Tuhuma ya kuruhusia kupomoa misikiti inayo makaburi na kuhalalisha damu za wanaoyazuru, na kupomoa misikiti ya Mashia

  • | Saturday, 19 August, 2017
Tuhuma ya kuruhusia kupomoa misikiti inayo makaburi na kuhalalisha damu za wanaoyazuru, na kupomoa misikiti ya Mashia

Daesh na makundi mengine ya kigaidi yanadai kuwa kupomoa makaburi hasa yanayowafuata Wasufi ni halai, na wanahalalisha kumwaga damu za wanaoyazuru wakidai kwamba ni mahali pa kufuru na kuabudu masanamu.
Kwa upande mwingine, mmoja wa wanamgambo wa Daesh ametoa fatwa ya kuwajibisha wapiganaji wa makundi hayo kuishambulia misikiti yote ya Mashia ya Ismailia, akiifananisha misikiti hiyo kwa mahekalu ambayo masanamu yanaabudiwa ndani yake.


Kujibu tuhuma
Yakiwa makundi hayo yanahalalisha kumwaga damu za wanaozuru makaburi haya wakidai kwamba ni mahali pa kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na haijuzu kujenga misikiti juu ya makaburi hayo, basi makundi haya yanasema nini kuhusu kauli za wanachuoni kuhusu kuhalalisha kujenga juu ya makaburi ya maswahaba na wahenga wema? katika kitabu cha Imam "Al-Turbishti ala Al-Masabiih alisema: "mmoja wa wahenga wema amehalalisha kujenga juu ya makaburi ya wanachuoni na mashekhi mashuhuri, ili watu wawazuru na wapumzike kwa kukaa ndani yake".
Na mwanachuoni aitwaye Ali Ibn Ahmad Al-Hadaad amesema: "anayetangaza kuwa wananchi wa nchi zinazo na makaburi ni nchi makafiri, basi kwa kufanya hivyo anakuwa anawakafirisha wanachuoni wanaoishi sasa na waliotangulia katika zama kadhaa zilizopita, kwani maswahaba wa Mtume (S.A.W) -walijenga juu ya kaburi la Abi Busair- (R.A.) jengo na wakazindua msikiti, na Mtume hakulikataza tendo hilo na hakuwaomba kupomoa kaburi hilo.
Pia Mtume (S.A.W.) amewaambia maswahaba wake kuingia na kutawala upya Jerusalem, na amempa Tamim Al-Dari kipande cha Ardhi mjini Al-Khalil ili ahadi ya Mwenyezi Mungu ihakikishwe, na Mtume (S.A.W.) alikuwa anajua kwamba kaburi la Nabii Ibrahim, Isaac, na Jacob, na juu yake kuna hekalu na hakuwaamuru maswahaba wake wapomoe jengo lililojengwa juu ya kaburi la Nabii Ibrahim au manabii wengine waliokuwepo mjini Al-Khalil, Jerusalem, maana dalili hizo zinaonyesha kwamba zinatahadharisha kutoka sababu ya kujenga na sio kutoka jengo lenyewe.
Ama kuhusu upomoaji wa misikiti, basi misikiti ya Mwenyezi Mungu ina heshima inayoizuia kuibadilisha kwenye nyanja za vita na migogoro, kwani misikiti ni uti wa mgongo katika kuunda jamii yoyote ya kiislamu, na Mwenyezi Mungu ametuamrisha kujenga na kulinda misikiti na kutoishambulia ikiwa ya Masunna au Mashia, kwani kuishambulia inapelekea kufanya uharibifu ardhini: )na kwamba misikiti ni ya Mwenyezi Mungu, basi msiabudu mwengine pamoja naye(. {Al-Jinn: 18}, na pia Mtume Mohammad (S.A.W.) Amesema: (maeneo yaliyopendezwa sana na Mwenyezi Mungu ardhini ni misikiti yake).
Hakika kuvunja heshima ya misikiti ni uhalifu wa kinyama na hatari sana katika Uislamu, hivyo ikiwa sheria ya kiislamu inaharamisha kuzungumza wakati wa kutoa hotuba ya Ijumaa, bali wanachuoni wamesema kwamba mazungumzo wakati wa hotuba ni haramu hata yakiwa kwa lengo la kuamuru kwa wema au kukataza mabaya, basi je, hukumu itakuwa nini kuhusu kuvunja heshima ya misikiti? Kwa hakika kuishambulia misikiti kwa aina yoyote ni miongoni mwa ufisadi iliyo mbaya zaidi, Mwenyezi Mungu (S.W.) Amesema: (Na ni nani aliye dhaalimu mkubwa zaidi kuliko yule anayezuia misikiti ya Mwenyezi Mungu kutajwa ndani yake jina lake na akajitahidi kuiharibu? Watu hao haitawafalia kuingia humo ila nao wanaogopa. Duniani watapata hizaya na Akhera watapata adhabu kubwa). 

Kituo cha Al-Azhar cha kupambana na mawazo makali
Kitengo cha lugha za Kiafrika

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.