Kuwakafirisha baadhi ya waislamu na kuwasifu kama ni makafiri na walioritadi kwani hawakuunga mkono dola ya khilafa iliyojulikana kwa jina la Daesh

  • | Wednesday, 16 August, 2017
Kuwakafirisha baadhi ya waislamu na kuwasifu kama ni makafiri na walioritadi kwani hawakuunga mkono dola ya khilafa iliyojulikana kwa jina la Daesh

Hakika suala la imani na ukafiri katika Uislamu ni suala lililomo baina ya mja na Mola wake mlezi…. kama alivyotufundisha Mtume (S.A.W) kwamba tuamiliana na watu kwa matamshi ya ndimi zao, na wala hatuhukumu juu ya vitendo vya nyoyo za viumbe na wala hatuanzishi mahakama ya ukaguzi ili kujua muumini na makafiri, kwani hajui yaliyomo nyoyoni isipokuwa Mola mlezi wa walimwengu… hatuhukumu isipokuwa mambo yaliyo wazi, na Mwenyezi Mungu pekee yake anayewahisabu waja wake.
Ama yanayofanywa na makundi ya kigaidi hivi sasa miongoni mwa kumkafirisha kila anayehitilafiana nao, na kila asiyefuata mbinu wao wa kikatili basi ni mhalifu katika mtazamo wao. Watu hawa wanakwenda kinyume na mafundisho wazi ya Uislamu yanayohusiana na jambo hilo, kwa hivyo Mtume (S.A.W) amemtahadharisha mwislamu kumkafirisha mwenzake au kuhalalisha damu yake, mali yake na heshima yake.
Kundi la kikafiri linatoa istilahi ya kuritadi na ukafiri likikusudia umati wa waislamu wanaohitilafiana na rai na misimamo yao mikali ili kuhalalisha kuwaua na kuharibu nyumba zao! basi kutoka wapi watu hawa wamechukua mafundisho yao?! Na ilhali Mtume (S.A.W) ameainisha maana ya imani katika hadithi sahihi alipomwuliza Jibrili (A.S) Akasema: "imani ni kumwamini Mwenyezi Mungu, malaika wake, vitabu vyake, mitume wake, siku ya mwisho na kadiri kheri yake na shari yake", imepokelewa na Al Bukhari na Muslim, na pia umma wote wamekubaliana kwamba imani ni tendo la moyo, na haitoki kutoka kwake isipokuwa baada ya kukanusha imani iliyomo ndani ya moyo. Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "mtu yeyote atakayemwambia mwenziwe ewe mkafiri basi  mmoja wao anastahiki sifa hiyo" (sahih la-bukhari, 5/226).

 

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.