Udugu wa Manabii na Uislamu wa kimataifa (1)

Umuhimu wa kuwaamini Mitume wote

  • | Wednesday, 18 October, 2017
Udugu wa Manabii na Uislamu wa kimataifa (1)

      Jambo lisilo na shaka ni kwamba Manabii ni wadugu, na sisi waislamu -wafuasi wa Mtume Mohammad (SAW)- tunawaamini wao wote, bila ya kutofautiana baina yao, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: {Mtume ameamini yaliyoteremshwa kwake kutoka kwa Mola wake, na Waislamu, wote wamemwamini Mwenyezi Mungu, na Malaika wake, na Vitabu vyake, na Mitume yake, Hatutafautishi baina ya yoyote katika Mitume yake, Tumesikia na tumetii, msamaha Mola wetu! Na marejeo ni kwako}, (Al-Baqarah:285)
      Kwa hiyo, mtu akimkadhibisha Mtume mmoja basi anakuwa amewakadhibisha Mitume wote, kwani asili ya ujumbe wa Mitume wote ni mmoja, nayo ni (hapana mungu anayestahiki kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu), kama alivyoeleza Mwenyezi Mungu katika Qurani, ambapo Alisema: {Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani}, na Amesema: {Na hatukumtuma kabla yako Mtume yeyote ila tulimfunulia ya kwamba hapana mungu isipokuwa Mimi. Basi niabuduni Mimi tu}.
      Na pia Mwenyezi Mungu Ametangaza katika Surat Ash-shu’araa kwamba kumkadhibisha Mtume mmoja ni kama kuwakadhibisha Mitume wote, kama Alivyosema Mwenyezi Mungu: {watu wa Nuhu waliwakadhibisha Mitume}, na inajulikana kwamba watu wa Nabii Nuhu walimkadhibisha Mtume Nuhu peke yake, lakini kumkadhibisha Mtume mmoja inamaanisha kuwakadhibisha Mitume wote, kwa sababu Mitume wote wana ujumbe mmoja, na wanaita kufuata dini moja, na Aliyewatuma ni mmoja naye ni Mwenyezi Mungu, kwani lengo na jukumu lao ni moja, aliyetangulia kutumwa miongoni mwao anabashiri kwa ujio wa anayetumwa baadaye, na anayetumwa baadaye anaamini aliyetumwa kabla yake.
      Kwa hiyo kuwaamini baadhi ya Mitume na kuwakufuru kwa baadhi yao ni kama kuwakufuru wao wote, Mwenyezi Mungu Amewasifu watu hao Akisema: {Hakika wale wanaomkataa Mwenyezi Mungu na Mitume wake, na wanataka kufarikisha baina ya Mwenyezi Mungu na Mitume wake, kwa kusema: Wengine tunawaamini na wengine tunawakataa. Na wanataka kushika njia iliyo kati kati ya haya}, (Al-Nisaa:150), kama Amesema pia: {Na waliomuamini Mwenyezi Mungu na Mitume wake, wala wasimfarikishe yeyote kati yao, hao atawapa ujira wao. Na Mwenyezi Mungu ni Mwingi wa maghfira, na Mwenye kurehemu}, (Annisaa’:152).

 

Print
Tags:
Rate this article:
No rating

Please login or register to post comments.