israili tu hasa waliozungumza na Bibi Maryam(A.S) na kumtuhumu kwa zinaa.
Hivyo haiwezikani kusema kwamba miongoni mwa misingi ya Uislamu: kuwapiga vita watu wote hadi waingie Uislamu au wawe chini ya utawala wake kwani hiyo kinyume cha hadithi hiyo waliyoitumia kama dalili , basi mtume (S.A.W) amesema hivyo akikusudia maadui  waliompigana miongoni mwa washirikina na hakuwakusudia watu wote.


Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.