Daesh: kumpwekesha kuna Sehemu kadhaa, kama kupwekesha Hakimiyah, yaani kukiri kwamba hukumu ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba anayehukumiana kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi ni mkafiri

  • | Thursday, 28 September, 2017
Daesh: kumpwekesha kuna Sehemu kadhaa, kama kupwekesha Hakimiyah, yaani kukiri kwamba hukumu ni kwa Mwenyezi Mungu peke yake, na kwamba anayehukumiana kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu, basi ni mkafiri

     Al-hakimiyyah (Utawala) ni istilahi ya kisasa iliyotumiwa kwa mara ya kwanza na "Abu Al-Aa'la Al-Maududi" alipokuwa anajitahidi kupata uhuru wa nchi yake kutoka mkono wa ukoloni wa Uingereza, na wakati ilipopata Pakistani uhuru wake na kujitenga na India mwaka 1947, Al-Maududi alijitenga mbali na mawazo za Al-hakimiyyah "utawala" na amefuata kanuni na katiba ya nchi yake bali aliteua katika uchaguzi.
Baadaye Sayyid Qutwb aliichukua fikra ile ile akitumia istilahi yenyewe baada ya kuipachika kwa mawazo yake ya kiuharibifu ili aseme kupitia istilahi hiyo kwamba Misri ni nchi ya kiujinga inayoishi katika giza za ukafiri kwani haihukumiwi kwa sheria ya Mwenyezi Mungu Mtukufu.
Makundi ya kigaidi tangu Sayyed Qutwb mpaka siku yetu hii yanatumia istilahi hii ili kuhalalisha upotovu wao nje ya njia iliyonyooka kwa lengo la kuwauwa wasio na hatia na kuharibu tamaduni wakidai kwamba hakuna hukumu isipokuwa kwa Mwenyezi Mungu na kwamba ni lazima kutekeleza sheria ya Mwenyezi Mungu katika ardhi.

 

Print
Tags:
Rate this article:
5.0

Please login or register to post comments.